MFULULIZO: KUPENYA KUSIO KWA KAWAIDA
SOMO MWANZO 26:18; MARKO 16:15-20
Ikiwa tutapata kuwa na nguvu, ishara maajabu, uponyaji na miujiza kama kanisa la kwanza katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ni lazima kuweka maombi katika mstari wa kwanza kama wao.
“Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti waliokuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu, Naye akayaita majina kufuata majina alivyoviita baadaye”-Mwanzo 26:18.
Leo hii tunataka kuchimba upya visima walivyochimba kanisa ya kwanza!!
“Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, akasema Bwana Wa Majeshi, na katika mahali hapa Nitawapa amani asema Bwana Wa Majeshi-(Hagai 2:9).
Hekalu la sasa halijawahi kuwa kuu kuliko lile la matendo ya mitume!!
Ni lazima sasa nasi tupigane sana kiasi tupate kupenya zaidi kuliko kanisa la Agano Jipya.
Tutapata Nguvu zaidi ya kanisa la kwanza ikiwa tutapata kuwa na njaa na kiu ya makuu ya Mungu, kwa kukataa maisha ya kawaida!!
Yesu Kristo alisema “Akafundisha Yesu Kristo akasema , Je haikuandikwa , Nyumba yangu itaitwa Nyumba ya sala kwa mataifa yote-(Marko 11:17).
Ikiwa tunataka kuona Nguvu zaidi, ishara zaidi, maajabu zaidi, uponyaji zaidi, na miujiza zaidi kama jinsi kanisa la Agano Jipya, katika Matendo ya mitume ni lazima kuweka maombi mbele kama walivyofanya wale.
Yesu Kristo anataka Nyumba hii, iweze kuwa nyumba ya maombi, kwa mataifa yote.
Lakini Je, Hii Nyumba inaweza kuwa nyumba ya maombi kwa mataifa yote Njia gani?
Hebu tutazame:-
MSINGI WA MAOMBI KATIKA KITABU CHA MATENDO: (Matendo 1:14-24, 2:1-4; 2:42).
Uwepo wa Mungu:
Nguvu za Mungu:
Katika kanisa la Agano jipya, kanisa la kwanza, kila mtu alishiriki ibada na kazi ya Mungu!!
JE, TUNASOMA NA KUJIFUNZA KITU GANI KATIKA MATENDO 3:1-11)?
Kwanza, maombi ndiyo maana zaidi.
Tunahitaji kuzidisha matarajio yetu kwamba Mungu atende kitu, ajidhiirishe mbele yetu kila kunapokutwa katika Nyumba yake na katika kila ushirika wa watu wake.
Ni lazima tupokee Nguvu za Mungu kwanza kabla hatujawapa watu hizo Nguvu.
HEBU TAZAMA MAOMBI YAO-(Matendo 4:23-24; 29-31).
Kwanza tunahitaji kuomba Pamoja kama kanisa.
Waliyainua macho yao, sauti zao kwa Mungu kwa Pamoja.
MWISHO.
MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1. Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…
SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6. Every destiny is a divine…
SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10 We have put off the…
SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20 Breakthroughs are divine interventions that…
SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…
MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4. Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…