Categories: Swahili Service

“ANGALIENI, MTU ASIWA DANGANYE”

MFULULIZO:  KURUDI KWA YESU KRISTO

 SOMO:   MATHAYO 24:1-28

Juu ya mambo ya nyakati za mwisho. Yesu Kristo anatuonya juu ya kudanganywa (V.4-5). Yesu Kristo anatuonya juu ya janga za kila haina (v.6-12). Yesu Kristo anatuonya juu ya kanuni ya unabii kutekelezwa mara mbili (V.15-21). Yesu Kristo ameahidi ukombozi kwetu tulio watoto wake (V.13-14)

Katika mlango hau sura hii ya Mathayo 24, Yesu Kristo alikuwa ametoka hekaluni mle Yerusalemu, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha, majengo ya hekalu. Yesu naye  akajibu akawaambia, hamyaoni haya yote? Amini na waambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe   ambalo halitabomoshwa.

Alipoketi katika mlima wa mizeituni,  wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakamuliza, mambo haya yatakuwa lini? Ni nini dalili za kuja kwako? Nini dalili za mwisho wa dunia?

Wanafunzi wa Yesu Kristo walitaka majibu. Nasi leo hii twataka majibu katika Mathayo 24.

Kupata majibu ni ngumu kwa sababu kuna mawazo na mafundisho mbali mbali. Lakini kila jambo alilosema Yesu Kristo lazima kutendeka na kutimia katika mathayo 24:1-3. Yesu Kristo aliwaeleza wanafunzi wake kwamba

  1. Wakati uliosalia ni mfupi sana
  2. Lazima kutafuta ukweli wa kiroho kutoka kwa Yesu Kristo mwenyewe.
  3. Baraka ni nyingi sana za kuokoka.
  4. Injili ya wokovu lazima kuhubiriwa ulimwenguni mwote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapa ndipo ule mwisho utakapokuja.

Hebu tujifunze:-

I.  YESU KRISTO ANATUONYA JUU KUDANGANYWA (MATHAYO 24:4-5, 23-26)

  • Kristo wauongo wengi (false Christs) watatokea.
  • Kristo wa uongo anayejulikana sana duniani alikuwa mtu kutoka Korea kwa jina Sun Myung Moon.
  • Moon alizaliwa mwaka wa 1920, alikuwa mwazilishi wa dini ya uongo linaloitwa “the        unification Church.”
  • Moon alifundisha yeye ndiye “Masihi na Kristo aliye rudi mara ya pili.”
  • Moon alifundisha kwamba, alikuja duniani kumaliza kazi ambayo Yesu Kristo alishindwa kumaliza kwa kuwa maisha yake ilikatishwa alipokufa msalabani!!
  • Katika mwaka 2004, Moon alijitawaza na “taji ya Amani” hapo Moon alitangaza kwamba amekuja duniani kuokoa, watu wote wa ulimwengu yaapata watu billioni sita. (6 billion)
  • Moon alizidi kusema, “wafalme, marais na viongozi wa dunia wameazimia kwamba “Moon ndiye mwokozi wa wanadamu wote, masihi, Bwana      aliyerudi tena na mzazi wa kweli kwa kila         mwanadamu.”
  • Moon alikufa mwezi wa tisa, tarehe tatu mwaka 2012 (03/09/2012) yaani miaka nane (8) iliyopita, alikuwa na miaka 92.
  • Wafuasi wa Moon yapata (3million) wangali katika inchi 100, hata hapa Kenya!!
  • Pili, Kristo mwingine wa uongo alikuwa Imamu wa kumi na mbili (12th) wa waisilamu wa shia (Shia Muslims) wa huko Iran.
  • Wao wanaamini imamu wa kumi na mbili Muhammad Al-Mahdi atakuja wakati ulimwengu umeingia katika shida kubwa na vita. Huyu Imamu atakuja huku amebeba upanga kuleta mwisho wa dunia. Musikiti uitwao “Jaukaran” huko Iran ndipo Imamu muhammed Al-Mahdi atakuja kama masihi!!
  • Yesu Kristo akawaambia “angalieni mtu asiwadanganye.”
  • “wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ndimi kristo na kuwadanganya wengi”
  • Watu millioni na millioni wamedanganywa (II wakorintho 4:3-4)
  • Hivyo, huhusu siku za mwisho Yesu Kristo      ametuonya juu ya kudanganywa.

II.  YESU KRISTO ANATUONYA JUU YA JANGA KAMA JINSI KORONA (COVID-19) (MATHAYO 24:6-10)

  • Katika Mathayo 24:6-10 – Yesu ametuonya juu ya janga za kisiasa (Political disasters)
  • Tunasikia habari za vita na matetesi ya vita.
  • Taifa (Ethinos) kabira, kuinuka juu ya taifa (Ethinos).
  • Ufamle kupigana na ufalme (nation against nation).
  • Yesu Kristo ametuonya juu ya janga za kiuchumi.
  • Njaa, matetemeko ya nchi, Haya yote ni mwanzo tu, lakini ule mwisho bado.
  • Katika (Mathayo 24:9-10) usaliti
  • Leo Wakristo wengi zaidi wanateswa kwasababu ya imani yao kuliko miaka ya kale. Misri, Pakistani, India, China (Nka).
  • Hata hapa Kenya kuna roho yapiga kazi ya kanisa, waziri wa afya (Matahi Kagwe) apendi kanisa na kazi yake.
  • Miaka kadha iliopita sinema ya “Da Vinci code” kukashifu Yesu Kristo ilikuja kuonyeshwa hapa Nairobi, tukamwendea kama waziri wa habari, akakataa kuisimamisha!!
  • Lakini ni ngumu sana kwake kupigana na Bwana wa Majeshi – Yesu Kristo.

III. KANUNI YA UNABII KUTIMIZWA MARA MBILI (THE LAW OF DOUBLE INSTANCE) (MATHAYO 24:15-21)

  • Katika tafsiri ya unabii, ni vizuri kuelewa na kanuni ya tafsiri ya unabii wa Biblia, kwamba, jambo la unabii linaweza kutimishwa mara mbili. Kwanza kwa sehemu na mara ya pili kwa ukamilifu kabisa.
  • Kwa mfano, Yesu Kristo alisema (V.15) “mtakapoliona chukizo la uharibifu” lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu” (asomaye na afahamu)
  • Tutakapoona mahali patakatifu hekaluni pamechukuliwa na kukaliwa na mwenye dhambi. (Daniel 9:21-27)
  • Maneno haya yalinenewa Danieli miaka 500 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  • Danieli aliona kipindi cha majuma 70 (70 weeks). Haya ni majuma ya miaka wala si juma la siku saba!!, Juma la miaka saba (wiki = miaka 7).
  • Hivyo kutakuwa na (miaka 70×7) hau miaka 490. mpaka ufalme wa masihi.
  • Katika mwaka wa 445 B.C, mfalme Artaxexxes wa uajeni (Persia) aliwaruhusu wayaudi kurudi Yerusalemu, kutoka kwa uamisho wa babeli. Kutoka wakati huo mpaka kifo cha Yesu Kristo ni miaka 483 hau juma 69.
  • Kilicho baki kwa miaka 490 ni miaka 7(Saba) kumaliza juma 70.
  • Katikati ya juma la 69 na juma la 70 tumekuwa na wakati wa kanisa hapa duniani yaani miaka (2020)
  • Katika mwaka 175-163 B.C mfalme Antiochus wa Syria aliingia Yerusalemu.
  • Alimbomoa hekalu na kuweka sanamu za Mungu Zeus, alikatisha kabisa ibada na sadaka hekaluni mpaka wakati wa Maccadean (Maccabees) Danieli 11:31 ikatimia.
  • Baada ya Yesu Kristo kupaa mbinguni baada ya miaka 40, yaani 70 A.d, Tito Generali mkuu wa Roma aliingia Yerusalemu pamoja na jeshi lake kubwa, wakaimboa hekalu la Yerusalemu. Tito aliweka sanamu za Roma katika mahali patakatifu. Hii ilitimiza unabii wa Yesu Kristo katika (Luka 19:41-44). Mathayo 24:20-24.
  • Wakati huu wakristo walikimbia milimani. Lakini kuna siku inakuja hivi karibuni unabii huu wa Yesu, Kristo na Danieli utimizwa kwa ukamilifu, hili (Mathayo 24:21) dhiki kuu inakuja duniani. Dhiki hii itakuwa kubwa   ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
  • Dhiki hii kubwa zaidi itafanyika katika juma la 70 la miaka yaani miaka 7 saba iliyosalia!!

IV.  BWANA AMEAHIDI UKOMBOZI KWA WATOTO WAKE. (MATHAYO 24:21-28)

  • Yesu Kristo ameahidi ukombozi wa haina tatu kwetu.
  • Ukombozi wa kwanza ni kwamba siku za dhiki zimefupishwa!!
  • Kama siku za dhiki asingefupisha hakuna asingeokoka mtu yeyote!!
  • Kwa sababu ya wateule siku za dhiki zitafupishwa!!
  • Hivyo ndungu na dada siku zakuteseka kwako (ugojwa, njaa) zimefupishwa!!
  • Kwa sababu ya wateule.

Ukombozi wa pili ni “habari njema” yaani injili ya Kristo lazima kuhubiriwa ulimwenguni kote, kama ushuhuda kwa watu wote na ule mwisho utafika (Mathayo 24:13-14) ukombozi wa tatu ni kwamba Yesu Kristo atalinyakua kanisa lake.

MWISHO

  • Kitu cha maana leo, kwa somo letu ni kwamba, Yesu Kristo yuarubi tena hapa duniani.
  • Pili, Yesu Kristo yutayari kuokoa atakaye liitia jina lake sasa.
  • Njia pekee ya kuwa tayari kwa kurudi kwa Yesu Kristo ni kuokoka.
  • Liitie jina lake sasa kwa njia ya imani katika maombi – Ameni.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

13 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

15 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

17 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago