Categories: RESURRECTION SUNDAY

HAIKUWEZEKANA KRISTO ASHIKWE NA KABURI

MATENDO 2:22-28

UTANGULIZI

Mwokozi Yesu Kristo aliuona uchungu wa mauti. Mwili wake ulikufa kweli, kweli. Lakini Kristo hakuona uaribifu maana Kristo alikuwa bila dhambi, dhambi ndio huleta uaribifu na kuoza na wadudu waletao kuoza. Hivyo mwili wa Kristo ulikombolewa na ufufuo ,Kristo asishikwe na kaburi. Kaburi inashika watu, ili mauti yafanye kazi kamilifu. Mfalme            Theodosius wa Ugiriki aliwafungulia huru     wafungwa wote, Basi akasema, “Ninaomba Mungu naye afungue makaburi yote na kuwapa wafu wote uzima kutoka kwa mauti” Siku moja maombi ya Theodosius yatajibiwa, wafu watafufuliwa (Danieli 12:1-4)

Hebu tuone:-

I.  HAIKUWEZEKANA NGUVU ZA MAUTI KUMSHIKA BWANA.

  • Ukuu wa Yesu Kristo uko juu ya nguvu za mauti.
  1. Kristo alikuwa na uwezo wa kuweka maisha yake chini nayachukue tena (Yohana 10:18)
  2. Kristo alikuwa katika umoja na Baba na Roho mtakatifu katika ukamilifu wa utatu wa Mungu.
  3. Kristo alikuwa amemaliza kazi yote ya ukombozi wetu.
  4. Kristo alikuwa na ofisi ya Kuhani Mkuu katika enzi ya Melchizdeki (Waebrania 6:20)
  • Alikuwa mfalme wa milele (Zaburi 45:6)
  • Alikuwa mchungaji wa milele (waebrania 13:20)
  1. Kama Kristo angeshikwa na kaburi;
  • Hakuna hakika ya ufufuo (I Wakorintho 15:17)
  • Hakuna kuhesabiwa haki (Warumi 4:25)
  • Hakuna mwombezi mbinguni (Waebrania 9:24)

II.  HAIWEZEKANI NGUVU ZOZOTE KUSHIKA UFALME WAKE.

  1. Philosophia za Roma, Ugiriki na nguvu za ufamle wa giza hazitashika kazi ya kanisa la Kristo.
  2. Masomo ya wasomi wote na elimu yao haitashika injili ya msalaba (I Wakorintho 1:20)
  3. Ujinga wa vizazi hautashika injili ya Kristo (Mathayo 11:5, Mathayo 4:16)
  4. Mamlaka, utajiri, mapambo, uogo na desturi za dunia hii hazitashika ufamle wake (Matendo 4:26)
  5. Uovu wa dunia hii ni mapambo ya dunia, haitashika kabisa ufalme wa Kristo duniani (Yohana 16:33)
  6. Nguvu za uchawi, ibada za shetani kanisani hazitaweza kushika kazi ya injili (mathayo 16:18)

 

III. HAIWEZEKANI KUSHIKA MATEKA CHOCHOTE KILICHO CHA KRISTO

  1. Mwenye dhambi dhaifu ataweza kwenda huru leo (Zaburi 124:7)
  2. Mtakatifu wa Mungu hatashikwa mateka na dhiki, majaribu na mateso (Zaburi 34:19, 116:7)
  3. Miili ya watakatifu haitashikwa na kaburi siku zote (I Wakorintho 15:23, I Petro 1:3-5)
  4. Viumbe vyote havitakaa siku zote katika kuugua katika uchungu (warumi 8:21)

 

MWISHO

  1. Haikuwezekana mauti na kaburi kumshika Kristo.
  2. Haitawezekana dhambi, mauti na kaburi kukushika Mwana wa Mungu.
  3. Leo uemokoka ? Leo tembea naye daima.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

15 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

17 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

19 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago