SOMO: 2 MAMBO YA NYAKATI 12:1-12
Mwanaye mfalme Suleimani, Rehoboamu pamoja na nafasi nyingi alizokuwa nazo, hakuukaza moyo wake amtafute BWANA. Je, tutafanyaje kukaza mioyo yetu kumtafuta BWANA, je kuna manufaa gani kukaza moyo wako? Hebu tuone:-
FAIDA ALIYOKUWA NAYO REHOBOAMU
Babu yake alikuwa Daudi.
Daudi alikuwa mwandishi wa Zaburi, mwimbaji mkuu wa Israeli.
- Aliandika Zaburi 73, zaburi za ibada na sifa kaa Mungu.
Daudi alikuwa jemedari Howard, alitoa Israeli kutoka nchi ya tatu (third world) mpaka Taifa ya kwanza (first world).
- Daudi alishinda vita vyote kutoka Misri mpaka Mesopotamia.
- Daudi alileta ustawi na maendeleo kwa Israeli kiasi amani na uhuru zikadumu kwa miaka 40.
Daudi alikuwa mfalme aliyempenda Mungu zaidi kupitia kaa Daudi, Masihi Yesu Kristo alizaliwa.
- Rehoboamu alikuwa mwaka mmoja alipokufa Daudi, lakini aliyakuta matendo makuu ya mfalme Daudi.
Babaye alikuwa Suleimani.
Mfalme Suleimani alikuwa na ndoto mbili kutoka kwa Mungu.
- Alijenga hekalu na kutumika mbele ya uwepo wa Mungu.
- Suleimani alikuwa mwerevu zaidi duniani isipokuwa Yesu Kristo.
- Suleimani aliandika vitabu vitatu Mithali, Mhubiri, na Wimbo ulio bora.
- Kwa kusoma Mithali Rehoboamu angekuwa mwerevu zaidi duniani Kote.
- Suleimani alitawala kwa amani Israeli, aliogofya juu ya adui zake. Alikuwa tajiri zaidi, mwenye nguvu zaidi juu ya wafalme wote wa dunia yote.
- Suleimani alikuwa miaka 28 alipozaliwa Rehoboamu, hivyo Rehoboamu aliona yote ya mfalme Suleimani kwa miaka 41 kabla hajawa mfalme.
UPUNGUFU WA REHOBOAMU
Mama yake alikuwa Naama Mwamoni.
- Waamoni walikuwa adui wakuu wa Israeli.
- Waamoni walizaliwa haramu na Lutu na binti yake.
- Waamoni ndio walimlipa Balaamu kuaalaani wana wa Israeli.
- Namna alikuwa na usemi mkuu na uongozi juu ya mwanaye Rehoboamu.
- Usifungwe nira moja na wanaoamini.
Si jambo la kushangaza Rehoboamu alikuwa ovyo sana kiasi Daudi hakumkataza Suleimani kumuoa Naama, Mwamoni.
- Lakini pengine ilikuwa ngumu kumkataza Suleimani kwa sababu ya mapenzi na umbo. Naama maanake ni ‘mrembo’ lakini urembo wa ngozi bila urembo wa rohoni ni bure kabisa!! Ni kama Pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe!!
Babaye Rehoboamu alikuwa amerudi nyuma kiroho.
- Biblia inasema Suleimani alipokuwa ameimarika sana na kuwa mzee, bibi wake waliokuwa aa kigeni walimsihi kuwajengea hekalu za miungu yao.
- Suleimani mtu wa hekima, sasa aliacha Mungu na kujitegemea.
- Maisha ya Suleimani yalichangia sana maisha ya wanawe pamoja na Rehoboamu.
DHAMBI KUU YA REHOBOAMU- HAKUUKAZA MOYO WAKE KUMTAFUTA MUNGU
Maovu ya Rehoboamu- 12:14.
“Naye akatenda yaliyo maovu kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute BWANA.”
- Rehoboamu hakufanya dhambi ambazo zimetajwa kwa wafalme wengine kama jinsi wizi, uasherati, mauaji, ibada ya sanamu.
- Lakini dhambi yake hakutengeneza moyo wake, hakuukaza moyo wake, moyo wake haukumpenda Mungu, alikosa kuomba, alikosa kutembea na Mungu wake.
- Rehoboamu hakufanya mabaya lakini alikosa kufanya yaliyo mema (sin of omission).
- Kwa njia gani Rehoboamu hakuukaza moyo wake amtafute Mungu?
- Hakuanza utawala kwa kumtafuta Mungu.
- Suleimani babaye Rehoboamu alianza Utawala wake kwa kuomba hekima.
- Katika mwanzo wa kila kitu, iwe ni ndoa, familia, biashara, shule, kaza moyo wako kumtafuta BWANA.
- Huyu kijana mfalme Rehoboamu alijua kwamba anahitaji ushauri lakini alitafuta watu wa rika yake, wala hakuukaza moyo wake amtafute BWANA.
- Rehoboamu alikuwa karibu na washauri wa baba yake, lakini alichagua vijana.
- Watu wanapokataa ushauri wa Mungu, wanaendea njia mbaya.
- Kwa sababu moyo wake Rehoboamu hukuwa haki mbele za Mungu, aliyaiga mabaya ya baba yake Suleimani.
- Rehoboamu aliongeza wake kama baba yake.
- Alijenga miradi mingi na kuwatoza watu wake ushuru kupita kiasi.
- Kazi ya miradi yake mingi ilitorosha moyo wake mbali na Mungu.
- Biashara zako si mbaya, lakini ikiwa biashara zako zitakutoa kwa Mungu basi- angalia Rehoboamu.
- Kwa sababu moyo wake hakuukaza amtafute BWANA, basi Rehoboamu angeliweza kustahimili majaribu.
- Alipoanza kustawi, Rehoboamu alipata kuwa na kiburi.
- Alipopata kiburi, Rehoboamu alimwacha Mungu na pia watu wa taifa Lake.
- Kwa sababu ya kumwacha Mungu, adui zake Misri walimvamia (Shishaki).
- Kuna watu, wakristo wengi kanisani wako kama jinsi Rehoboamu.
- Wanaingia kanisa, wanamuahidia Mungu kumfuata, lakini marafiki zao, party, club, kwa kukosa msimamo wanaanguka mara moja.
MAANAKE KUUKAZA MOYO KUMTAFUTA BWANA
- Kwanza, fahamu unahitaji Mungu.
- Imani kamilifu inafanya maombi na kushudia ukuu wa Mungu- Matendo 17:24-28.
- Pili, lilia nguvu za Mungu na usaidizi wake. Omba utakatifu kila saa.
- Nyenyekea mbele zake mwokozi.
- Pokea mpango wa Mungu kwa wokovu wa nafsi yako.
- Mshukuru Mungu kila wakati kwa ukuu wake juu ya maisha yako.
- Linda moyo wako, kuliko vyote ulindavyo.
MWISHO
- Je, moyo wangu nimeukaza umtafute Mungu?
- Rehoboamu hakuukaza moyo wake amtafute Mungu hata baada ya kuvamiwa na Shishaki mfalme wa Misri.
- Wengine wetu hata baada ya ajali, ugonjwa au janga wanarudi kwa dhambi kwa maana hawakukaza mioyo yao kumtafuta BWANA.
- Usiwe kama Rehoboamu amua kumsimamia Yesu Kristo, choma kila daraja ya kurudi dhambini- UAMUZI NI WAKO LEO.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.