Categories: Swahili Service

HAIJAISHA MPAKA MUNGU ASEME IMEKWISHA

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA

SOMO: 2 WAFALME 13:14-21

 

Wengi walisema kifo cha Elisha kilikuwa mwisho wake na huduma yake. Lakini Mungu aliendelea kumtumia Elisha hata katika kaburi lake!! Benny Hinn angali anaenda kupokea nguvu zake kwa kaburi ya Kathryn Kulman. Hivyo wewe nami tusijihuzuru katika kazi ya Mungu mpaka mauti na zaidi hata kukiwa kaburi zetu tutafute kuacha Kumbukumbu na mifumo ya urithi (legacy) kwa watoto wetu (never give up!! It is not over until God says it is over).

  • Yachiro Miura alipanda mlima wa Everest akiwa miaka 80.
  • Gladys Burrill alikuwa miaka 92 wakati alimaliza Olympic marathon.

Leo twatamatisha mfululiza juu ya Maisha na nyakati za Elisha katika 2 Wafalme 13.

Elisha alikuwa na umri wa miaka 80. Alianza huduma ya unabii akiwa miaka 25. Elisha alimtumikia Eliya kwa miaka 7. Aliendelea kumtumikia Mungu kwa miaka 48. 

Elisha sasa ni mgonjwa sana, pengine utasema kwa Elisha hajastaafu kazi ya unabii. Lakini anaendelea kutumika mpaka siku ya mwisho hapa duniani na leo twaona hata kaburini mwake bado Elisha anafanya kazi na miujiza!! Hebu tuone:-

TUMIKIA MUNGU WAKO MPAKA MWISHO-2 Wafalme 13:14-20.

  • Kwa sasa Elisha alikuwa bila nguvu, ni mgonjwa sana na ugonjwa wa mwisho.
  • Mungu atakuponya magonjwa yako yote lakini si ugonjwa wa mwisho!!
  • Ugonjwa wa mwisho ndio utakao kuua!!
  • Elisha alikuwa bado na jambo moja la kufanya kabla ya kufa kwake.
  • Ilimbidi kumtolea unabii mfalme Yoashi, mfalme wa Israeli.
  • Huu ulikuwa unabii mwafaka kwa sababu atakalofanya mfalme Yoashi ndivyo siku zake za usoni zitakavyokuwa.
  • Elisha alimwambia “piga mshale wako kuelekea mashariki.” Hivi nabii Elisha akatabiri ushindi juu ya Shamu na adui za Israeli.
  • Pili Elisha alimwambia mfalme Yoashi achukue mishale na kuendelea kupiga.
  • Lakini mfalme Yoashi kwa uzembe wake alipiga mara tatu.
  • Moyo wa Elisha ulivunjika sana. Kama mfalme Yoashi angeendelea kupiga mishale yote, kila mshale ulikuwa ni ishara ya ushindi juu ya adui zake Israeli yote!!
  • Hivyo mfalme Yoashi akajidhibiti kwa jinsi alichoka kupiga mishale.
  • Somo kwetu ni:-
  1. Amri za Mungu ni za kutii mpaka atakaposema mwisho!!
  2. Wakristo wengi wamejiuzulu kumtumikia Mungu wao.
  3. Wengi wanaacha kazi ya Mungu hata kwa sababu wanao hawana jambo au chochote cha kutoa kwa Mungu.
  4. Wengine wanaacha kazi ya Mungu kwa sababu hawataki kuendelea.
  • Siku moja mmishonari alitembelea kazi huko Amerika kusizi (South Amerika). Kwa hospitali ya kanisa aliingia kwa wadi ya watu wenye ukoma.
  • Hapo alimwona mtu ambaye alikuwa na ukoma zaidi kiasi. Vidole vyake vyote vya miguu na mikono zilikuwa zimekatika, sehemu za uso wake zilikuwa zimekatika mpaka masikio yake.
  • Ulimi pia ulikuwa umekatika na meno kutoweka!!
  • Lakini huyu mtu alikuwa na furaha nyingi sana, alionyesha kwa mikono wake kuelekea juu mbinguni.
  • Ndipo mmishonari akauliza daktari, je, kwa nini anafurahi na kuelekeza mikono juu mbinguni?
  • Ndipo akwamwambia, “huyu mtu alikuwa mhubiri wa Injili katika vijiji kwa miaka mimgi, sasa kwa ukoma hawezi kwa hivyo anawaelekezea watu wote mbinguni kwa furaha kupata kiasi!!
  • Je, wewe na mimi tutaendelea kumshuhudia Yesu Kristo mpaka mwisho?

WAACHIE WATU KUMBUKUMBU NA URITHI MFUMO WA KUIGA (Leave a legacy)-2 Wafalme 13:20-21.

  • Jambo la ajabu, Elisha aliishi katika upako wa Roho Mtakatifu kwa miaka mingi.
  • Elisha alifanya miujiza mimgi na ishara za ajabu kuu.
  • Elisha alimtumikia Mungu wake kwa nguvu zote na moyo wake wote.
  • Lakini Elisha alikufa na kuzikwa kaburi.
  • Pengine ungesema kasi na huduma za kazi ya Elisha pia ilikufa.
  • Pengine utasema mwisho wa Elisha na miujiza yake ndio mwisho kabisa.
  • Lakini bado mwisho, mpaka Mungu aseme huu ndio mwisho.
  • Nguvu za kuponya na kufufua wafu bado zilikuwa na Elisha hata kaburini mwake.
  • Hata mwili wake ukiwa umeoza na kuwa mavumbi. Bado kulikuwa na muujiza mmoja zaidi. Muujiza mmoja katika Kumbukumbu yake Elisha.
  • Je, tutawacha Kumbukumbu kwa njia gani?
  1. Kupitia jamii yako.
  • Ishi maisha yako mbele ya watoto wako, waachie kitu cha kuiga.
  • Wafundishe watoto wako jinsi ya kufanya kazi kwa bidii, kufaulu maishani.
  • Waonyeshe jisni ya kuwapenda mke au mume wao.
  • Wafundishe jinsi ya kuwa waaminifu kila mahali.
  • Ikiwa umechoma maisha yako, basi wafundishe jinsi ya kutochoma maisha yao kama jinsi ulifanya!!
  1. Kuwa kielelezo kwa huduma.
  • Waonyeshe watoto wako missioni ya Injili.
  • Waachie Kumbukumbu ya kumtumikia Mungu kwa kuwasaidia wagonjwa, maskini na waliopotea dhambini.
  1. Kupitia maombi yako.
  • Maombi yako yanaendelea kuishi miaka baada ya kifo chako.
  • Fundisha jamii yako kuomba na kumtegemea Mungu katika kila hali.
  • Ombea maisha ya watoto wako, wake wao, waume wao hata kabla hawajaoa.

KUFUFUKA KWA YESU KRISTO.

  • Katika siku ya chakula cha mwisho (last supper) shetani aliweka mtego juu ya Yesu Kristo.
  • Kristo alikamatwa, akahukumiwa na kuhukumiwa kifo-Yohana 19:17-18.
  • Walimpeleka mpaka Golgotha wakamslubisha msalabani.
  • Yesu alipokufa shetani alishangilia sana kwa kuona kwamba ameshinda.
  • Yusufu aliutoa mwili wa Yesu Kristo akauzika-Mathayo 27:59-60.
  • Walimfunga Kristo sanda, kaburini waliweka jiwe kubwa na mhuri wa Roma, askari wengi walishika doria.
  • Tumaini ya wote, wanafunzi wake ilididimia ndani yao.
  • Wengi waliona shetani ameshinda vita vyote juu ya Masihi, Yesu Kristo.
  • Lakini jibu lilikuja siku ya Jumapili. Kuna nuru gizani, kuna tumaini katika giza-Mathayo 28:1-7.
  • Wakolosai 2:13-15 ushindi wa shetani ulididimia mara moja.
  • Yesu alifufuka kutoka kwa wafu.
  • Yesu Kristo ametuachia Kumbukumbu ya ushindi, ufufuo na wokovu wa milele-Yohana 11:25-26.

MWISHO

  • Je, ni Kumbukumbu gani utawaachia watu?
  • Je, umepanga kuvumilia mpaka mwisho na zaidi ya kifo?
  • Elisha katika mauti alifufua maiti.
  • Je, umekuwa na hakika ya wokovu wako?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago