MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI
SOMO: 1 SAMWELI 16:1-13
Huu ni ujumbe wa kwanza katika mfululizo wa ujumbe huu juu ya maisha na nyakati zake Daudi. Hakuna maisha ya mtu anayelinganika na maisha ya Daudi.
- Maisha ya Daudi ni maisha ya ukuu na pia maisha ya kawaida.
- Daudi alikuwa mtu shujaa na pia mtu mwoga.
- Daudi aliishi katika ushirika na Mungu na pia ushirika na mbinu za shetani.
- Daudi alikuwa mtakatifu na pia mtu wa kawaida sana.
- Mungu huwatumia watu wa kawaida kama wewe na mimi- 1 Wakorintho 1:26-31.
Hebu tujifunze:-
JINSI DAUDI ALIPOKEA UPAKO WAKE
Sauli- mtu aliyetupa mbao! – 1 Samweli 16:1-3.
- Moyo wa Samweli ulivunjika kwa maana Mungu amemkataa Sauli kuwa mfalme Israeli.
- Mfalme Sauli alikuwa chaguo la watu lakini chaguo lao halikumpendeza Mungu.
- Mfalme Sauli alikuwa amemwasi Mungu mara tatu hivyo Mungu alimtema mfalme Sauli.
- 1 Sam.13- Sauli alimwasi Mungu kwa kutoa dhabihu wakati Samweli alichelewa kufika kwa ibada mle Gilgali- 1 Sam.13:5-14.
- 1 Sam. 14- Mfalme Sauli alitoa nadhiri ya haraka juu ya Jonathani- 1 Sam.14:24-31.
- 1 Sam.15- Mfalme Sauli alimwasi Mungu kwa kutomwangamiza mfalme Agagi.
- Alipoulizwa juu ya kumwasi Mungu, mfalme Sauli alitoa vijisababu vingi- 1 Sam.15:24-25.
- Sauli alikuwa mtu bila msimamo kamili, alikosa tabia.
- Sauli alikuwa mtu wa hofu nyingi hivyo aliwapendeza watu kuliko Mungu!!
- Sauli alifanya yaliyo mema machoni mwake, si mbele ya macho ya Mungu.
- Sauli alikuwa mtu wa kuchanganyikiwa kuliko udhabiti wa tabia na mwelekeo.
- Jinsi alivyo endelea kuishi hapa duniani, ndivyo alivyotenda maovu mbele ya Mungu.
Mungu alimtuma Samweli kwa nyumba ya Yesse.
- Mungu alimwambia Samweli, kumwombolezea mfalme Sauli yatosha- 1; 16:1.
- Mungu tayari alikuwa na mtu wake pembeni- 16:10.
- Mungu anajali sana tabia kuliko heshima za wanadamu na maneno matupu.
- Samweli alipendezwa sana na Eliabu lakini Mungu alitizama ndani mpaka roho ya mtu.
- Pia Samweli alivutiwa na Abinadabu na Shama na ndugu zao. Lakini Mungu kumbe anatazama roho ya mtu na tabia kuliko sura na umbo- 16:7-10.
Daudi aliletwa kutoka malishoni.
- Mungu anayatumia malisho ya kila aina kuwaandaa watu wake kwa kazi yake.
- Mfalme kutoka kwa malisho.
- Yusufu kutoka shimoni na gerezani.
- Gideoni naye alikuwa amejificha katika pango.
- Musa alikuwa jangwani.
- Eliya alikuwa milimani ya Efraimu.
- Elisha naye alikuwa shambani akilima.
- Mungu kwanza anatujaribu na kazi ndogo ndogo kabla hajatupa kazi ya juu zaidi.
- Mungu anatumia huduma ya chini kabla ya huduma ya juu zaidi kutengeneza mioyo yetu.
- Daudi alichukuliwa bure na ndugu zake na pia baba yake- 1 Sam.16:11-13.
- Daudi alikuwa ndiye wa heshima ya chini zaidi katika nyumba ya Yesse.
- Lakini Mungu alikuwa anatazama roho na moyo wa Daudi.
JE, MOYO WA DAUDI ULIKUWA AJE?
- Zaburi 15:1-3- Moyo wa kweli, ukamilifu, haki.
- Zaburi 23:1-6- Moyo wa kumwamini Mungu- 14:1.
- Zaburi 26:2- Moyo uliofunguliwa- Zaburi 139:23.
- Zaburi 37:4-5- Moyo unaomtarajia Mungu na kumtegemea.
- Zaburi 40:8- Moyo unaomkumbuka Mungu.
- Zaburi 51:10, 17- Moyo unao tubu dhambi.
- Zaburi 131:1- Moyo unao nyenyekea Mungu.
MOYO WA MWANADAMU KATIKA BIBLIA
- Mungu anapomtafuta mtu, kwanza anapeleleza moyo wake. Haijalishi utaalamu, talanta, masomo, umbo, ujuzi na urembo la mtu.
- Mioyo ni ya namna nyingi sana;-
Ovu- Mwanzo 6:5-6.
Kutoamini- Mwanzo 17:17.
Hofu- Mwanzo 42:28.
Ngumu- Kutoka 7:13-14, 22.
Hekima- Kutoka 28:3; 35:10, 1 Wafalme 3:12.
Kukata Roho- Hesabu 32:7.
Kuelewa- 1 Wafalme 3:12; 4:29.
KWA NINI MOYO WA MTU NI WA MAANA?
- Kwa maana moyo ndio maskini na makao ya maisha yetu.
- Mwanadamu anaishi katika moyo wake si katika nyumba yake.
- Mioyo yetu ni uwanja wa mashindo ya Mungu na shetani.
- Hivyo Mungu anatazama roho na moyo wa nyumbani, alipotazama moyo wa Daudi Mungu aliona:-
- Moyo wa ushujaa.
- Moyo wa ibada na sifa.
- Moyo wa kuuishwa (restorer).
- Moyo wa ufalme.
- Moyo wa kumpenda Mungu na neno lake- Zaburi 19.
MWISHO
- Je, moyo wako ukoje?
- Wengine wako na mwili na umbo lakini mioyo yao ni sumu.
- Bwana nipe moyo safi.