MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA
SOMO: 2 WAFALME 8:7-15.
Mwana philosophia mmoja kwa jina Socrates hapo zamani alisema “jifahamu mwenyewe” na “maisha isiyojulikana aina maana kuishi” “The unknown life is not worthy living.” Kila mtu anaye mbwa ndani yake. Miti mikubwa inaanguka kwa upepo na dhoruba. Saa nyingine mtu anafanya jambo linalo washangaza watu wote. Nani alifikiri mtu kama TD Jakes alikuwa shoga? Na pia Tony Evans? Elisha alienda mpaka Dameski, kule mfalme wa Shamu alikotoka Naamani. Dameski ilikuwa mji mkuu wa Shamu (Aramu). Shamu ndio alikuwa adui mkuu wa Israeli. Shamu ndio walikuwa na mfalme aitwaye Beni-Hadadi (mwana wa Hadadi). Yule mfalme aliyetaka kumkamata Elisha na kumuua. Elisha alipofika kule, mfalme Beni-Hadadi alikuwa mgonjwa karibu kufa.
Kila mtu anakuwa bila nguvu mbele ya mauti. Mauti si mweshimu mwanadamu yeyote!!
Tajiri kwa maskini, msomi na mjinga, mwenye nguvu na mwenye hoi, mjumbe au mfungwa, mtoto na mkubwa, mfalme au raia. Beni Hadadi kweli alikuwa mgonjwa sana.
Madaktari wote walishindwa ugonjwa wake mfalme, pia na waganga wote.
Hivyo mfalme Beni Hadadi amesikia yule mtu wa Mungu aliyemponya Naamani yuko mjini Dameski. Basi, mfalme akamtuma jemedari wake aitwaye Hazaeli kwa Elisha.
- Badala ya kumtuma kwa Elisha kuomba maombi ya uponyaji, anatumana swali “je, nitapona ujonjwa huu au nitakufa?”
- Miungu yake ya sanamu imemwangusha kabisa.
- Nabii Elisha alipomwona Hazaeli hakushtuka kamwe maana Mungu amemjulisha tayari.
- Hazaeli alifika kwa Elisha na ngamia 40 ya mali ya dhamani sana.
- Hatujui kama Elisha alikataa kupokea zawadi ile au alikataa kama jinsi alikataa zawadi kutoka kwa Naamani.
- Basi kwa swali ya Ben Hadadi “nitapona au nitakufa?” Elisha alimwambia Hazaeli mambo mawili, habari njema na habari mbaya.
- Mfalme ataenda kufa.
- Lakini si kwa ugonjwa ule.
- Elisha alipomwambia Hazaeli habari hizo Elisha alianza kulia!! Hazaeli alichanganyikiwa sana kwa jibu la Elisha.
- Hazaeli alimlaza Elisha, “Bwana wangu kwa nini unalia?”
- Ndiposa Elisha akamwambia, Hazaeli “ni kwa sababu yako wewe Hazaeli, ninalia.”
- Ndipo Elisha akamweleza Hazaeli jinsi atamuua mfalme wake Ben Hadadi na kuchukua ufalme wake, jinsi akiwa mfalme atavamia Israeli na kuwauwa watoto na wanawake wenye uzito wa minba.
- Ndipo Hazaeli jemedari alimuuliza Elisha “Je, mimi ni mbwa?” mnyama ndie anaweza kufanya mambo hayo.
- “Je, hivyo ndivyo unavyo nifikiria-Elisha?”
- Elisha alimweleza Hazaeli “Bwana amenijulisha mambo hayo yote.”
- Hazaeli alirudi kwa makao ya mfalme Ben-Hadadi.
- Alipofika kwa mfalme, hakumwambia kweli yote bali alimwambia nusu yake. “Hautakufa kwa ugonjwa huu ulionao.”
- Hata hivyo mfalme Ben-Hidadi alifurahi na akalala.
- Mfalme alipolala-Hazaeli alienda kupanga jinsi atakavyo muua mfalme Ben-Hidadi.
- Basi Hazaeli alipojua mfalme amelala na hana nguvu kwa sababu ya ugonjwa wake.
- Alishuka godoro, au pazia, au taulo kubwa akailowesha maji, akamfunika mfalme hasipate hewa ya kupumua mpaka mfalme Ben-Hidadi akafa.
- Alipokuwa pale na hio towel au godoro Hazaeli alikumbuka kweli kunao mbwa ndani yake.
- Petro hakujua kulikuwa na mbwa ndani yake alipomkana Yesu Kristo. Hebu tujifunze:-
KWA KWELI WENGI WETU HATUJIFAHAMU NAFSI ZETU.
- Kweli hatujijui nafsi zetu, hatujui maovu yanakaa ndani ya mioyo yetu, hatujui tunao uwezo wa kufanya maovu mabaya zaidi.
- Walimwengu wanasema (humanism) mwanadamu asili yake ni mbaya (evil) kwa asili yetu sisi si wazuri lakini wabaya, Noma!!
- Walimwengu wanasema mwanadamu anaendelea kuwa mzuri sana (utopia).
- Hazaeli hakujua anaweza kumtenda mfalme Ben-Hadadi maovu kiasi ya kumuua mfalme na kwa njia ile aliotumia.
- Aliuliza, Kwani mimi ni mbwa? Lakini alikua mbaya zaidi kuliko mbwa.
- Wengi wetu tunaamini tunaweza kuvunja amri ya 1, 2 na 6 lakini hawezi kuvunja amri ya 3, 5 na 8-Kutoka 20:1-17.
- Je, unafahamu uovu unaokaa ndani yako?
- Usicheze na watu na zaidi watu unaolala karibu nao, watu wanaokupikia chakula, wanaokupa chakula chochote na kinywaji!!
- Biblia inasema, “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha. Nani anaweza kuujua?”-Yeremia 17:9.
- Katika amri kumi za Mungu ni gani unavunja kwa rahisi zaidi?-Kutoka 20:1-17.
- Hakuna ajuaye ouvu na ukatili unaokaa ndani yake, isipokuwa Mungu pekee.
KUNA UOVU NDANI YETU SOTE, UOVU HUU UNANGOJEA NAFSI UTOKE NJE.
- Uovu unakaa ndani ya kifua cha kila mtakatifu.
- Uovu unakaa katika kifua cha kila mwenye dhambi mualifu.
- Kila mwanadamu anao sehemu tatu-mwili, nafsi na roho.
- Tunapodharau nafsi na roho na kutojali neno la Mungu-Mabaya yatakayo tokea (Hebu tazama mauaji ya maandamano). Polisi wanalenga vijana kwa bunduku zao na kuua!!
- Shida ni mioyo yetu na roho zetu zisizo na Mungu.
- Kuna mbwa mkubwa ndani yako, huyu mbwa anapigana na roho yako.
- Ukimpa nafasi huyu mbwa atatoka mchana kila mtu akiona!!
- Ukiacha mlango wazi huyu mbwa atatoka na kuwauwa watu.
KUJIKATAA SI GUARANTEE.
- Kama ungemuuliza Adamu kwamba atakula lile tunda alilokatazwa na Mungu Adamu angesema, “mimi siwezi-kwani mimi ni mbwa?”
- Kama ungemwambia Sulemani juu ya ibada ya sanamu angesema mimi siwezi kumwacha Mungu “kwani mimi ni mbwa?”
- Kama ungemwambia mfalme Daudi alipoandika Zaburi 23 kwamba atafanya uasherati na Bathsheba na kumuua Uria-“Je, mimi ni mbwa?”
- Kama ungemwambia Petro atamkana Kristo mara tatu-“Je, mimi ni mbwa?”
- Ulipokuwa mtoto haukuwa na tamaa ya uasherati-lakini sasa?
- Tambua kuna mbwa ndani yako lakini pengine amelala, saa ingine unamsikia mbwa anataka kutoka na kuwika-kubweka.
- Jifahamu moyo, nafsi na mwili wako. Jua sana nguvu na udhaifu wako, linda moyo wako, funga sana huyo mbwa wako.
TAMAA NA MAFIKIRA YAKO YANAKUONGOZA KWA MAOVU.
- Kwanza, mawazo yanaingia katika kichwa-2 Wakorintho 10:3-6. Je, Elisha ndiye alimpa Hazaeli mbinu za kumuua mfalme Ben-Hadadi? La, mawazo ya kuua ilikuwa tayari ndani yake.
- Pili, majaribu yanatoka kwa mawazo yetu. Tamaa ya kuwa mfalme tayari ilikuwa ndani ya Hazaeli.
- Tamaa, inakaa ndani yetu na mazoezi ya dhambi tunayafanya ndani yetu mara nyingi.
- Kila wazo, tamaa zatu zinalisha yule mbwa ndani yetu.
- Dhambi ni tamaa iliyopata nafasi (desire+opportunity=sin).
- Kudhibiti tamaa si kushinda dhambi (repressed desire is not winning over sin).
- Baadaye tunasema je, mimi ni mbwa?
MWISHO.
- Kubali moyo wako ni dhaifu na ni ovu na dhambi kila wakati imo mlangoni mwako-Mwanzo 4:6-7.
- Jiadhari sana wewe unayefikiri unasimama.
- Peleleza moyo wako. Je, unasikia mbwa ndani yako?
- Ikiwa tayari umeanguka-
- Yesu angali anakupenda.
- Anajua dhambi zako.
- Hawezi akakutupa mbali.
- Ungama dhambi zako-1 Yohana 1:8-9. Mshukuru Mungu, tubu-1 Yohana 2:1-2.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.