Swahili Service

SIMBA KATIKA TUNDU LA DANIELI!!

MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 6:1-28

 

Danieli anatupatia mfano mwema wa jinsi ya kuishi maisha. Danieli alikuwa mtu wa Mungu katika nchi ya kigeni, tamaduni za mwanadamu bila Mungu. Sisi nasi tunaishi katika nchi ambayo Yesu Kristo na Ukristo zinapingwa sana kila kuchao.

Katika mlango wa kwanza, Danieli alikataa kula chakula cha mfalme na ile divai yake. Danieli alichagua kula mtama na maji pekee. Mlango wa pili mfalme Nebukadreza aliona ndoto ya yule sanamu mkuu katika uwanda ule wa ndura, Maanake ni falme zote za Wayunani. Katika huu mlango wa sita tutaona ufalme wa pili katika ile sanamu ambao ni ufalme wa Wamede na Uajeni (Medes + Persians). Katika mlango wa tatu wale vijana Waebrania walikataa kuabudu ile sanamu ya mfalme Nebukadreza hivyo wakatupwa katika tanuri ya moto. Hawa vijana watatu waligundua moto si moto panapo Yesu Kristo. Mlango wa nne tuliona ushuhuda wa mfalme Nebukadreza baada ya kufanyika ng’ombe kwa miaka saba na jinsi mfalme Nebukadreza alivyookoka, jinsi mfalme Belshazzar aliona maandishi juu ya ukuta wa nyumba ya enzi yake yaani “Mene mene Tekeli Persi.” Leo hii na tutazame “Simba katika tundu la Danieli.”

  • Katika Danieli 6:1-7 wazee wa Uajeni Persia walimchezea mfalme Dario.
  • Walimchezea kwamba wamfanye kuwa “Mungu” kwa mwezi mmoja. Dario alipendekezwa na hoja zao, hivyo akaweka sahihi yake juu ya ile amri.
  • Danieli 6:10-11 mfalme Dario alipopitisha ile sheria, hakujua njama za wale Wazee wake.
  • Sheria ya wa Mede na Waajemi haingeweza kupinduliwa hata kamwe.
  • Wazee walipenda sana wazo lao la kumkamata Danieli.
  • Danieli 6:16-24, Danieli anatuonyesha jinsi itupasavyo kuishi na tabia tunayohitaji kuwa nayo. Je, tunajifunza nini kutoka maisha ya Danieli ambaye sasa alikuwa mzee wa miaka 80? Hebu tuone:-

ADHARANI: ISHI MAISHA SAFI NA TAKATIFU.

  • Hawa viongozi wa Persia waliona uchoyo juu ya Danieli hivyo walitaka kumwaibisha.
  • Lakini tabia na maisha yake Danieli ilikuwa takatifu na safi.
  • Maisha na tabia ya Danieli ilikuwa safi sana, Danieli aliishi katika utakatifu kiasi hakuwa na lawama yeyote.
  • Biblia inasema Vs. 3 kwamba “Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na waliwali, kuwa roho bora ilikuwa ndani yake, naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.”
  • Roho bora ni roho ilivyo nzuri zaidi. Nia yake Danieli (attitude) ilikuwa nzuri na ya kupendeza.
  1. Uwe na roho bora-Haijalishi umri wako (stay positive).
  • Roho bora Maanake ni hata ingawa Danieli alikuwa mzee sana, roho yake haikuharibika juu ya kazi yake na maisha kwa jumla.
  • Unaona watu wengi wanapoendelea kuzeeka roho zao zinakuwa ngumu, hasira na ghadhabu zinawaandama kiasi inakuwa ngumu kuishi na watu.
  • Wazee wengi wanapatwa na kinyongo, hasira kila asubuhi, matusi na kulalamika kila kitu.
  • Danieli alikuwa mzee wa miaka 80, na anaendelea kuwa na roho bora, roho safi, roho ya amani na furaha!!
  1. Uadilifu, ukamilifu na uaminifu wa Danieli.
  • Onyesha uadilifu katika kila haina ya kazi!!
  • Uadilifu (integrity) ni kuwa mwaminifu, tegemeo na mkweli. Je, wewe ni mwaminifu kazini?
  • Danieli 6:4, “Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshtaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa, kwa maana alikuwa mwaminifu wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.”
  • Waliangalia kila kitu, kila mahali kuona kosa lolote, bila kupata!!
  • Unaweza kumpenda Mungu sana na pia kuifanya kazi yako vizuri na kwa uadilifu.

KATIKA MAISHA YA SIRI: MAOMBI IWE TABIA YAKO.

  • Maisha ya adharani ya Danieli ilikuwa maisha ya uadilifu na utakatifu, lakini maisha yake ya siri yalikuwa maisha ya maombi.
  • Danieli alipopata fahamu ya kwamba mfalme Dario amepitisha sheria kinyume cha maombi, Danieli aliazimu kuendelea maombi yake kama kawaida.
  • Danieli aliamua kwamba afadhali kumtii Mungu kuliko kumtii mwanadamu (civil disobedience).
  • Wakati serikali ya mwanadamu inaenda kinyume na serikali ya Mungu, Mkristo anahitaji kumtii Mungu na sheria yake. Mume wako au wazazi wako akikukataza kuabudu Mungu, ni lazima kumtii Mungu kuliko mume wako au wazazi wako.
  • Danieli aliposikia mfalme Dario ameweka sheria ya kutoomba, Danieli aliendelea kumwomba Mungu wake.
  • Katika maombi yako ya binafsi:-
  1. Chagua mahali pa kuomba; panga mahali rasmi, pawe mahali pako kuomba-Marko 1:35.
  • Hapa ndipo mahali pako pekee kuomba.
  1. Wakati kamili.
  • Danieli aliomba mara tatu kila siku katika mahali pake pa maombi-Zaburi 55:17 (Jioni, asubuhi na adhuhuri).
  • Siku ya Wayahudi inaanza jioni saa kumi na mbili.
  • Katika maombi yako soma Zaburi moja, soma mlango moja katika Agano la kale na moja Agano jipya, tena soma Mithali moja, basi omba.
  1. Msimamo katika maombi (posture).
  • Danieli aliomba juu ya magoti yake, hata katika miaka zaidi ya 80!!
  • Kuna msimamo kadha ya kuomba, unaweza kupiga magoti chini, kuyainua macho mbinguni, kusimama huku mikono imenyanyuliwa, kuweka kichwa chako katikati ya miguu, juu ya kitanda chako.
  • Hakuna mahali tumeambiwa tufunge macho na kuinamisha kichwa.
  • Yesu Kristo alipiga magoti chini na pia Mtume Paulo (Waefeso 3:14).
  1. Omba kila siku, kila mara-Vs. 10.
  • Ilikuwa kawaida kwa Danieli kuomba kila siku.
  • Hakuna kitu shetani anaogopa kama maombi ya Watakatifu wake Mungu.

KATIKA PRESSURE: AMANI ITAKUWA DHAWABU YAKO.

  • Watu wa Persia walikuwa na desturi ya kuweka simba katika tundu. Wanaoasi mfalme walifanywa chakula cha wale simba.
  • Hapa ndipo walimtupa Danieli-mzee wa miaka 80.
  • Hebu tuone “simba katika tundu la Danieli.” Hii ni kwa sababu Danieli hapa ndiye alikuwa mwenye kusema.
  1. Kila mmoja wetu atakuwa na kipindi cha kutupwa katika tundu la simba-2 Petro 5:8.
  • Tundu lako linaweza kuwa kesi kortini, kukosa fedha, chakula, nguo au kazi.
  • Tundu lako laweza kuwa hali ya mahusiano, talaka, ndoa mbaya, magonjwa, maadui.
  1. Unapokuwa katika tundu la simba, tafuta yule kiongozi wa wale simba wote!!
  • Danieli alikutana na simba kiongozi wao ambaye ni Yesu Kristo, simba wa Yuda-Ufunuo 5:5. Dario alishuhudia “Mungu alimtuma malaika” kumlinda Danieli-Yohana 16:33.
  • Usiku huo Danieli alikuwa katika tundu la simba-pia naye Dario alikuwa akipigana simba wake, kilio, wasiwasi, kukosa usingizi wake!!
  1. Yesu Kristo angali anawafuga simba.
  • Mtume Paulo aliwaona wale simba pia-2 Timotheo 4:17-18.
  • Kunao simba kila mahali, lakini walio wa Yesu Kristo wanapiganiwa.

MWISHO

  • Mfalme Dario aliamuru wote waliomfitini Danieli watupwe katika ile tundu la simba.
  • Walitupwa pamoja na jamaa zao wote, walikulwa wangali hewani!!
  • Tofauti na Danieli ilikuwa ni kuokoka.
  • Bila Yesu Kristo hatutakuwa na wakusaidia katika tundu za maisha, magonjwa, kifo, hakutakuwa na kuokoka na kukufufua kutoka wafu.
  • Je, simba wako ni gani? Simba anaguruma au simba wa kabila la Yuda.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *