Categories: Swahili Service

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI.

SOMO: 1 YOHANA 5:4.

 

Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa kwa sababu hawajui jinsi ya kuchochea ule ushindi na ushujaa ulio ndani ya maisha yao.

Kila aliyezaliwa na Roho anaye mbegu ya ushindi ndani yake. Ulipookoka mshindi alizaliwa ndani yako, lakini uchochee ule ushindi. Umeumbwa kuwa mshindi na mtawala juu ya yote.

Vita vya maisha huenda vikawa kali zaidi, lakini hakikisho tumepewa na Mungu kwa maana ndani yetu tumebeba uwepo na nguvu za Mungu aliye juu.

Maisha huenda yakatupa changamoto kwa njia na mapito yetu, lakini zile changamoto si za kukusimamisha, lakini changamoto za kukupeleka kwa ukuu.

Katika ujumbe wa leo tutajifunza jinsi ya kuchochea mshindi aliyekaa ndani yetu na jinsi ya kumiliki na kutawala kila upinzani, kwa maana sisi tuwashindi na zaidi ya washindi. Hebu tutazame:-

UMEZALIWA NA MUNGU ROHO UPATE KUSHINDA.

  1. Kuzaliwa kwa Roho Mtakatifu kunadhibitisha hatima-1st Yohana 5:4.
  • Kila mtu alizaliwa na Roho wa Mungu amezaliwa kuwa mshindi juu ya dunia.
  • Ulipookoka uliamishwa kutoka giza kuingia nuruni.
  • Umeamishwa kutoka jamii ya dhambi na kushindwa, ukaingia katika jamii ya ushindi.
  1. Sasa we ulipooloka umepewa mbegu (DNA) ya ushindi-Warumi 8:37.
  • Tu zaidi ya washindi kwa Yesu Kristo, hivyo hakuna kushindwa katika kitambulisho chako cha kiroho.
  1. Ushindi wako hautegemei jinsiunavyojisikia-2 Wakorintho 5:17.
  • Hata wakati haujisikii kuwa na nguvu, imani yako inatia nanga katika ushindi.
  • Bwana tayari ametangaza wewe ni mshindi-Isaya 54:17.

CHOCHEA NGUVU ZA MUNGU ZILIZO NDANI YAKO.

  1. Unazo nguvu za Mungu ndani yako-2 Timotheo 1:6-7.
  • Roho ya nguvu, upendo na kiasi ziko ndani yako tayari.
  • Chochea hizi nguvu kupitia imani na maombi.
  1. Usiwache hofu kukunyamazisha-Warumi 6:12-14.
  • Kama jinsi Gideoni, lazima kuinuka juu, zaidi ya hofu zako na kufikia mshindi anayeishi ndani yako.
  1. Ujasiri wako utachochea nguvu za Mungu ndani yako-Mithali 28:1.
  • Usidharau kipawa kilichoko ndani yako-1st 4:14.
  • Unapodharau neema uliyopewa, mshindi anaye ishi ndani yako hatakufa.
  • Paulo alimwambia Timotheo kuchochea karama iliyo ndani yako-2 Tim. 1:6.
  • Paulo alimweleza Timotheo kwamba ukuu unahitajo kuchochewa karama zilizo ndani yetu.

POKEA USHINDI KWA KUFANYWA UPYA NIA NA AKILI ZETU.

  1. Nia inapobadilishwa na neno la Mungu ushindi utapatikana.
  • Ushindi unakaa ndani yetu, kushindwa pia kunaanza katika akili zetu-Mithali 23:7.
  • Ikiwa unajiona kushindwa huwezi kuwa mshindi katika lolote.
  1. Ishi na ongea kama mshindi-Wafilipi 4:8.
  • Kata kabisa mafikira ya kushindwa, ondoa kila ngome-2 Wakorintho 10:4-5.
  • Caleb na Yoshua waliona ushindi wa Yeriko-Hesabu 13:30-33.
  1. IMANI CHANZO CHA USHINDI.

Imani ni ushindi-1 Yohana 5:4.

  • Imani ndio unganisho na nguvu za Mungu.
  • Washindi wanatembea kwa imani, si kwa kuona-Waebrania 11:1.
  • Nena lugha ya imani-Marko 11:23.
  • Usiungame kushindwa, ungamo lako liwe la imani na ushindi.
  • Imani ni Matendo-Yakobo 2:17.
  • Mwanamke mwenye kutokwa na damu aliweka imani yake katika zoezi-Marko 5:25-34.
  1. MSHINDI ALIYE NDANI YAKO ANAHITAJI KULISHWA KILA MARA.
  2. Lisha roho yako kwa neno la Mungu-Mathayo 4:4.
  • Mtu wa ndani yako (inner man) anapata nguvu anapolishwa na neno la Mungu.
  1. Maombi nayo ni mawasiliano na Mungu wako, Mungu ndiye ushindi wako-Luka 18:1.
  2. Ushiriki na washindi wenzako-Mithali 27:17.
  • Usiipe njaa roho yako-Wagalatia 16-17.

MWISHO

  • Wewe si dhaifu, haujashindwa. Wewe ni mwana wa Mungu aliyepewa uwezo na Mungu. Miliki na tawala kwa nguvu za Mungu.
  • Hakuna vikwazo mbele yako unapochochea karama ya Mungu ndani yako. Karama ya ushindi ipo ndani yako.
  • Ulizaliwa mara ya pili uwe mshindi, lakini ni lazima kuchochea karama yake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

4 days ago

THE GOD WHO BREAKS YOKES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 10:27.   God’s desire is that none…

1 week ago

THE REWARD OF SEEKING GOD

SERIES: DRAW NEAR TO GOD. TEXT: HEBREWS 11:6.   The Bible tells us that God…

3 weeks ago

JINSI YA KUTAMBUA NA KUVUNJA VIZUIZI VYA BINAFSI.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: WAAMUZI 6: 11-16   Moja ya vizuizi kubwa zaidi kwa…

3 weeks ago

GOD TURNS SHAME TO GLORY.

SERIES: THE HOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 61:7   Shame is not the end…

3 weeks ago

THROUGH THE BOOK OF COLLOSIANS.

TEXT: COLLOSIANS 2:1-23   Apostle Paul writes to the church in Colossae from prison in…

3 weeks ago