MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO.
SOMO: KUTOKA 12:12-13.
Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa utakaso. Utakaso kwa damu ya YESU KRISTO unakulinda, kukuifadhi na kukudumisha kama mwana na mtoto wake Mungu, unatakaswa kutoka mauti, uaribifu, hukumu na hatari na janga zote.
“Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu nitapita juu yenu. Lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri”-Kutoka 12:13.
Tangu mwanzo wa dahari, damu imefanya kazi muhimu sana katika uhusiano wa Mungu na wanadamu.
Katika Agano la Kale, damu ya wanyama ilitumika kama njia ya kufunika dhambi, na kama utakaso kutokana na maangamizo.
Wakati wa Pasaka ya kwanza, Misri, Mungu aliwaamuru wana wa Israeli wapake damu ya kondoo juu ya milango ya nyumba zao, malaika wa mauti asipate kuwaguza. Hii ilikuwa Agano ya utakaso kwao kupitia kwa damu.
Katika Agano Jipya, sadaka iliyo kuu zaidi ilitolewa. Yesu Kristo alitolewa kuwa sadaka na dhabihu ya kutosha kwa wakati wote. Pale Kalvari Yesu Kristo aliangikwa msalabani. Yeye ndiye dhabihu ya kutosha milele na milele. Yeye ndiye sadaka kamilifu, damu ya Yesu Kristo si ya kufunika dhambi, lakini kuondoa kabisa, kusafisha kabisa.
Damu yake Yesu Kristo inanena mema zaidi kuliko damu ya Habeli, Maanake damu ya Yesu Kristo inanena utakaso, wokovu, ukombozi, kuhifadhiwa na ushindi wa milele na milele.
Kutakaswa kwa damu yake Yesu, Maanake ni kutengwa kutoka ubaya wote, tauni zote, janga zote, mikosi yote, hukumu zote na vitu vyote vinavyo wapata wengine. Vinavyowaua wengine, sasa haziwezi kuwaua walio katika damu ya utakaso-yaani Yesu Kristo.
Damu ya utakaso ndio muhuri wa Agano la uzima, Maanake uaribifu wote, tauni zote, janga zote zinapita juu yako bila kukuguza wewe na nyumba yako. Hivyo hatima yako itang’ara kwa utukufu wake milele.
Hebu tuone:-
DAMU NDIYO MHURI WA MUNGU KWA UTAKASO.
- Damu si kitu cha kawaida lakini ni ishara inayo tutenga kama watu wa Mungu kutoka kwa hukumu na ghadhabu.
- Isipokuwa dini ya Ukristo, dini zingine zote hazina damu.
- Damu ndiyo ishara ya usalama wako-Kutoka 12:3.
- Tauni za Misri hazingeweza kuwaguza waliokuwa chini ya ile damu ya utakaso.
- Damu ya utakaso inakuzungumzia-Waebrania 12:24.
- Damu ya Yesu Kristo inanena mema kuliko damu ya Habeli.
- Damu ya Yesu Kristo inanena wokovu, upendo, amani na ukombozi.
- Damu ya Habeli inanena laana, hukumu na kisasi.
- Damu ya msalabani ni ngao kutokana na hukumu-Warumi 5:9.
- Tumeokoka kutokana na ghadhabu ya Mungu kupitia kwa damu ya Kristo.
- Damu ya Yesu inanyamazisha mshtaki-Ufunuo 12:11.
- Tunamshinda mshtaki (shetani) kwa damu ya Mwana kondoo, kwa neno la ushuhuda na kwa kutojipenda nafsi yetu mpaka mauti.
- Wana wa Israeli mle Misri kwa damu juu ya miimo ya milango ya nyumba zao-Tauni na lile janga la mauti halikuweza kuwaguza.
- Mahali wengi walikufa, hapo hapo waliokuwa chini ya damu waliishi.
DAMU YA UTAKASO INATUKOMBOA KUTOKANA NA UARIBIFU.
Damu ya utakaso inatukomboa kutokana nguvu za dhambi, mauti na laana ya sheria.
- Damu inatukomboa kutoka dhambini-Waefeso 1:7.
- Tunao ukombozi wetu, msalaba wa dhambi, sawa sawa na wingi wa neema yake.
- Damu inatukomboa kutoka mauti-Waebrania 2:14.
- Yesu Kristo aliharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti (yaani ibilisi) pale msalabani.
- Damu inavunja laana ya vizazi-Wagalatia 3:13.
- Yesu Kristo alitukomboa kutokana na laana ya sheria kupitia dhabihu ya damu yake msalabani.
- Damu yake imeleta na kuidhimisha uzima wa milele-Yohana 6:53-54.
- Anayeipokea damu ya Yesu Kristo amepokea uzima wa milele.
- Rahab wa Yeriko-Yoshua 2:18-19. Kwa ule mshipi mwekundu, ishara ya damu alipata utakaso pamoja na jamii yake, pamoja naye, wakati kuta za Yeriko zilipoanguka.
DAMU YA UTAKASO INAHAKIKISHA ULINZI WA MUNGU.
- Damu ya Yesu Kristo inapotekelezwa kwa njia ya imani, ulinzi, usalama na kinga la Mungu linapatikana.
- Damu inatufunika kutokana na mabaya yote-Zaburi 91:10.
- Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitakukaribia hema yako.
- Damu inadumisha hatima-1 Petro 1:19.
- Damu ya dhamani, ya Yesu Kristo inalinda na kuifadhi maisha yetu.
- Damu ya Yesu Kristo inanyamazisha na kuharibu mavamizi ya shetani-Wakolosai 2:15.
- Kwa damu ya Yesu Kristo, Yesu Kristo alizivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri.
- Damu ya Yesu Kristo inatuletea malaika kutulinda-Kutoka 23:20.
- Mungu anawatuma malaika kuwalinda walio chini ya Agano naye.
- Ayubu alilindwa na kuta zilizowekwa kumlinda-Ayubu 1:9-10.
JINSI YA KUTEMBEA KATIKA NGUVU ZA DAMU YA YESU KRISTO.
- Hili upate kufurahia utakaso wa damu ya mwana kondoo ni lazima kuishi na kutembea katika imani na utii kila saa.
- Tekeleza ile damu kwa imani-Warumi 3:25.
- Damu ya Kristo inafanya kazi kwa wenye imani pekee.
- Ita damu ya Yesu Kristo kwa maombi-Waebrania 10:19.
- Tunamjia Mungu kwa damu ya Yesu.
- Kiri damu ya Yesu Kristo kila saa na kila wakati-Ufunuo 12:11.
- Waambie na kushuhudia watu nguvu na uwezo wa damu ya Yesu Kristo juu ya maisha yako.
- Ishi katika utakatifu chini ya damu ya Yesu Kristo-Waebrania 9:4.
- Damu ya utakaso inatusafisha dhamiri zetu na Matendo mfu, tupate kumwabudu Mungu aliye hai.
- Petro kupitia damu ya utakaso alitengwa kwa wafungwa wote gerezani kwa sababu ya Agano la utakaso na malaika akamkomboa ajabu.
MWISHO
- Damu ya Yesu Kristo ndio mhuri wa utakaso wetu kutoka kwa Mungu.
- Damu ya Yesu inatakasa, inakomboa, inalinda wote walio chini ya damu yake.
- Kinachoua, kinachodhuru, kinachoharibu wengine wasio chini ya damu, hakitaweza kukukaribia.
- Damu ya utakaso, damu ya Yesu Kristo inanena mema, inanena uzima, rehema na ushindi.
- Kutembea katika utakaso, lazima kuishi katika ufahamu na imani katika damu kila siku.
- Shuhudia ukuu na nguvu za damu ya Yesu Kristo kila wakati.
- Je, umeokoka? Je, umejazwa na Roho Mtakatifu, fanya makuu damu ya utakaso-Damu ya Agano.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.