BILA NGUVU MBELE YAKE ANAYE KUFUATIA

SOMO: MAOMBOLEZO 1:6 –12
UTANGULIZI

Haya ni maombolezo makali sana. Mkimbizi ako katika shida kubwa kwa sababu anafuatwa na wenye nguvu zaidi kuliko yeye. Mtu anayefuatwa hawezi kupumzika. Hakiwa bila nguvu, basi yeye amepatikana. Maombolezo 1:6- “Naye huyu binti Sayuni, Enzi yake imemwacha; wakuu wake wamekuwa kama ayala anayewafuatia”.

Bila nguvu mkimbizi anakuwa bila haja ya kukimbia. Hivyo ndivyo ilvyo hali ya wengi wetu. Tumekuwa na adui nyumbani kwa baba, nyumbani kwa mama, wakwe zetu, kazini, kanisani, sokoni, nasi hatuna nguvu!! Je, wanao kufuata ni nani ? Je, unafuatwa na hasira, tamaa mbaya, hofu, ndoto mbaya, mazingaombwe, wachawi, bahati mbaya, njaa, umaskini, vuguvugu, kurudi nyuma, dunia, usharati, Je, mambo yaliyokuwa bali nawe yamesongea karibu nawe ? Je, magonjwa ya zamani yameaza kukurudia? Kanuni ya Kiroho inasema “Kama mtu atarudia dhambi ya kitambo, basi shida za kitambo zitakurudia “ (Yohana 5:1-15) Hivyo, “dhambi za kitambo, shida za kitambo”

Kama njinsi ilivyo, Mkristo ndiye anahitaji kuwa anakimbiza dhambi na adui zake, lakini kinyume chake, wakristo wa sasa tumekosa nguvu. Kanuni nyingine ya roho inasema “kama nguvu kuu inakadhibiana na nguvu kidogo, nguvu ndogo lazima kutii na kujisalimisha” hivyo kama huna nguvu, mbele ya adui zako ni lazima shida iwemo.

Tujifunze:-

I.  JINSI YA KUFUATIA ANAYE KUFUATIA (Zaburi 51:17)

  • Kunao watu wanao dharauliwa na Mungu (Mithali 1:28)
  • Moyo uliovunjika na kumbondeka, Mungu, hataudharau.
  • Mungu yuko karibu na walio rafiki zake (Zaburi 34:18)
  • Tafute kuwa rafiki wa Mungu wako.
  • Unapowindwa na adui mwenye nguvu kuliko wewe, shida-hivyo soma (Waefeso 6:10)

II.  JE, KUVUNJIKA NI NINI ?

  • Kuvunjika ni kudhibiti nafsi yako, Mungu anadhibiti nafsi yako, ndio kuvunjika.
  • Moyo usio vunjika unalaani watu na ulimi wake ni kali.
  • Kuvunjika ni kumruhusu Roho mtakatifu kutawala.
  • Mtu aliye vunjika hatendi mambo kwa hasira.

III. UKWELI WA VITA VYA KIROHO (Waefeso 6:10-17)

  • Lazima kumpiga shetani na kazi zake.
  • Lazima kudhibiti akili na nafsi yako.
  • Lazima kusulubisha mwili wako (Ufe kabisa)
  • Unapokufa nafsi yako, shetani atashindwa kwako.

* Utafahamu siri za Mungu, Mungu ataongea nawe

* Mishale ya shetani itashidwa, nyoka na inge watakuwa chini ya miguu yako

* Utakuwa tisho kwa shetani na malaika zake.

* Hautashirikiana na shetani .

IV.  ISHARA ZA KUTOVUNJIKA

  1. Mkali wa moyo, kutotii na kutojifunza
  2. Tabia Mbaya hazikutishi kamwe.
  3. Dhambi haikutishi.
  4. Huoni udhaifu wako, neno la Bwana haina nafasi dani yako, unakaa katika unafiki, marafiki zako ni watu hawajaokoka.

 

 

V.  BASI TUFANYE JE ?

  • Tunao wachungaji, ushers, waimbaji na watumishi wengi wasiovunjika nafsi zao.
  • Samsoni alikuwa mtoto wa ahadi, lakini hakuvunjika.
  • Lilia Mungu wako leo, Omba hatima yako ikang’are

 

MWISHO

Omba:

  • Ee, Bwana ninaomba moyo wa kuvunjika katika Jina La Yesu.
  • Ee, Bwana nisaidie kushida vita dhidi ya umaskini, kurudi nyuma, tabia mbaya na kiburi.
  • Bwana, nitatembea, nitakimbia , nitavuka kuwa tai mwaka huu, katika Jina la Kristo Yesu.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE

TEXT: LUKE 2:1-14.   The birth of Jesus Christ shattered spiritual, social and eternal barriers,…

24 hours ago

CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME?

TEXT: JOHN 3:16-17.   Christmas unveils the divine mission behind the birth of Jesus Christ;…

1 day ago

KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA

MFULULIZO: KRISMASI NI KUFUNULIWA KWA YESU KRISTO.  SOMO: LUKA 2:8-14.   Krismasi inafunua jibu la…

5 days ago

CHRISTMAS IS WHEN HEAVEN CAME DOWN TO EARTH.

SERIES: CHRISTMAS IS CHRIST. TEXT: JOHN 1:1-14.   Christmas is the divine moment when God…

5 days ago

FOR GOD SO LOVED THE WORLD

TEXT: ISAIAH 53:1-12.   The son of man came to seek and save that which…

5 days ago

JESUS OUR SAVIOR

SERIES: CHRISTMAS IS JESUS CHRIST. TEXT: MATTHEW 1:21   Jesus Christ is the savior of…

2 weeks ago