MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA
SOMO: 2 WAFALME 5:1-8
Mungu amepanga kila mmoja kupata baraka kupitia kwa wasaidizi wa hatima. Naamani alisaidiwa na kijana mwanamke asiyetoka nchi ya Israeli. Huyu kijana mwanamke alikuwa mtumwa.
- Mungu pekee anawainua watu kupitia watu wengine. Mungu anawabariki watu kupitia watu.
- Usaidizi wa Mungu unapitia watu wanaoinuliwa na Mungu kukusaidia. Hawa watu wanaoinuliwa na Mungu kukusaidia wanaitwa wasaidizi hatima (destiny helpers).
- Uwezo wako kugundua, kupokea, kudhamini, kuhifadhi na kusheherekea watu waliotumwa kwako kukusaidia ni jambo la busara kwako mwenyewe.
- Watu wengi wanatekeleza katika maisha si kwa sababu ya kukosa elimu na maarifa, lakini wanakaa mbali na wasaidizi hatima waliotumwa kwao na Mungu.
- Safari ya kufikia hatima yetu katika Bwana itakuwa rahisi kupitia ushauri, urafiki, ushirika na ufahamu wasaidizi wanaotumwa na Mungu kwako, katika kila hatua ya safari yako duniani.
- Mungu hakupangia Naamani kufa kama mwenye ukoma-lakini usaidizi wake utapitia kwa kijana mwanamke-mtumwa katika nyumba yake.
- Msaidizi hatima si lazima awe tayari, mtu mkuu, msomi, mwenye kujulikana, mashuhuri, lakini awe chombo kilichopangwa na Mungu kutimiza jambo kuu katika hatima na maisha yako. Hebu tuone:-
HAINA ZA WASAIDIZI HATIMA (Kinds of destiny helpers).
- Ni lazima utambue haina mbali mbali ya wasaidizi hatima na kujiweka katika hali na mahali pa kuwapokea ndiposa uyapokee yote kutoka kwao.
- Mwenye kushikanisha (the connectors).
- Hawa ni watu wanao uwezo wa kukuunganisha na watu walio na uwezo na kuchangia maisha na hatima yako.
- Huyu kijana mwanamke mtumwa katika nyumba ya Naamani alikuwa connector katika Naamani na Elisha.
- Kuna uhusianao madhubuti katika tabia yako na nafasi utakayo pata katika maisha yako.
- Tabia zako na nafasi (opportunity) zako zinaenda pamoja.
- Walimu na washauri (role models and mentors).
- Hawa ni watu walio na uwezo na ujuzi na uzoefu wa kufahamu unachohitaji kufikia hatima yako katika Mungu.
- Uaminifu wako, unyenyekevu wako katika uhusiani wenu utachangia sana kwa kile utapata kutimiza hatima yako.
- Kwa mfano, Musa na Yoshua, Elisha na Eliya, Timotheo na Paulo, Yoshua na Kalebu.
- Wadhamini (the sponsors) wafadhili.
- Hawa ni watu ambao Mungu amewatuma kukulipia kutimiza ndoto zako zote hau sehemu.
- Hawa wanaweza kulipa gharama za maisha yako, miradi yako.
- Yesu Kristo alikuwa na wafadhili, wanawake wakuu kama jinsi Susana, Mariamu, Yusufu wa Arimathea, Nikodemu.
- Mwenye kupendekeza, mashabiki (the recommenders).
- Hawa ni watu watakao pendekeza kwa wale wasiokufahamu hau mahali sauti yako haiwezi kusikizwa.
- Yusufu alipendekezwa kwa farao, Daudi alipendekezwa kwa mfalme Sauli.
- Onesimo alipendekezwa kwa Filemoni na mtume Paulo-Filemoni 1:8-20.
- Kuna watu hawataweza kukufahamu bila kushabikiwa.
- Kujua watu wanaoweza kukushabikia ni jambo bora sana.
- Waombezi (the intercessor)
- Hawa ni watu wanaokuombea kwa moyo safi na upendo.
- Hawa wanakuombea ili mipango ya Mungu juu ya maisha yako ikatimie.
- Yesu Kristo alimwombea Petro.
- Wakuu wa kiroho, maaskofu (the overseers).
- Hawa ni watu wanaojipa jukumu juu ya maisha yako kwa wema.
- Hawa wakuu wanakuombea, wanatoa unabii juu ya maisha yako na ndani ya maisha yako.
- Hawa wanakushauri, wanakutia moyo kwa neno la Bwana.
- Hawa wanauwezo wa kukukemea na kukuonyesha njia za Mungu.
- Washikadao (partners).
- Hawa wanafanya kazi ya maisha pamoja nawe.
- Mke au mume wako ni mshiriki pamoja nawe katika safari ya maisha.
- Kuchagua mume au mke ni jambo na uamuzi wa hatima.
- Ndoa inabadilisha maisha ya mtu daima!!
- Pia washiriki katika biashara, huduma.
- Unapopanga maisha yako usiwausishe watu wasiofaa, watakusumbua katika maisha na hatima yako.
- Mfano ni Paulo na Sila na Barnabasi katika huduma, Prisilana Akila katika ndoa na biashara.
- Wanaokuhudhi (the persecutors).
- Hawa ni watu wanaokusudia kukufanya mabaya, hawa hawakutakii mema.
- Lakini hawajui kwamba Mungu atatumia chuki na wivu yao kukubariki.
- Yusufu na ndugu zake, Hannah na Peninah, Mordecai na Haamani.
SABABU ZA KUOMBEA WASAIDIZI WA HATIMA.
Kila mtu anahitaji kusaidiwa kwenda haraka na mbali katika safari ya maisha.
- Shetani anaweza zuia wasadizi wako kwa kuwafanya adui au wasionekane.
- Shetani alileta dhoruba katika bahari ya Galilaya ili mtu mwenye pepo (legion) asikombolewe-Marko 5:1-10.
- Shetani anaweza kukufanya kudhihaki wasaidizi wako.
- Naamani alikuwa karibu kukosa uponyaji wake kwa sababu nabii Elisha alikosa kumwona na kumlaki-2 Wafalme 5:11-14.
- Wakati mwingine wasaidizi wako wanaweza kuwakilishwa na shetani.
- Tabia ya Mordekai na heshima zake ziliaribiwa na Naamani mbele ya mfalme.
- Tena wasaidizi wako wanaweza kutumiwa na shetani wasikusaidie.
- Tambua, kwa watu Mungu ameweka katika maisha yako na katika kila musimu wa maisha kukusaidia ikafikie hatima yako katika Bwana.
- Omba sana wasaidizi wako wakakufikie.
MWISHO
- Ombea wasaidizi wako wakafunuliwe kwako.
- Omba wasaidizi wako wakakufikie.
- Omba Mungu akufunulie wewe ni msaidizi wa nani.
- Omba, ukatimize hatima yako katika Bwana.