I SAMWELI 1:1-11

UTANGULIZI

Hanna ni picha nzuri ya mama na umama. Hana alitaka kuwa na watoto wake. Hana alimwomba Mungu mtoto na kumlea kwa kazi ya Mungu.

Elkana alikuwa kuhani hasiye mwaminifu kabisa, maana alikuwa na wake wawili.

Kuhani mkuu alikuwa Eli, naye alikuwa na wana wawili yaani; Hofni na Finehasi, wote wawili walikuwa waasi (I Samweli 2:12,17,29)

Imani ya Hana ilikuwa katika hali     ngumu sana, Penina alikuwa mke mwenza mwenye chuki na matusi ya kila siku. Penina alifikiri kwamba Hanna alikuwa tasa, lakini kumbe Mungu alimfunga tumbo. Kuna watu wanafikiri wewe ni tasa, kumbe wakati wako ujafika !! Samweli twafahamu lakini watoto wa Penina. Penina alifikiri matusi yake yatamfanya hana kukata tamaa, kumbe yalimfanya Hana kuomba kwa Imani. Watu wanao kuchukia wanafanya Baraka za Mungu kutimia katika maisha yako.

Hebu Tuone:-

I.  HATUA SABA ZA MAJIBU KWA MAOMBI.

Mahitaji makuu yanatuelekeza kwa maombi,

  1. a)Hana hakuwa na mtoto, “Mungu alikuwa amemfunga tumbo” (v.5)
  2. b)Hana alichukiwa sana na Penina, hivyo Penina humchokoza sana na kumsikitisha (v.6)
  3. c)Eli alikosa kumuelewa Hana-utakuwa mlevi mpaka lini? (v.14)

Mahitaji makuu yatufanya kuomba na kutoa sadaka.

  1. a)Kujitoa– Hana aliweka nadhiri (v.11)
  2. b)Hana alifunga Saumu (zaumu) (v.8)
  3. c)Hana alitoa wakati wake wa jamii kuomba Bwana (v.9)
  4. d)Hana aliomba sana na kulia sana (v.10)

Sadaka kuu inatufanya kuzidi katika maombi.

  1. A)Mwaka kwa mwaka—Jamii ya Elkana walienda maombi pale shilo (v.7)
  2. B)Kristo alisema omba nawe, utapewa, bisha nawe utafunguliwa, tafuta nawe utapata (Mathayo 7:7)

Imani kuu huzaliwa kutokana na mahitaji makuu, tamaa kuu na sadaka kuu (V.11)

  • Hana kweli aliomba
  • Hana alitoa nadhiri (Hesabu 6:1-21)

Imani kuu huleta majibu makuu.

  1. A)Eli alimwambia Hana- “Enenda kwa Amani, na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyo mwomba” (v.17)
  2. B)Mungu alimkumbuka Hana– Hana alishika mimba (V.19-20)

Majibu makuu lazima kufuatiliwa

  1. a)Jina la mtoto– Samweli—”Nime mwomba kwa Mungu”
  2. b)Hana alikaa nyumbani mpaka mtoto akue (V.22)
  3. c)Hana alimtoa huyo mtoto Samweli wakfu kwa Bwana (V.26-28)

Hana alifanya Ibada Kuu

  • Hana aliomba na kuimba nyimbo za sifa (2:1)
  • Hana alimwomba Bwana mtoto moja, Mungu alimpa watoto saba (2:5, Waefeso 3:20)
  • Mungu huwalinda watu wake (2:9)
  • Kwa nguvu zetu hakuna atakayeshinda.
  • Washindanao na Bwana watapondwa kabisa.

 

MWISHO

  • Imani lazima kuomba
  • Je, umeokoka? Leo ndio wakati wa kuokoka.
  • Je, penina wako yupo ?Ameshindwa.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

2 days ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

2 days ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

2 days ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

5 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago