Categories: Swahili Service

BWANA AKAWA PAMOJA NA YUSUFU

MFULULIZO: YUSUFU

SOMO: MWANZO 39:1-6.

 

Tulipokuwa na Yusufu hapo awali alikuwa amesalitiwa na nduguze na kuuzwa kama mtumwa kwa Waishimaeli kwa bei ya chini sana. Ndugu zake walimuuza kwa bei ya kiwete. Basi Waishimaeli na wao wakamuuza Yusufu huko Misri kwa mtu wa Misri aitwaye Potifa, mkuu wa askari mtu (mzaliwa) wa Misri.

Hebu kwa muda ujiweke katika viatu vya Yusufu. Umenyang’anywa nguo zako na koti (kanzu) ya rangi nyingi, umesalitiwa na ndugu zako, watu walio karibu na wewe, umetengwa kabisa na baba yako, umeuzwa kama mtumwa kwa nchi ya mbali ya kigeni.

Tazama jinsi hio safari ilikuwa ndefu katika mikono ya wafanya biashara ya watumwa!! Lakini Mungu alikuwa naye Yusufu!!

Hebu tuone jinsi ya kufahamu kwamba kile Mungu amefanyia wengine atakufanyia wewe pia. Hebu tutazame:-

MUNGU ALIMLINDA YUSUFU-Mwanzo 37:36.

  1. Yusufu aliona kama kila jambo limepasuka.
  • Lakini Yusufu alikuwa katika mikono ya Mungu.
  • Tazama jinsi Reubeni alitafuta kumwokoa Yusufu-Mwanzo 37:21-22.
  • Yuda ndiye alipendekeza Yusufu kuuzwa kama mtumwa kuliko kumuua-Mwanzo 37:26-27.
  • Tazama jinsi Wamidiani/Waishimaeli walitokea mara hiyo hiyo-Mwanzo 37:28.
  • Ukweli kwamba Yusufu aliuzwa kwa mkuu wa askari aitwaye Potifa-Mwanzo 37:36.
  • Mungu alipanga kila jambo kwa ratiba yake juu ya maisha ya Yusufu.
  • Pamoja na kuwa mtumwa, Mungu alimlinda Yusufu kila siku.
  1. Mungu atawatumia watu wa mataifa kukutumikia kila uendako.
  • Kila jambo katika maisha litafanyika katika ulinzi wa Mungu-Warumi 8:28.
  1. Hata ingawa maisha ya Yusufu ilikuwa katika mikono ya waovu, Mungu alikuwa katika kila jambo.
  • Ona jinsi Mungu alimlinda Yusufu.
  1. Kwa ulinzi wa Mungu, Yusufu hakuwa na uchungu katika maisha yake-Mwanzo 39:2. Uwepo wake ni ulinzi.
  • Yusufu alianguka katika mikono ya Mungu.
  1. Mungu alimtosheleza Yusufu.
  • Ndoto zake zikatimia.
  • Wewe pamoja nami tunakaa katika uwepo wa Mungu-Waebrania 13:5; Mathayo 28:20.
  • Tunao msaada kupambana na maisha ya kale-Waefeso 4:29-32.
  • Si lazima kuwa na uchungu, hasira wala roho ya kutosamehe.
  • Tunaweza kuwa na roho tamu hata katika mateso na majaribu.
  • Tunao ahadi kutoka kwa Mungu wetu, kila jambo litakuwa sawa sawa mwishowe-Warumi 8:28; Waefeso 1:11; Isaya 46:10; 2 Wakorintho 4:17-18.
  1. Utii kwa Mungu unatupeleka kupitia dhoruba nyingi-Isaya 53:10.
  • Mapenzi ya Mungu katika majaribu si kutuumiza, bali kutokosa-Yeremia 29:11.

MUNGU ALIMPA YUSUFU USTAWI-Mwanzo 39:2-3.

  1. Yusufu alipofika Misri hakuwa na ile kanzu la rangi nyingi.
  • Alipoteza ile kanzu lakini tabia yake ilikuwa timamu ndani yake.
  • Yusufu alipopoteza ile kanzu hakupoteza chochote cha kumfanya mtu mkuu.
  • Ukuu wa Yusufu haukutoka kwa mavazi yake lakini kutoka tabia ya maisha yake na uadilifu wake.
  • Hata watu wakunyang’anye mavazi lakini bado unaye Kristo.
  1. Yusufu alipofika Misri angalifuata njia kadhaa.
  • Pengine angefuata desturi na maisha ya watu wa Misri.
  • Pengine angemwacha Mungu wa Israeli na kufanana na miungu ya Misri ambayo ilikuwa miungu mingi (polytheism).
  • Yusufu aliambatana na Mungu wa Israeli.
  • Yusufu kwa kweli alinunuliwa na Potifa lakini Yusufu bado alikuwa mali ya Yehovah!!
  • Haikujalisha Yusufu yuko katika nyumba ya babaye, katika shimo, mikononi mwa Waishmaeli, katika nyumba ya Potifa.
  • Yusufu aliazimu kutembea na Yehova kokote aendako.
  • Yusufu alikuwa mali ya Mungu popote maisha yalimpeleka!!
  • Kama jinsi Yusufu azimu, amua, chagua kumwishia Yesu Kristo kokote uendako.
  • Amua kumwishia Kristo kwamba utamfuata Bwana, azimia kuwa na ushuhuda wako popote daima.
  1. Mwanzo 39:2, Yusufu alistawi, Mungu alifanya chochote Yusufu anafanya kubarikiwa-39:3.
  • Kustawi kwa Yusufu kulitokana na uwepo wa Mungu katika maisha yake.
  1. Yusufu alikuwa katika hali mbaya, lakini hali mbaya haiwezi kufanya Mungu asiweze kukubarikia.
  • Furaha ni kumjua Mungu wako katika kila hali ya maisha.
  • Zinge wawili walianguka katika ndoo ya maziwa.
  • Zinge wa kwanza aliona hofu mpaka akazama akafa.
  • Zinge wa pili alijaribu kutoka, kwa mabawa yake alipigana na maziwa mpaka maziwa yale yakawa siagi, akatembea juu ya siagi mpaka nje!!
  • Inategemea imani yako panapo majaribu.
  • Mhubiri mbatisti John Bunyan alifungwa gerezani mikaka 12 kwa kuhubiri bila leseni. Bunyan alichagua sifa katika gereza mpaka akaandika kitabu “Pilgrim’s progress.”
  • Kitabu hiki kimeuzwa zaidi duniani, ndicho kitabu cha pili kuuza sana cha kwanza ni Biblia.

MUNGU ALIMPANDISHA YUSUFU CHEO-39:4-6

  1. Potifa aliona kwamba mkono wa Mungu ulikuwa juu ya Yusufu-Vs. 3.
  • Potifa aliona kwamba chochote Yusufu anashika kinabadilika kuwa dhahabu!!
  • Potifa alimpandisha Yusufu cheo akawa mkuu juu ya wafanyakazi wake wote-Waefeso 6:5-9; Wakolosai 3:22-4:1.
  1. Kama samuli (cream) Yusufu alipanda juu ya wote. Potifa aliona kwamba Yusufu hakuwa mtu wa kawaida.
  2. Yusufu aliishi maisha ya kiungo, Mungu alimpandisha juu zaidi-Luka 16:10.
  • Yusufu alimea alipopandwa!!

MWISHO

  • Mungu alikuwa pamoja na Yusufu.
  • Machungu ya Yusufu Mungu aliyatumia kumjenga Yusufu.
  • Kwa wale Bwana anawajeruhi zaidi, anawatumia zaidi.
  • Bwana alikuwa pamoja na Yusufu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago