Categories: Swahili Service

FURAHA YA WENYEJI WA UFALME WA MUNGU.

MFULULIZO: JINSI YA KUISHI MAISHA YA UFALME WA MUNGU.

SOMO: WAFILIPI 3:20-21.

 

Zaidi tunapofahamu utambulisho wetu kama wenyeji wa ufalme wa Mungu, ndiposa tutakapopata ujuzi kamili wa furaha inayoletwa na ufalme wa Mungu.

“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni, kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo-Wafilipi 3:20.

Wenyeji unakuja pamoja na haki na marupurupu na jukumu. Katika maisha ya asili hapa duniani, watu wanadhamini sana wenyeji wa nchi, taifa na falme zao. Hii ni kwa sababu wenyeji (citizenship) inawapatia watu mali, usalama na kitambulisho.

Sisi kama Wakristo wenyeji ulio maana sana si utaifa wetu hapa duniani, lakini utaifa na wenyeji wetu katika ufalme wa Mungu.

Mtu anapompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mkombozi wa maisha yake, huyo mtu anahamishwa kutoka ufalme wa giza na kuingia katika ufalme wa nuru-ufalme wa mwana wa upendo wake-Wakolosai 1:13.

Kuwa mwenyeji wa mbinguni na usalama wa Mungu ni kiini kikubwa na kinatupa furaha kwa sababu kinahakikisha usalama wa milele, utoshelevu na amani isiyo na kifani. Mataifa ya ulimwengu huu yana kikomo, lakini ufalme wa Mungu ni wa milele na huwezi kushindwa na chochote kile.

Wakristo wengi sana hawana hakika juu ya ufalme wa Mungu, hawana furaha na ujasiri unaotokana na wenyeji wa mbinguni.

Wengi wanaishi katika hofu, wasi wasi na majuto. Hawajui utajiri ulio wao katika Kristo Yesu.

Leo, tusome na kutambua furaha ya wenyeji wa ufalme wa Mungu na jinsi ya kutekeleza furaha ya Mungu katika maisha ya kila siku. Hebu tutazame:-

WENYEJI WA UFALME WA MUNGU UTUPATIA FURAHA YA WOKOVU.

  • Wokovu ndio faida kubwa zaidi ya kuwa wenyeji wa ufalme wa Mungu.
  1. Majina yetu yameandikwa mbinguni.
    • Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake wafurahi. Si kwa sababu ya mamlaka, lakini kwa sababu majina yao yameandikwa mbinguni-Luka 10:17-20.
  2. Tumekombolewa kutoka dhambi na hukumu.
    • Kupitia Yesu Kristo tumewekwa huru kutoka utumwa wa dhambi-Warumi 8:1-2.
  3. Tumepata hakika ya uzima wa milele.
    • Wenyeji wa ufalme Mungu unatupatia tumaini ya uzima wa milele katika Yesu Kristo-Yohana 3:16; 1:11-13.
  4. Tumefanyika wana (adopted) katika jamii ya Mungu.
    • Tumekuwa wenyeji wa ufalme wa Mungu, sisi si tena watumwa, lakini tumekuwa wana wa Mungu-Warumi 8:15.
    • Furaha aliyepata yule towashi wa Kushi.
    • Alipompokea Yesu Kristo kupitia mahubiri yake Filipo yule towashi alienda zake akiwa mwenye furaha nyingi kwa kuingia katika ufalme wa Mungu.

UFALME WA MUNGU NI UFALME WA HAKI, AMANI, NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU.

  • Tofauti na falme za dunia hii, ufalme wa Mungu unatupatia amani na furaha kamili.
  1. Ufalme wa Mungu si mali ya ulimwengu.
    • Furaha ya kweli inatoka kwa Mungu pekee si kutoka vitu na mali-Warumi 14:17.
  2. Amani huja tunapotambua na kufahamu kwamba tuko katika mikono ya Mungu.
    • Amani ya Mungu inahifadhi mioyo yetu na nia zetu-Wafilipi 4:7.
  3. Roho Mtakatifu ndiye kiini hasa cha furaha ya ufalme.
    • Yesu Kristo alisema furaha yake itadumu ndani yetu kupitia Roho Mtakatifu.
  4. Furaha yetu inapatikana tunapoteka maji kutoka chemi chemi za wokovu.
    • Wokovu unaleta mafuriko ya furaha katika maisha yetu-Isaya 12:3-6.

WENYEJI WA UFALME WA MUNGU UNATUPATIA NJIA YA UTOSHELEVU WA MUNGU.

  • Wenyeji wa ufalme wa Mungu unatupatia utajiri wa mbinguni.
  1. Mungu anawashugulikia walio wake.
    • Yesu Kristo alituakikishia kwamba baba yake aliye mbinguni atashugulikia kamili-Mathayo 6:31-33.
  2. Tunapotoshelezwa na Mungu.
    • Mfalme Daudi alitangaza “Mungu ndiye mchungaji wangu”-Zaburi 23:1-6.
  3. Mahitaji yetu yanatimizwa sawa sawa na utajiri wa Mungu-Wafilipi 4:19.
  4. Wenyeji wa mbinguni hawaishi kwa hofu ya kukosa chochote.
    • Mungu ametupa Roho ya nguvu, upendo na kiasi-2 Timotheo 1:7.
    • Yule mjane wa Zeraphathi aliona uaminifu wa Mungu wakati wa njaa kali-1 Wafalme 17:13-16.
    • Unga wake na mafuta ya kupika yalidumu siku zote.

WENYEJI WA UFALME WA MUNGU WANALINDWA NA MUNGU.

  • Ufalme wa Mungu ni mahali pa ulinzi na salama.
  1. Tunalindwa chini ya mabawa ya Mungu.
    • Yeye anayeishi katika mahali pa siri pake aliye juu, atakaa mahali pa siri pake Mwenyezi-Zaburi 91:1-4.
  2. Malaika wanawalinda wana wa ufalme wake Mungu.
    • Mungu anawatangazia malaika zake wakulinde katika njia zako zote-Zaburi 91:11.
  3. Hakuna silaha yeyote itafaulu.
    • Wana wa ufalme wa Mungu wanalindwa kutoka adui wote-Isaya 54:17.
  4. Tunamshinda adui kwa damu ya mwana kondoo.
    • Tumepewa ushindi wote juu ya adui zetu-Ufunuo 12:11.
    • Hata Danieli alilindwa katika tundu la simba-Danieli 6:22.

WENYEJI WA UFALME WA MUNGU MAANAKE NI KWAMBA TUNAWAKILISHA MUNGU DUNIANI.

  • Kama wenyeji wa ufalme wa Mungu sisi tu mabalozi wa Mungu duniani.
  1. Sisi tuwakilishi wa Yesu Kristo.
    • Tumeitwa kuishi katika ufalme wa Mungu humu duniani-2 Wakorintho 5:20.
  2. Maisha na tabia zetu lazima kuonyesha tabia za mbinguni.
    • Sisi ni nuru ya ulimwengu, lazima tuangaze-Mathayo 5:14-16.
  3. Ni lazima kutangaza Injili ya ufalme wa Mungu-Mathayo 28:18-20.
  4. Wenyeji wa ufalme wa Mungu lazima waishi sawa sawa na sheria za ufalme.
    • Wanafunzi na mitume wa Yesu Kristo waliwakilisha ufalme wa mbinguni vizuri sana-Matendo 4:18-20.
    • Walikataa kunyamaza juu ya imani yao katika Bwana.

MWISHO.

  • Furaha ya wenyeji wa ufalme wa Mungu haitegemei hali ilivyo duniani bali wanategemea Mungu asiyebadilika.
  • Kama wenyeji wa mbinguni tumepewa wokovu, amani, ulinzi na uzima wa milele.
  • Furaha yetu ni kwamba tumeokoka kabisa, tumeaidiwa ufalme mwema zaidi kuliko falme za dunia hii.
  • Je, umeokoka? Je, unaishi kifalme?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE

TEXT: LUKE 2:1-14.   The birth of Jesus Christ shattered spiritual, social and eternal barriers,…

15 hours ago

CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME?

TEXT: JOHN 3:16-17.   Christmas unveils the divine mission behind the birth of Jesus Christ;…

1 day ago

KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA

MFULULIZO: KRISMASI NI KUFUNULIWA KWA YESU KRISTO.  SOMO: LUKA 2:8-14.   Krismasi inafunua jibu la…

5 days ago

CHRISTMAS IS WHEN HEAVEN CAME DOWN TO EARTH.

SERIES: CHRISTMAS IS CHRIST. TEXT: JOHN 1:1-14.   Christmas is the divine moment when God…

5 days ago

FOR GOD SO LOVED THE WORLD

TEXT: ISAIAH 53:1-12.   The son of man came to seek and save that which…

5 days ago

JESUS OUR SAVIOR

SERIES: CHRISTMAS IS JESUS CHRIST. TEXT: MATTHEW 1:21   Jesus Christ is the savior of…

2 weeks ago