Categories: Swahili Service

HABARI NJEMA KUTOKA MBINGUNI

MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA

SOMO: YOHANA 3:16

 

Siku hizi ni kama kila mtu anazo habari za kueleza. Wanahabari na watangazaji wanataka uwasikilize, wanasiasa pia, wahubiri na sikiza na Citizen. Lakina kuna Yeye anenaye kutoka mbinguni. Mungu baba anao ujumbe kwa ajili yako na mimi. Mungu anaponena nawe anasema nini? Hebu tuone:-

MUNGU ANA UJUMBE KWAKO JUU YA UPENDO

Kiini cha upendo:

  • Huu si upendo wa mwanadamu- upendo wa mwanadamu unao ubinafsi.
  • Upendo wa mwanadamu unategemea kile utapata.
  • Upendo wa Mungu ni upendo takatifu, upendo wa Mungu utatafuta mazuri kwa ajili yako.
  • Upendo wa Mungu unakutakia mema, ni upendo wa milele- Yeremia 31:3.
  • Upendo wa Mungu unapenda bila kupendwa- 1 Yohana 4:19- Mungu alitupenda kwanza.

Ukuu wa upendo wa Mungu:

  • Biblia inasema upana wa upendo wa Mungu ni kwa ulimwengu wote.
  • Mungu hajui mtu asiyempenda. Kwa upendo Mungu alimtoa Mwana wake wa pekee- 1 Yohana 4:8, 16.
  • Mungu anapenda watu na hakuna chochote kinaweza kumfanya Mungu asikupende- Warumi 8:38-39.

Sadaka ya upendo:

  • Upendo unatoa- kipimo cha upendo ni sadaka.
  • Mungu aliupenda ulimwengu, akamtoa Mwana wake wa pekee (Begotten).
  • Sura ya upendo ni msalaba. Msalaba ni asili ya mema ya Mungu- Warumi 5:8; Yohana 15:13; 1 Petro 3:18.

MUNGU ANA UJUMBE KWAKO JUU YA UZIMA

Dhamana ya uzima: (worthy of life)

  • Mungu hakupenda tuangamie dhambini.
  • Pamoja na dhambi zetu, Kristo alitufia msalabani- Warumi 8:7.
  • Mwanadamu ni mwenye dhambi, dhambi ni kinyume ya Mungu.
  • Mungu anapenda uzima, mwanadamu anapenda kuua (abortion)-uavyaji mimba, (euthanasia)- kuua wazee na wagonjwa, kuua maskini na mauaji ya halaiki (genocide).

Fadhaha ya maisha: (the worry of life).

  • Fadhaha kuu duniani ni kifo.
  • Fadhaha ya kifo ni kubwa kuliko fadhaha ya saratani (cancer), kupoteza mtoto, kupoteza wazazi.
  • Fadhaha kuu zaidi ni kuishi maisha yako na baadaye kupotea jehanamu daima- Zaburi 9:17; 2 Wathesalonike 1:8-9.
  • Mwisho wa watu wengi ni kupotea jehanamu hata wenye dini- Mathayo 7:21-23.

Ajabu ya uzima: (the wonder of life)

  • Si kila mtu anapotea katika moto wa jehanamu, walio okoka wamepata uzima yaani Yesu Kristo- Yohana 11:25-26.
  • Roho zao walio na Yesu Kristo, wataishi milele na milele- 2 Wakorintho 5:1-8; Wafilipi 1:23.
  • Tofauti ya walio okoka na wale wamepotea ni- Yohana 5:10-13.

MUNGU ANA UJUMBE KWAKO JUU YA WAJIBU

Kuna wajibu kwa wote:

  • Yesu Kristo anasema tofauti ya mtu aliyeokoka na asiye okoka ni kuamini- imani.
  • Kila mtu anayeamini na kumtegemea- tulio na Yesu Kristo na tumemwamini kutuokoa- Warumi 16:9-10; Matendo 16:31; Waefeso 2:8-9.

Kuna wajibu wa binafsi:

  • Ikiwa utaenda jehanamu, utajilaumu mwenyewe.
  • Hakuna mtu anaweza kukuchukulia wajibu wako kuokoa- Ufunuo 20:11-15.
  • Leo mtazame Kristo, yeye ndiye wokovu wako- Yohana 5:39-40, 8:24; Hesabu 21:4-10.
  • Mtazame Yesu Kristo upate kuishi.

MWISHO

  • Ikiwa umeokoka mshukuru Mungu leo.
  • Ikiwa bado kuokoka, mjie Kristo hivi sasa.
  • Ujumbe wa Mungu ni wokovu kwetu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

4 days ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

4 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

4 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

2 weeks ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

4 weeks ago

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

1 month ago