MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.
SOMO: DANIELI 7:1-28.
Katika siku hizi tunaona kama watu wa Mungu wanaendelea kupoteza. Lakini usife moyo. Jipe moyo na ujasiri katika ushindi mkuu unaokuja, na uwe tayari, Yesu Kristo anaokuja kutupa ushindi huo. Katika dunia inayoongozwa na wanyama hakuna usalama. Hakuna usalama katika mwanadamu, bali unatoka mbinguni. Usalama hauletwi na mwanadamu, bali unatoka mbinguni. Usalama unatoka mbinguni, utapata kuwa salama tu unapoingia katika ufalme wa Yesu Kristo, ufalme usioweza kuharibiwa-Danieli 7:13-14.
Danieli aliota ndoto. Katika ndoto yake Danieli aliona falme za wanyama (wanadamu) ambazo ni historia ya dunia hii na falme zake. Mwishowe Danieli aliona kurudi kwa mwana wa Mungu (Yesu Kristo) na ufalme usio na mwisho pia katika ile ndoto Danieli ameona hukumu ya mwisho katika kile kiti kikubwa cheupe cha hukumu.
Kitabu cha Danieli kinao sehemu mbili, mlango 1-6 ni visa vya Danieli, vijana watatu wa Kiebrania mfalme Nebukadreza na mfalme Belshaza na hukumu ya Mungu juu yake, “Mene Mene Tekeli Persi.” Mlango 7-12, ni sehemu juu ya unabii. Kunao maono manne. Unabii wa Danieli sehemu umetimia, bado kunao sehemu bado kutimia-Daniei 12:9.
Kuna onyo mbili juu ya unabii.
- Usishikwe na unabii kiasi kukosa mwelekeo na kukosa kuona picha iliyo kuu.
- Usiogope unabii kiasi kukataa kusoma unabii na vitabu vya unabii. Biblia enyewe ndio tafsiri kuu juu ya unabii. Mungu mwenyewe ndiye nabii na unabii-Isaya 46:10. Hebu tutazame:-
FALME NNE (4) ZA DUNIA-(Danieli 7:1-7, 17).
- Falme nne za dunia zilitoka baharini ya wanadamu.
- Falme hizi nne zinaakilishwa na wanyama wanne.
- Leo tunatazama historia miaka 2,500 tangu Danieli. Leo sisi tunaelewa vyema zaidi kuliko Danieli, maana hizi falme tayari zimekwishapita.
- Ufalme ule wa nne ndio wa maana zaidi kwetu, kwa maana falme tatu za kwanza zimepita.
- Simba/Tai-Babeli-Danieli 7:4.
- Ishara ya simba aliyekuwa na mabawa ya tai ni ishara ya ufalme na enzi ya Babeli chini yake mfalme Nebukadreza.
- Danieli aliangalia mpaka manyoya ya mabawa ya yule simba yalifutika, Maanake nguvu na mamlaka yake yalipunguzwa sana.
- Kumbuka kwamba nguvu, sifa na heshima yake mfalme Nebukadreza ilipunguzwa sana wakati Nebukadreza alifanyika kuwa mnyama kwa miaka saba.
- Enzi ya Babeli ilikuja na kupita!!
- Dubu: Mdo-Yuajemi (7:5) Medo-Persia).
- Wamedo na Wajemi (Medo-persia) ilikuwa ufalme wa enzi yake Dario.
- Ufalme huu ulikuwa umekaliwa na Wafalme wawili-Wamedi na Waajemi. Lakini Wajemi walikuwa na nguvu zaidi ya Wamedi.
- Mifupa mitatu ya mbavu ilikuwa katika kinywa cha yule dubu ni ushindi tatu waliopewa Waajemi Lydia katika Asia minor.
- Babeli chini ya Nabonidus, Misri chini ya Psamtik.
- Chui: Wagiriki (Greek)-7:6.
- Chui anajulikana sana kwa mwendo wa kasi (speed).
- Wagiriki waliwashinda Wamedi na Waajemi kupitia kwa mfalme Alexander the Great.
- Kwa miaka kumi pekee Alexander the Great kutoka Macedonia aliwashinda vita na kumiliki Asia Minor, Babeli, Misri, Syria, Persia, India Afrika yote Uchina na karibu Europa yote.
- Katika mwaka wa 323BC akiwa na miaka 33, Alexander alikufa huko Babeli kwa homa kali. Alikuwa akirudi toka vitani Mashariki ya mbali.
- Wana historia wengi wanasema Alexander the Great alikuwa mlevi sana, kwa majeraha huko India, homa iliposhika yeye alikufa.
- Mabawa manne aliyekuwa nayo yule chui ni majenerali wake wanne walio miliki enzi yake Alexander the Great.
- Mnyama wakutisha sana-Roma 7:7-8.
- Maono na ndoto ya Danieli inaenda sambamba na maono yake Nebukadreza katika mlango wa pili.
- Nebukadreza aliona sanamu kubwa sana, kichwa-dhahabu-Babeli=simba.
Kifua cha fedha-Wamedi-Waajemi=Dubu.
Tumbo la shaba-Giriki (Greek)-chui.
Miguu-chuma-Roma=Mnyama wa kutisha sana.
- Kwa nini Mungu amerudia ndoto hii na maono haya?
- Hili Mungu apate kusisitiza umuhimu wa falme hizi zote, katika historia ya ulimwengu.
- Mungu apate kutufafanulia zaidi juu ya mnyama huyu wa nne.
- Ufalme huu wa nne haujatajwa jina lake na Wafalme wake.
- Katika maka wa 550BC wakati wa Danieli, Roma ilikuwa mji mdogo sana katika mto wa Tiber.
- Mnyama wa nne anao meno kali-maanake jeshi lake lina nguvu sana.
- Danieli alionyeshwa ufalme huu wa Roma, wakati uliopita na wakati ujao.
- Ufalme wa Roma ulitapakaa sana kutoka Uingereza (Britain) mpaka Uchina na Japan, Afrika, Asia.
- Ufalme huu wa nne pia unaenda pamoja na maono ya Ufunuo 17:12-14.
- Danieli aliona baada ya siku yule mnyama wa nne alimea “pembe ngodo” itakayo tawala zile pembe kumi.
KUINUKA NA KUANGUKA KWA MPINGA KRISTO-7:8, 11, 21-25.
- Mpinga Kristo (anti-Christ)-Ufunuo 13:1-7 alionekana na nabii Danieli akishinda vita juu ya wateule (Wakristo).
- Katika Danieli 9, kutatokea mtu, kwanza ataingia kuleta amani duniani, lakini baada ya miaka tatu na nusu atageuka kuwa mtu wa vita kali.
- Huyu mpinga Kristo atakuwa mwanasiasa na pia mwenye vita. Akili zake zitapita akili za wote duniani.
- Huyu mpinga Kristo atakuwa mnenaji mkuu, usawishi wake juu ya watu wa mataifa yote utakuwa wa juu zaidi, kila mtu duniani atapenda huyu mtu.
- Huyu mpinga Kristo atakuwa na usemi kama jina Julius Ceaser, Napoleone Bonaparte, Adolph Hitler, Joseph Stalin na Sadam Hussein ndani ya mtu mmoja!!
- Mpinga Kristo bado hajafika duniani, lakini roho yake mpinga Kristo imo duniani tayari-1 Yohana 4:3.
- Mwisho wa ulimwengu uko karibu zaidi leo kuliko jana!!
KURUDI KWA YESU KRISTO NA UFALME WAKE-Danieli 7:13-14, 26-27.
- Katika maono ya Danieli (Dan. 2) Yesu Kristo ameonyeshwa kama (jiwe lililokatwa mlimani bila mkono wa mtu). Jiwe lile lilipiga ile sanamu (falme za mataifa).
- Katika Danieli 7:13, tunaona katika maono ya Danieli lile jiwe sasa limeitwa “mwana wa Adamu) Danieli 7:13, Marko 14:62.
- Danieli 7 inasema “Mwana wa Adamu” atarudi katika mawingu atamshinda yule mpinga Kristo na kuanzisha ufalme wake wa miaka 1,000 na baadaye milele na milele-Ufunuo 19:11-12; 19-20.
HUKUMU WA MWISHO-Danieli 7:9-10.
“Mzee ya siku” Maanake sio mzee wa uzee (mkongwe) lakini Maanake ni “milele, au asiye na umri.”
- Mungu si “Mzee” lakini ni “Mungu wa milele” Zaburi 90:2, Alpha na Omega”-Ufunuo 1:8, 17.
- “Mzee wa siku” ni Mungu katika utatu wake (Holy Trinity). Baba, Mwana na Roho.
- Mavazi meupe Maanake ni utakatifu, nywele nyeupe Maanake si uzee lakini utakatifu wake-Ufunuo 1:14.
- Danieli 7:10, mto wa moto-Mungu ni moto ulao-hukumu.
- Mungu anatumikiwa na maelfu juu ya maelfu ya watumishi.
- Hukumu zake ni hukumu za kweli vitabu vilifunguliwa-Ufunuo 20:11-15.
- Hukumu hii ni hukumu juu ya wale wasiookoka, wale wamekufa kiroho.
- Ikiwa umeokoka huwezi kuwa katika hukumu hii.
- Vitabu ni vitatu:
- Kitabu cha Matendo-Mathayo 12:36.
- Biblia-Yohana 12:48.
- Kitabu cha uzima.
- Mtu anapookoka jina lake linaandikwa katika kitabu cha mwana kondoo-kitabu cha uzima wa milele-Mathayo 7:21.
- Siku moja, kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri Yesu Kristo-lakini kwa wasiookoka itakuwa wamechelewa-Wafilipi 2:10-11.
MWISHO.
- Je, jina lako liko katika kitabu cha Mwana kondoo, kitabu cha uzima?
- Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake, “furahini kwa maana majina yenu yameandikwa katika kitabu cha uzima, kitabu cha Mwana kondoo.”
- Yesu Kristo yuarudi, je, umeokoka?
Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)
- DIVINE INTERVENTION IN DESTROYING THE YOKE OF DELAY. - March 26, 2025
- KUGUZWA UPYA - March 23, 2025
- “LIVING DOGS AND DEAD LIONS.” - March 23, 2025