Categories: Swahili Service

MAHALI PAITWAPO JEHANAMU (KUZIMU)

MFULULIZO: KURUDI KWA YESU KRISTO

SOMO: LUKA 16:19-31.

 

Kifungu cha leo kinatueleza juu ya mahali paitwapo jehanamu au kuzimu. Katika ulimwengu wa leo watu wengi hawaamini kuna mahali paitwapo kuzimu. Lakini Biblia ni neno la Mungu na Mungu ni mkweli. Hata ingawa Biblia inatufundisha sana juu ya kuzimu watu wengi bado hawakuamini neno la Mungu. Kuna vikundi vitatu vinavyopinga jambo la kuzimu.

  1. Watu wa mawazo ya juu (Rationalism).
  • “Hakuna Mungu, hivyo hakuna kuzimu na jehanamu.”
  • Charles Darwin alikuwa mpagani alikanusha mambo ya jehanamu.
  • Lakini “wacha Mungu awe kweli na kila mwanadamu mwongo.”
  1. Watu wenye kupuuza (ridicule).
  • Watu wanaopuuza ukweli juu ya jehanamu (kuzimu) wanasema Mungu yupo lakini hawezi kuruhusu watu kuchomeka hivi.
  1. Watu wa dini.
  • Dini inasema “Mungu yupo, lakini Mungu ni wa upendo mwingi, hivyo hawezi kuacha watu waende kuzimu.”
  • Madhehebu ya uongo (cults) msimamo wao ndio huu.
  • Christian Science “kuzimu ni makosa ya akili potovu.”
  • Jehovah’s Witness (mashahidi wa Yehova) “wenye dhambi watapotea hewani (annihilated).
  • Mormonism “watu wote wataokolewa.
  • SDA-sabato “Mungu siku moja atafuta dhambi zote na wenye dhambi wote.”
  • Lakini “Wacha Mungu awe kweli na kila mwanadamu mdanganyifu.”
  • Mengi zaidi tunayojua juu ya kuzimu yalisemwa na Yesu Kristo mwenyewe.
  • Kristo alikuwa mhubiri juu ya kuzimu na jehanamu.
  • Kuzimu imetajwa mara 162 katika Biblia, mara 70 Kristo alinena juu ya kuzimu.
  • Yesu Kristo aliamini sana juu ya kuzimu.
  • Yesu Kristo alituonya juu ya kuzimu. Hebu tuone:-

KUZIMU- NI MAHALI PA HISIA (SENSATION)-Luka 16:23-25.

Akiwa kule kuzimu, mtu tajiri aliweza kuona, kisikia, kuongea, kujisikia, alikuwa na mahitaji, aliweza kuwaza na kufikiria.

  1. Hata ingawa mwili wake ulikuwa kaburini, duniani alipozikwa, lakini mle jehanamu-kuzimu huyu tajiri yuko na mwili aliyeweza kuendelea kukishi baada ya mauti duniani.
  2. Usikubali kudanganywa na watu, ukifa leo katika Yesu Kristo au ukifa bila Yesu Kristo hauwezi kukaa kaburi hata nukta moja.
  • Papo hapo unaamka kuzimu au mbinguni kulingana na uamuzi wako juu ya Yesu Kristo-2nd Wakorintho 5:8; Luka 16:22-23.
  1. Kifo sio mwisho wa kuishi, nafsi yako haiwezi kufa-niya milele. Baada kufa ni mbinguni au kuzimu-katika mwili mpya.
  2. Kuzimu ni mahali pa kujiisi, hivyo waendao kuzimu wajiisi na kujuta uamuzi wa kutookoka.

KUZIMU NI MAHALI PA KUTENGANA (SEPARATION)-Luka 16:26.

  1. Tajiri yule alijikuta ametengana kabisa na Lazaro na Ibrahimu.
  • Ufa katika mbinguni na kuzimu ni mkubwa sana.
  • Ufa huo umewekwa milele, kutengana huku ni milele na milele.
  1. Ghadhabu moja ya kuzimu ni kule kutengwa milele na milele (eternal separation).
  • Kutengwa na Mungu milele na milele.
  • Kuzimu hakuna jamii, ndoa, rafiki, ushirika.
  • Kuzimu ni kifungo cha maisha na kutengana na kila jambo njema, milele na milele.
  1. Kuzimu, mwenye dhambi, hatasikia tena neno la Injili, tumaini, faraja. Hakuna Biblia, mhubiri, hamna tumaini la mabadiliko.
  2. Kuzimu ni kutengana na Mungu muumba milele na milele. Hakuna neema, rehema na upendo.
  3. Kuzimu ni kutengana daima na upendo wa Mungu na wema wake-2 Wathesalonike 1:8-9.
  • KUZIMU NU MAHALI PA KUTESEKA MILELE-Luka 16:24-25.
  1. Kuzimu ni mahali pa matatizo.
  2. Kuzimu ni mahali pabaya zaidi.
  • Moto usiozimika-Marko 9:45.
  • Mahali pa kiu-Luka 16:25; 27-28.
  • Mahali pa shida, hasira na kutengwa-Ufu. 21:8.
  • Mahali pa ghadhabu ya Mungu.
  1. KUZIMU NI MAHALI PA SHINGO NGUMU-Luka 16:24-31.
  2. Huyu tajiri angali na ubinafsi na kujiinua-Vs. 24-Mtume Lazaro!!
  • Huyu tajiri anafikiri juu ya ndugu zake pekee.

Bado huyu tajiri hajajua jina linalookoa.

  • Bado anamjua Ibrahimu na Lazaro, lakini kuna jina linalookoa-Bwana Yesu Kristo.
  1. Majina ya Watakatifu, hayawezi kuokoka.
  2. Majina ya madhehebu na makanisa hayawezi kuokoa-Kristo pekee ni wokovu.

MWISHO

  • Kuzimu haikutengenezwa kwa ajili ya watu, bali shetani na pepo zake-Mathayo 25:41.
  • Kristo alikufa msalabani kwa ajili yako. Laiti leo kama ungejua yaletayo amini katika nafsi-Kristo.

Si lazima yeyote kwenda kuzimu, mapenzi yake ni wokovu kwako.

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago