SOMO:  WAEBRANIA 11:1-7

UTANGULIZI

Kila mtu anayo Imani kiasi Fulani. Kila siku sisi zote tunatumia Imani. Unapoakisha taa unayo Imani kwamba mwangaza utatokea. Unapoingia gari unayo Imani utafika uendako, unapotumana barua unayo Imani itafika  kwa anwani yake. Katika maisha ya Roho, wengine Imani yao imo katika korani na mitume, wengine Imani yao imo katika kuzaliwa mara nyingi na katika Nirvana. Wengine Imani yao  imo ndani ya Nafsi zao na katika matendo yao mema, Lakini kiini hasa cha Imani ni tengemeo lenyewe. Sisi tuliookoka Imani yetu imo katika Kristo Yesu (Matendo 4:12)

Leo tutazaame mambo mawili, Imani ni nini? Na jinsi Imani inafanya kazi. Hebu tujifunze:-

I. IMANI NI NINI ? (Waebrania 11:1-3)

Watu wengi wanaelewa Imani kimakosa.

  1. Kuna wale wanafikiri Imani ni kumlazimisha Mungu. (Health and wealth or prosperity gospel)
  2. Kuna wale wanafikiri, Imani ni kushika mafundisho Fulani, lakini Paulo anasema (2 Timotheo 1:12).                                        Imani Lazima iwe katika mtu.
  3. Kuna wale wanaamini Imani ni kujitupa katika giza-hivyo Imani ni kinyume cha sayanzi.
  4. Kuna wengine wanao amini kwamba Imani nikujitoa kabisa kumfuata mtu hau jambo Fulani.
  5. Biblia inasema “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyooneka” (11:13-3)
  6. Imani ya kweli ni utii wa ujasiri kwa neno la Mungu, bila kutengemea hali hau matokeo yake.
  • Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo
  • Imani ni bayana (Evidence) ya mambo yasiyoonekana.
  • “Hakika “ (GK=hupostasis) maana yake ni “Kusimama juu ya msingi imara “
  • Hivyo Imani ni msingi unaotupa udhabiti wa kusimama.
  • Imani inatuwezesha kuchukua mambo yajayo , mambo yasiyonekana kama yatatendeka tayari.
  • Hivyo Imani ni bayana (evidence) ya mambo yasiyoonekana.

II. JINSI IMANI INAFANYA KAZI YAKE (Waebrania 11:4-7)

  1. Kwanza, Imani ya kweli inamuabudu Mungu-Habili (11:4)
  • Habili kwa Imani alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini. (Mwanzo 4:3-7)
  • Mungu anatafuta wanao abudu katika kweli na katika Roho (Yohana 4:24)
  • Ukweli unakuja kupitia ufunuo
  • Imani ya kweli inatafuta nafasi ya kuabudu

     2. Pili, Imani ya Kweli Inatembea na Mungu. Henoko (11:5-6) (Mwanzo 5:4).

  • Henoko aliishi katika wakati na kizazi mbaya Zaidi.
  • Lakini Henoko aliishi maisha safi na takatifu.
  • Henoko alitembea na Mungu.
  • Henoko hakuanza maisha yake kutembea na Mungu.
  • Kwa miaka ya kwanza (65)
  • Lakini alipoamzaa Methusela alianza kutembea na Mungu. (Miaka 300)
  • Henoko alitembea na Mungu siku zote-Mbaya na nzuri. (Mwanzo 5:21-24)
  • Henoko alimpendeza Mungu (11:6)
  • Imani ndio njia pekee ya kumpendeza Mungu.

    3. Tatu, Imani ya Kweli inamtumikia Mungu– Nuhu (V.7)

  • Dhambi ilizidi wakati wa Nuhu (Mwanzo 6:5,11)
  • Dhambi inapozidi Neema ya Mungu, inazidi pia
  • Nuhu alisimama pake yake (Mathayo 24:37-39)
  • Nuhu alijenga safina kwa maana alimwamini Mungu.
  • Je, Kazi yako inaonyesha Imani yako?
  • Kwa miaka izo Nuhu alijenga safina (6:15)

 

MWISHO

¨ Imani itakupa bayana, na hakika , kumwabudu Mungu kama jinsi Habili.

Kutembea kama Henoko na kutumika kama Nuhu.

 

root

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

2 days ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

2 days ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

2 days ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

6 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago