Categories: Swahili Service

KUNYAKULIWA KWA KANISA

SOMO: MATHAYO 24:1-34

 

Tangu Adamu na Hawa kuumbwa mpaka leo ni jumla ya miaka 5,786 kulingana na kalenda ya Wayahudi. Kuna wakati Mungu atakamilisha dahari (close of this age). Huu ni wakati ambao dhiki kuu itaisha. Kabla ya dhiki kuu kuanza, kutakuwa na unyakuo (rapture of the church).

Bwana alipaa mbinguni kwenda kutuandalia makao-Yohana 14:2-3. Je, Bwana atarudi?

    • Matendo 1:9-11, Bwana Yesu atarudi jinsi vile alipaa mbinguni.
    • 1 Wathesalonike 4:16-17, Bwana atarudi hapa duniani.
    • Mathayo 26:64, Bwana akamjibu kuhani mkuu, “mtamwona Mwana wa Adamu akirudi mawinguni.”
  • Juda 1:14, “Enoko akasema namwona Bwana akija na watakatifu wake maelfu kwa maelfu.”
  • Ufunuo 1:7, “Yuaja mawinguni na kila jicho litamwona.”
  • Ufunuo 22:12, “Tazama naja upesi na ujira wangu mikononi.”

Mengi zaidi kuhusu ukamilifu wa dahari hii:-

UNYAKUO WA KANISA-Mathayo 24:7.

  • “Unyakuo” yamaanisha kuchukuliwa kwa ghafla. Ijapokuwa hili neno lenyewe “kunyakuliwa” (rapture) haiandikwi kwenye maandiko lakini maandiko yafundisha kila wakati ya kuwa Bwana atarudi kulichukua kanisa lake, Bwana harusi anapomjia bibi harusi.
  • Hakuna mwanadamu ajuaye ni siku gani Bwana atarudi lakini Bwana alituachia ishara nyingi kuonyesha majira yanayozingira unyakuo wa kanisa.
  • Tetemeko za ardhi zitatokea kwa wingi zaidi tunapokaribia unyakuo wa kanisa. Sasa hivi mwaka huu wa 2025 zimetokea tetemeko nyingi za ardhi katika dunia.
  • Magonjwa. Magonjwa ya kawaida yamekuwa duniani lakini magonjwa mapya kama vile Covid-19, ukimwi, ebola na kadhalika yazidi kutokea duniani.
  • Njaa-watu kama milioni 350 wakabiliwa na njaa leo. Hapa Kenya njaa hutokea mara nyingi.
  • Vita zimetokea. Kwa miaka 120 iliyopita kumetokea vita vya dunia mbili. Sasa hivi vita vyaendelea duniani katikati ya Ukraine na Urusi, Israeli na Wapalestina, D.R.C, Sudan kusini, India na Pakistan na kadhalika.

VITA YA GOGU NA MAGOGU-Ezekieli 38 na 39.

  • Ezekieli 37 ni unabii kuhusu kuzaliwa upya kwa taifa la Israeli baada ya kuangamia kwa miaka 1,877 kutoka A.D 70 mpaka A.D 1,948. Kwa hiyo miaka hapakuwa taifa la Israeli duniani. Mti mtini ambao Bwana alitaja ulichipuka na matawi, ukachanua-Mathayo 24:32-34. Kizazi kilichoona kuchanua kwa huu mtini (fig tree) hakitapita kabla Bwana harusi kurudi.
  • Ezekieli 38 na 39 yaeleza kuhusu vita kali katikati ya Israeli na Iran (Persia), Urusi, Uturuki, Sudan na mataifa mengine ya kiarabu. Juzi Israeli ilipigana na Iran mwezi mmoja uliopita, lakini Iran itajiandaa tena ikishirikiana na mataifa yaliyotajwa na Ezekieli 38 na watashambulia Israeli.

KUJENGWA KWA HEKALU HAPO JERUSALEMU.

  • Kutoka mwaka wa A.D 70 mpaka leo hapajakuwa na hekalu la kumuabudu Mungu kwa Wayahudi.
  • Bwana Yesu alisema ya kwamba baada ya kanisa kunyakuliwa patakuwa na kipindi cha miaka saba duniani ya dhiki kuu.
  • Wakati wa dhiki kuu mpinga Kristo (Anti-Christ) ataingia hekaluni Yerusalemu na atawalazimisha Waisraeli kumuabudu-2 Wathesalonike 2:4.
  • Wakati huu Wayahudi wamejiandaa kujenga hilo hekalu tena. Wamechanga pesa, wameandaa makuhani watakaotumika katika sadaka ndani ya hekalu, wamechanga pesa ya kujenga hilo hekalu na wametayarisha ndama wa kutakasa makuhani na hekalu.

MWISHO

  • Ishara zote zaonyesha Bwana anarejea karibuni. Je, umeosha mavazi yako kukutana na Bwana harusi?
The following two tabs change content below.

Geoffrey Munyae

Latest posts by Geoffrey Munyae (see all)

Geoffrey Munyae

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago