MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI
SOMO: 1 SAMWELI 20:1-3
Kinyume cha imani ni hofu. Kila mtu anazo hofu zake. Mwanadamu ana hofu vitu vingi zaidi. Kamusi ya hofu inaangazia aina za hofu zaidi ya 6000. Tuna hofu ya kuishi na hofu ya kufa. Hofu ya magonjwa na hofu ya uzee, hofu ya leo na hofu ya kesho. Hofu ya kukataliwa na kuachwa. Hofu ya kutofaulu na hofu ya kufaulu. Hofu ziko kwa kila mtu.
Hofu ilianza katika Bustani la Edeni- Mwanzo 3:8-10.
Hofu si mapenzi ya Mungu kwetu kama watoto wa Mungu. 2 Timotheo 1:7 tunaona kwamba shida ya kwanza ya mwanadamu ilikuwa ni hofu. Pamoja na hofu mwanadamu anaona aibu. Aibu ilitangulia hofu. Mpaka hivi leo, shetani anatumia mbinu hizi mbili kama silaha ya kumlenga mwanadamu.
Kabla Adamu hajajua dhambi ya chuki, wivu, ghadhabu, hasira, kiburi, iliyompata kwanza ilikuwa ni aibu na hofu.
Dhambi ya hofu inatujia bila kutarajia. Imani yetu inampendeza Mungu lakini hofu inampendeza shetani.
Kwa njia nyingi tunaruhusu hofu kutawala mioyo yetu.
Biblia inatufundisha zaidi juu ya watu waliopatwa na hofu katika maisha yao na jinsi Mungu aliwasaidia kushinda dhambi ya hofu.
Hebu tuone:-
KISA CHA DAUDI- 1 Samweli 20
- Mfalme Sauli alianza kumwinda Daudi akitafuta kumuua.
- Kwa miaka nyingi Sauli alitaka kuyatoa maisha ya Daudi.
- Daudi kwanza alikimbia NAIOTHI akajificha kwa nyumba ya nabii Samweli.
- Mara tatu mfalme Sauli aliwatuma watu (askari) kumtafuta Daudi kwa nyumba ya nabii Samweli.
- Kila wakati Mungu alimlinda Daudi. Usalama wetu u katika uwepo wa Mungu.
Hali ya shida.
- Hata ingawa Daudi alikuwa na upako wa Mungu na kwamba alikuwa katika mapenzi ya Mungu, bado hatari zilimwandama.
- Mauti yalimwandama Daudi kila mahali lakini uwepo wa Mungu ulikuwa karibu zaidi.
- Maisha yetu ni mafupi zaidi- Yakobo 4:14, Zaburi 39:5, Ayubu 9:25-26, Zaburi 102:11.
- Pamoja na hayo yote Mungu tayari alikuwa amempaka mafuta kuwa mfalme.
- Ahadi za Mungu juu ya maisha na hatima yako ni tumaini kwako hautakufa mpaka ahadi, upako wake kutimia.
- Shida ni kwamba Daudi aliacha hofu kuchukua nafsi kubwa katika maisha yake.
- Hofu ilimfanya Daudi kukimbia toka nyumba ya nabii Samweli. Alikimbilia Gibea.
- Kutoka Gibea, Daudi alikimbilia Ahimeleki na kumdanganya- 1 Samweli 21:1-2.
- Tunapopoteza uwepo wa Mungu tunarudi nyuma na kuishi katika dhambi- Wagalatia 5:17.
- Hofu inatufanya kukimbia, kukimbia nyumba ya Mungu na watu wake na ufalme wa Mungu.
- Hapo mbele siku chache, Daudi alimuua Goliathi aliyekuwa na nguvu zaidi kuliko Sauli, sasa Daudi amemkimbilia Sauli.
- Imani ya Daudi ilipungua kiasi alimkimbia mfalme Sauli.
- Imani ikipungua, hofu inatawala katika mioyo yetu.
Majaribu makuu. Mwanadamu dhaifu.
- Kwa kawaida hofu inatawala zaidi kuliko imani.
- Hata wenye nguvu wanaanguka majaribu yanapokuwa mengi.
- Abrahamu kwa hofu alidanganya kwamba Sarai ni dada yake.
- Musa kwa hofu nyingi alikasirikia watu na kuupiga ule mwamba.
- Kwa hofu Ayubu alilaani siku ya kuzaliwa kwake.
- Nguvu zetu haziwezi kuwa ndani yetu lakini ndani ya Mungu.
- Haijalishi umekuwa ndani ya imani miaka mingapi, majaribu yatakujia kiasi kukimbia kwa hofu.
- Mfalme Yehoshaphati katika hofu yake alimtafuta Mungu kwa maombi na kufunga saumu- 2 Mambo ya nyakati 23:3.
- Kuna hofu za aina mbili katika Biblia:-
Hofu ya kumhofu Mungu- Zaburi 111:10; 112:1; 34:7.
Hofu ya dhambi ambayo ni kukosa imani na tumaini katika Mungu.
- Hofu hii ya dhambi ilimpata Adamu na Hawa, hofu ya aibu na hukumu- Warumi 8:15; Mithali 29:25.
- Hofu ni dhambi ya kukosa imani- Warumi 14:23; Ufunuo 21:8.
- Katika Agano la kale, wenye hofu hawakuruhusiwa kwenda vitani- Kumbukumbu 2:8; Waamuzi 7:3. Wenye hofu ndio wengi.
- Hofu huleta utumwa lakini imani huleta uhuru- Waebrania 2:14-15.
- Hofu ilileta mauti kwa mfalme Sauli na wanawe- 1 Samweli 28:3-20.
- Hofu ya kesho, hofu ya maumivu, hofu ya upweke, hofu ya kukataliwa, hofu ya kuachwa, lakini Mungu anatuokoa na hofu zote kwa imani.
IMANI NDIO DAWA YA HOFU
- Kwa sababu hofu ni roho anayetumia shetani kinyume chetu, ni lazima kupambana na hofu zetu.
- Mungu hapendezwi na hofu ndani ya maisha yetu, hivyo tunahitaji kuishi kwa imani- Warumi 10:17.
- Ni mapenzi ya Mungu tukaishi katika ushindi- Wakolosai 3:1-4.
- Mungu ametuinua juu zaidi ya kila aina ya hofu- 1 Petro 4:1-2.
MWISHO
- tunapopatwa na hofu, tunahitaji kusimama kwa imani.
- Kataa kuishi maisha ya hofu, iwe ni shetani, mwanadamu, nyakati, mauti na uchumi.
- Kwa mara 63 katika Biblia “Usihofu, Usiogope” imetajwa katika Biblia- Maombolezo 3:57.
- Leo hii Bwana anasema tukampe fedheha zetu zote- 1 Petro 5:7.
- Mungu yupo pamoja nawe usiogope.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.