Categories: Swahili Service

BABA AWATAFUTA WAABUDUO KATIKA KWELI NA ROHO

MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA.

SOMO: YOHANA 4:20-25; YEREMIA 26:3-11.

 

Mungu awatafuta watu watakao mwabudu katika kweli na katika roho, je, wewe ni mmoja wao? Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo ametujulisha mapenzi ya moyo wake-anatafuta watu wamwabudu yeye.

Katika historia ya mwanadamu wengi wamejaribu kuabudu. Lakini wengi waliabudu Mungu asiyejulikana. Leo tutazame haina mbali mbali ya ibada na watu tafaka wanaotafuta kuabudu.

HAINA ZA IBADA NA WENYE IBADA.

  • Tunapo tazama watu wamnaofanya ibada, wewe basi ujioji unamwabudu nani-wewe ni “Mwabudu wa nani?”
  1. Waabudu wasiojua (ignorant worshippers)-Matendo 17:22-31.
    • Hawa waabudu wanaabudu bila ufahamu wa Mungu, bila ufahamu wa mapenzi ya Mungu.
    • Hawa waabudu hawajui Mungu ni nani na jinsi ya kuabudu.
    • Hawa wabudu hawajui jinsi Mungu alivyo-Yohana 4:25.
    • Hawa waabudu wanaishi katika madhabadu yaliyojengwa na mikono ya mwanadamu-17:24.
    • Hawa waabudu wanaanudu Mungu asiyedhibitiwa.
    • Hawa waabudu wanaabudu Mungu maskini anayehudumiwa na mikono ya mwanadamu-17:25.
    • Mungu wa Biblia anazo nguvu zote, anayafahamu yote, yuko kila mahali, ni muumba wa yote, isipokuwa dhambi-17:24.
    • Mungu wa Biblia ndiye anatupa uzima, ndiye ametuumba-Matendo 17:22-31.
    • Basi tumwabudu Mungu aliye MWENYEZI-Zaburi 95:6-7.
  2. Waabudu wasiojitoa (adamant worshippers)-Yeremia 26:3-11.
  • Waabudu hawa ni visiwi-Vs. 3, 5.
  • Waabudu hawa wanakataa kutubu dhambi-Vs. 3.
  • Waabudu hawa ni shingo ngumu-Vs. 4.
  • Waabudu hawa wanapenda kusikia wapendayo-Vs. 9-11.
  1. Waabudu wanafiki (hypocritical worshippers)-Zefania 1:5.
  • Waamini hawa wanatoa nadhiri zao kwa Mungu (Yehova) lakini pia kwa sanamu Milkoni.
  • Yesu Kristo alisema huwezi kuabudu na kuwatumikia mabwana wawili-Mathayo 6:24.
  • Herode alikuwa mnafiki-Mathayo 2:8, 16; Zaburi 78:36-37.
  1. Waabudu wanao abudu malaika na shetani (Angels & devil worshippers)-Ufunuo 9:20; Wakolosai 2:18)
  • Mtume Yohana alijaribu kumwabudu malaika-Ufunuo 19:10; 22:8.
  1. Waabudu wa bure-(vain worshippers).
  • Waabudu hawa wanaabudu kwa vinywa vyao na midomo yao, bila mioyo yao-Isaya 29:13.
  • Mioyo yao imo mbali sana na Mungu-Isaya 59:1-2.
  • Bwana Yesu Kristo aliwaona waabudu hawa katika Mathayo 15:7-9 wanafuata mafundisho ya wanadamu.
  1. Waabudu wanaofuata mawazo yao binafsi (self-willed).
  • Wanafanya mapenzi yao na fikira zao (Wakolosai 2:20-23; Isaya 2:8, 20).
  1. Waabudu wa kweli (true worshippers)-Yohana 20-24; Wafilipi 3:3.
  • Si kila ibada inakubalika mbele za Mungu.
  • Tunaweza kuwa na haina nyingi za ibada lakini ibada moja tu, inakubalika mbele za Mungu.
  • Ibada hii haipingwi na mahali.
  • Ibada hii haidhibitiwi na vifaa vya ibada.
  • Ibada hii haiitaji mavazi spesheli.
  • Ibada hii haina ufumba, mafuta, haina sheria na mapokeo ya baba.
  • Ibada hii inafanyika katika Roho na kweli, ibada hii inausisha “mtu wa ndani.”
  • Ibada hii inaanza katika Roho, kupitia nafsi mpaka mwili.
  • Ibada hii ni kila siku saa mpaka mwisho.
  • Tunahitaji kumwabudu Mungu kila saa, mahali popote, kazini, njiani, nyumbani, shambani, shule, chuoni popote pale.
  • Watu wengi wameweka Mungu wao katika sanduku-kanisani-lakini sasa Mungu hakai katika nyumba, bali anaishi ndani ya mioyo yetu saa zote.

MWISHO

  • Mungu alituumba kwa lengo-ibada.
  • Mungu ametuokoa kwa lengo-ibada.
  • Mungu ametujaza kwa lengo-Ibada.
  • Mungu ametuita kwa lengo-Ibada.
  • Sababu ya kuishi ni-Ibada.
  • Mungu anatafuta watu watakao mwabudu katika Kweli na katika Roho.
  • Je, wewe ni mwabudu wa haina gani?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago