MFULULIZO : KURUDI KWA YESU KRISTO
UJUMBE : MFALME ANAKUJA.
SOMO : UFUNUO 19:11-21
MHUBIRI: REV. DR.WILLY MUTISO.
Kwa miaka 6,000 maisha ya mwanadamu imeendelea. Tangu mwanadamu kufanya dhambi katika Bustani mwa Edeni , historia imeendelea safari yake kusongea siku na jambo kuu. Hili jambo ni kurudi kwa Yesu Kristo duniani. Yesu Kristo atakaporudi atakuja kwa nguvu uwezo na utukufu mkuu. Atakapokuja Kristo basi ataketi na kutawala juu ya kiti cha mfalme Daudi Isa.9:7, Luka 1:32.
Yesu Kristo alipokua hapa duniani aliahidi wafuasi wake mambo mengi sana. Ahadi kuu ya Yesu Kristo ni kuja kwake mara ya pili ( Mathayo 24:27-30 ). Ahadi yake ya mwisho ni “Tazama ñaja upesi ” (Ufunuo 22:20 ).
Ukweli wa mambo ni kwamba Kristo yuaja Tena. Kwanza Kristo akuja mawingu, kunyakua waliowake mbinguni (Yohana 14:1-3 ; I Cor 15:51-52 : I Wathessalonike 4:13-17)
Kama jinsi sarufi ilio katika mfuko wako iko pande mbili, pia kurudi kwa Yesu Kristo. Kwanza atakuja mawinguni kuwapokea Bibi Arusi wake. Pili atarudi yeye mwenyewe pamoja na kanisa la watakatifu wote, kwa utukufu na nguvu, kuwashinda adui zake na kutawala dunia yote.
Huku kurudi, hapa duniani kutawala ndio somo letu Leo.
- Watu wengi wakuu wameacha maneno Yao hapa duniani.
- Rais Nixon alisema, “Mimi si mwizi sitawaongezea ushuru” Lakini ushuru ulipanda .
- Rais Clinton alisema “Mimi sikufanya mapenzi na huyu mwanamke” Lakini alifanya.
- Rais Gaddafi alisema ” Mimi ntakua Rais wa Afrika yote “Lakini akafa.
- Rais Mzee Kenyatta alisema “Mimi ntamaliza umaskini, ugonjwa, ukoloni na ujinga “Lakini Kenya imejaa umaskini, ugonjwa, ukoloni na ujinga!! Miaka 60 baadaye.
- Rais William Ruto amesema “tutapanda miti Billioni 15” Lakini haitawezekana!!
- Wanadamu hawatimizi ahadi zao, lakini Yesu Kristo atatimiza ahadi yake yuaja tena!! Haleluya – Ameni. Hebu tuone :-
KURUDI KWAKE YESU KRISTO KUTAKUWA HADHARANI ( UFUNUO 19:11-16).
- Yesu Atakapokuja mawinguni, kunyakua kanisa lake, itakua ni jambo haraka zaidi watu wengi hawata jua kilicho fanyika .
- Kunyakuliwa itakua ni kama jinsi mwivi usiku.
- Yesu Kristo atarudi kama mwivi usiku kunyakua Bibi Arusi wake (Kanisa la ukweli) .
- Kunyakuliwa hautakuwa hadharani, Lakini kurudi mara ya pili ni hadharani. Kila jicho lazima kuona utukufu na nguvu zake (Ufunuo 1:7)
KUTOKEA KWAKE( V.11-13 )
Asili yake : ( V.11-12 )
- Sura yake ni tofauti na jinsi alivyokuja mara ya kwanza.
Amejaza utukufu v.12 amevaa taji nyingi saana – ” diaderms”
- Hizi ni taji za ufalme .
- Shetani “mpinga Kristo” alikuwa amepewa taji za kushinda “Stephanos”
- Lakini Yesu Kristo ni tayari mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana .
- Macho yake ni kama ” miale ya moto ” Kuonyesha utakatifu wake, yeye ndiye Simba wa Yuda – Nguvu, mamlaka na utukufu.
- Mara ya kwanza alikuja kwa unyenyekevu mwingi (Wafilipi 2:5-8) mwana wa simanzi, kondoo wa kuchinjwa (Isa 53:2-3)
- Mara ya kwanza alikuja kwa dhiaka, wachache walimtambua, alichukiwa bila sababu, walimuua mtini.
- Lakini sasa, ni Mfalme wa wafalme wote safi na milele utukufu wake hauna kifani.
Yeye ni mwaminifu na kweli ( v 11 )
Tunaweza kumtumaini, Hana uongo .
- Kumbuka – unaweza kumtumaini yeye aliye Bwana !!
- Yeye amepigana vita kwa kweli (v.11 )
- Katika historia kumekuwa na vita nyingi bila haki . ( just war )
- Mfalme wa Amani anafanya vita vya haki – ( Kutoka 15:3 ) .
MAJINA YAKE ( v. 12-13 )
- Atakaporudi Yesu Kristo majina tatu amepewa :
Jina ajabu asilolijua mtu yeyote (Mystery)
- Wakati wa kumjua Yesu ni Leo, Leo ni mwokozi (Savior ) ( Yesu ).
- Kuna siku watu hawataweza kumjua atakuja kama hakimu mkuu.
- Leo ndio siku la kuliita Jina lake na kuokoka, arudipo, Haji kama Mwokozi kuokoka.
Jina la Huduma – “Neno la Mungu”
Hii ndio Jina lake la Huduma (I Yohana 1:1, 14)
Jina la ufalme ( V.16)
- MFALME WA WAFALME, BWANA WA MBWANA .
- Alipokuja kwa walio wake walimkataa (Yohana 1:11-12 ).
- Pilato alimpa Jina la Dharao (Yohana 19:15) Mathayo 27:37. ( Mfalme wa wayahudi ) Lakini ni Mfalme wa wote.
- Leo hii, mpokee MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
MAJESHI WA YESU KRISTO ( v.14 )
- Kila mfalme anayo jeshi lake, Yesu Kristo pia .
- Ona uniformu Yao – Kitani safi Nyeupe na safi sana .
- Jeshi lake halina silaha!! Kwa sababu Kristo anapigana yeye mwenyewe pekee!!
- Wanajeshu ni nani ? ( v.14) v.8 – Bibi Arusi wa Yesu Kristo.
- Utajua jinsi ya kupanda farasi !!
SILAHA ZA YESU KRISTO v.15
- Hakuna bunduki, Kifaru, Nuclear Lakini ” Neno “
- SILAHA yake ni Neno (Waebrania 4:12) (Isaya 11:4).
- JE ,utakuwa katika Jeshi la Bwana ?
KUJA KWA YESU KRISTO KUTAKUWA FUJO SANA (VIOLENT) (v.17-18 )
Ndege warukao mbinguni wataitwa !! ( v.17 )
- Damu ya watu itafurika kuliko Elnino ( Ufunuo 14 :20).
Nyama za majeshi na wafalme ( v.18 )
- Daraja zote za majeshi.
- Katika maisha walitengwa na vyeo vyao Askari kawaida na commissioned officers.
- Siku hii wote watakuwa bure ni chakula cha ndege wa angani!!
- Kifo – Kina leta watu level Moja.
- Katika kifo, hakuna cheo, elimu, sura, pesa – Bila Yesu Kristo maisha na Bure !! Kabisa .
- Bila Kristo ni jihanamu Express.
KUJA KWA YESU KRISTO KUTAKUWA NI USHINDI ( v.19-21 ).
MAJESHI YOTE YA DUNIA YATAVUTIWA KUINGIA KWA VITA VYA ARMAGEDDON ( v.19 )
- Majeshi yote ya ulimwengu huu, hata majeshi ya mataifa adui watashirikiana pamoja!! Kupingana na Bwana Yesu Kristo!!
- Hata majeshi watakao kuwa katika vita kama jinsi Urusi na Ukrain, Israeli na Gaza watashikana na kujiunga , kupigana na Yesu na watakatifu!!
- Majeshi yote ya ulimwengu yaharibiwa kabisa mle Armageddon.
- V.20 – Yule mnyama (Anti – Christ) Beast na Yule Nabii wa Uongo watashikwa na kumalizwa .
- Watu wa dunia wataangamizwa .
- Kwa Neno la kinywa cha Yesu Kristo – Ushindi utawezekana kabisa-Haleluya.
- Itakuwa siku ya Ushindi mkuu kwetu, Haleluya.
MWISHO
- Haya yote lazima kufanyakia – Tutaona!!
- Kama bado kuokoka huenda utakua mmoja katika Yale majeshi ya dunia hii na mataifa kama tuyajuavyo Leo.
- Ni afadhari kuokoka – mpokee Leo – uwe tayari ajapo.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.