Categories: Swahili Service

HAIKUWEZEKANA KRISTO ASHIKWE NA MAUTI

MFULULIZO: PASAKA 2024

SOMO: MATENDO 2:22-36

 

Kweli haikuwezekana Mwokozi wetu Yesu Kristo ashikwe na mauti na kaburi. Alifufuka siku ya tatu-Haleluya.

Yesu Kristo alionja mauti kwa ajili yetu, akakufa hivyo hatuna haja ya hofu tena. Leo tunatazama ujumbe wa kwanza wa Injili ya Yesu Kristo.

Kwa ujumbe huo wa kwanza wa Injili tunaona kwamba kufufuka kwa wafu ndio ujumbe wa maana zaidi katika Injili.

Kwa maana kama imani yetu inasalia pale msalabani, basi tunapoteza ukweli ulio mkuu zaidi katika Ukristo.

Kama tukitulia pale msalabani tunaona uchungu na upendo wa Yesu Kristo lakini tupoteze tumaini na nguvu zinazo tufungua kuona uzima ulio tele aliyetuahidi.

Tukisimama pale msalabani tunaona hukumu na nguvu za dhambi, lakini tupoteze “maisha ya kufufuka” ahadi tuliyo nayo kutoka kwake.

Katika Ukristo kunao mahali mbili ambapo tunapokea nguvu zetu, yaani msalabani (damu) na kaburi iliyo wazi.

Mtume Petro alitangaza kwa ujasiri mkuu katika Matendo 2:24, “Ambaye Mungu alimfufua akiufungua uchungu wa mauti. Kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao, Zaburi 16:8-11.

  • Hapa mtume Petro anatangaza kwamba ilipofika kwa Yesu Kristo adui mkuu wa mwanadamu, yaani mauti. Mauti haingeweza kumshika Yesu Kristo.
  • Hii ni kwa sababu haingewezekana mauti kumshika (it was not possible).

HAIKUWEZEKANA NGUVU ZA MAUTI KUMFUNGA YESU KRISTO.

  • Haikuwezekana kuzuia mfungwa gerezani huyu mfungwa akiwa na kifunguo chake zaidi.
  • Kupitia Kalvari Yesu Kristo alikuwa na kifunguo cha “mauti” jehanamu na kaburi.
  • Yesu alikuwa na uwezo wa kutumia vifunguo vyote.

Yesu alikuwa na uwezo wa kufa na kufufuka-Yohana 10:17-18.

  • Yesu Kristo alikuwa na ufunguo wa mauti, kaburi na kuzimu, pia alikuwa na uwezo, mamlaka na nguvu.
  • Yesu Kristo yuko na nguvu za uzima na ufufuo.
  • Yesu alimwambia Martha na Mariamu “Mimi ndimi ufufuo na uzima”-Yohana 11:24-26.
  • Uliza Lazaro aliye fufuliwa baada ya siku tatu kaburini.
  • Uliza mjane wa kule Naini jinsi mwanawe alifufuliwa kwa mauti tayari akipelekwa kaburini.
  • Uliza Jairo jinsi Binti yake alifufuliwa na Yesu Kristo. Yesu alisema “Binti ishi.”
  • Zamani miaka 200 iliyopita, palikuwa na malkia aliyekuwa kafiri, hakumwamini Mungu na uwepo wake. Hakuamini ufufuo wa wafu na nguvu za Mungu.

Alikufa akiwa miaka 40, kabla ya kufa aliacha masharti ya maziko na kaburi lake. Alisema “Nikifa na penda kaburi langu liwe la futi 12’ kina, upana 6’ futi, sementi kali zaidi na mawe manne makubwa kila upande. Juu ya jeneza langu kuwekwe jiwe kubwa (slab) na maandishi haya yaandikwe, “Mahali pa kaburi hili pamenunuliwa milele na milele. Kaburi hili lisifunguliwe na yeyote yule daima.”

  • Baada ya miaka, mti ukamea juu ya lile kaburi, mizizi ya ule mti ikapasua lile kaburi na kuacha lile kaburi wazi.
  • Mizizi ya uzima likapasua miamba.
  • Walinda kaburi ya Yesu Kristo walikuwa bure, jiwe la mlango wa kaburi lilivingirishwa mbali.
  • Nguvu za kufufuka na uzima haziwezi kuzuiliwa.

Kwa sababu upendo wake kwetu unazo nguvu zaidi ya kaburi.

  • Yesu alienda kaburini kwa ajili yetu. Upendo wake ndio ulimweka hapo msalabani na kumweka mle kaburini.
  • Upendo uliomweka kaburini ndio upendo ule ule ulimfufua kutoka kwa wafu.
  • Alitupenda kiasi ya kutotuacha!!

Kwa sababu kazi ya ukombozi imemalizika.

  • Yesu Kristo alifufuka kwa wafu kwa maana alikamilisha kazi iliyomleta duniani.
  • Sasa hakuna kazi imesalia juu ya wokovu na uzima wetu, “yote yamalizwa.”

IKIWA MAUTI HAINGEWEZA KUMSHIKA YESU KRISTO BASI HAKUNA CHOCHOTE KINAWEZA KUMSHIKA.

  • Mauti ndio adui mkuu wa uzima. Hakuna kitu ambacho ni kibaya kama mauti.
  • Lakini Yesu Kristo aliyashinda mauti, akafufuka!!
  • Leo hii, sisi twamfuata Yesu Kristo aliyefufuka kwa wafu!! Alishinda mauti kwa ajili yetu.
  • Sasa hakuna chochote hata hekima ya dunia hii haiwezi kumzuia Yesu Kristo.
  1. Kumkataa Yesu hakuwezi (atheism). Waliposhindwa Yesu bado alikuwa Bwana.
  2. Ubuntu (utu) (humanism) walitafuta kumwinua mwanadamu na hekima yake juu ya ufahamu wa Mungu-ufalme wa Mungu wetu hauna mwisho.
  3. Ukomunisti (communism) ulijaribu kupinga Ukristo katika muunngano wa ulunzi (soviet socialist) lakini mwaka wa 1987 communism ilikwisha, sasa Injili ya Yesu Kristo yaubiriwa kote kote katika nchi zote.

KWA SABABU KIFO NA MAUTI HAZINGEWEZA KUMSHINDA YESU KRISTO SASA HAKUNA NGUVU AMBAZO ZINAWEZA KUTEGA KILICHO CHAKE YESU.

  • Sasa Mungu hawezi kuacha chochote kilicho chake kuzuiliwa na shetani.
  1. Pingu vya tabia haviwezi kuzuia.
    • Kwa sababu ya Yesu Kristo tabia na mazoea yako ya dhambi haziwezi kutushinda.
    • Damu na nguvu za Yesu Kristo zina uwezo wa kuvunja kila dhambi na mazoea yote ya dhambi juu yetu.
    • Yesu kwa kufufuka kwake amevunja kila laana, mateso na pingu za dhambi na nguvu zake.
  2. Pingu za kukzimu haziwezi.
  • Mlango wa kuzimu umeshindwa kabisa.
  • Tumewekwa huru juu ya shetani na pepo zake zote. Tumeponywa kwa nguvu zake.
  1. Pingu za dhiki zimevunjwa.
  • Kaburi ni wazi, sasa hatuwezi kuishi tena katika kaburi ya dhiki ya maisha haya.
  • Leo siku mpya ya kufunguliwa kutoka kwa dhiki na dhoruba za maisha.
  1. Pingu za mauti haziwezi kutuzuia.
  • Yesu Kristo amefufuka kwa wafu, pia sisi tulio wake tumefunguliwa.
  • Sasa hatuogopi mauti, twangojea kupokelewa na Bwana katika uzima wake.

MWISHO

  • Haikuwezekana mauti kumshika Yesu Kristo.
  • Haiwezekani mauti kutushika kaburini maana twaingia mara moja katika uzima wake.
  • Haiwezekani kufungwa na dhambi na tabia za dhambi ya zamani.
  • Haiwezekani kuishi katika dhiki na hofu-tumewekwa huru.
  • Leo ni wakati wako kuokoka toka kwa kaburi ya dhambi na kuwekwa huru daima na milele.
  • Yesu Kristo yupo leo kwa ukombozi wako-Amen.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago