Categories: Swahili Service

HATARI YA KUTOTAMBUA MAJIRA

SOMO: LUKA  19:28-44

Leo ni jumapili ya matawi ya mitende. Siku hii miaka 2000 iliyopita Yesu Kristo aliingia nji Ya Yerusalemu. Alipofika karibu aliuona Mji akaulilia akisema “laiti ungalijua hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako” .Kuna hatari kubwa sana mtu asipotambua majira na wakati ya kujiliwa na Mungu na kupoteza nafasi ya kuokoka (the tragedy of a lost opportunity)

Tunapotazama siku hii ya jumapili ya mitendo pengine twaona ushindi mkuu, Yesu Kristo amepanda juu ya punda, kuingia Yerusalemu kama mfalme wa Amani…. Pia umati na kusanyiko la watu halaiki wanamwimbia sifa Kristo na Mungu Baba.

Lakini juu ya mlima yesu kristo alisimama mbele yake mji mkubwa wa Yerusalemu ulisimama mbele ya macho yake. Kundi mzima lilikuwa katika shangwe na sifa na furaha huku wakiimba nyimbo zao – lakini Yesu Kristo alikuwa akilia!

Jumapili ya mitende (Palm Sunday) haikuwa siku ya ushindi, lakini siku ya hatari.

Yesu Kristo alikuwa akiwaambia watu wa Yerusalemu, mji uliombarikiwa sana”laiti leo kama ungalijua yaletayo Amani, lakini sasa yamefichwa machoni pako”

Yerusalemu na watu wake walikuwa katika hatari ya kutotambua siku na majira ya kujiliwa kwao.

Hebu tuone katika neno hii:-

I.  YESU KRISTO HATAZAMI MAMBO JINSI TUNAVYO YATAZAMA.

  1. Wanafunzi wa Yesu Kristo waliona urembo wa hekalu na jinsi mawe yake yalipendeza macho sana.
  • Lakini Yesu aliona hekalu kuwa pango la wezi!
  • Wakuu wa dini waliona kundi kubwa la watu wakasema hawa ni wenye dhambi lakini Yesu Kristo aliwaona hawa watu kuwa wagonjwa wanaohitaji tabibu na kondoo wanaohitaji mchungaji.
  • Wanafunzi wa Kristo walipendezwa sana na mji wa Yerusalemu lakini Kristo alioona mji unaoenda kuangamizwa na adui (Lk.19:43-44)
  1. Kwanini Yerusalemu kuhukumiwa?
  • Si kwa sababu haikuwa na elimu – maana wasomi wakuu waliishi Yerusalemu
  • Si kwa sababu ya dhambi kuu zaidi, kwa maana miji mingine ya Israeli ilikuwa na dhambi pia.
  • Lakini Yerusamelu ilipokea hukumu kwa sababu hawakutambua majira ya kujiliwa kwao
  • Yerusalemu ilipoteza nafasi yake kuokoka
  • Leo Yesu Kristo analilia maisha ya wengi wasio tambua majira ya kujiliwa kwao!
  1. Hakuna mji duniani kote ulipata kibali cha Mungu kama jinsi mji wa Yerusalemu
  2. Yesu Kristo alifundisha zaidi pale Yerusalemu
  3. Yesu aliwaponya wengi zaidi pale Yerusalemu
  4. Yesu Kristo aliwafufua wafu Yerusalemu
  5. Yesu Kristo alikuja kwa walio wake Yerusalemu lakini walimkataa!!
  6. Nafasi waliopata Yerusalemu haikuwa moja tu
  • Kristo alitumika katika Yerusalemu miaka 3 1/2
  • Aliwaponya, aliwafundisha, mlango wa kibali cha Mungu kwao ulikuwa wazi, lakini…
  1. Na sisi pia tumepata nafasi na fursa kubwa zaidi
  • Hakuna kizazi kimesikia injili kama kizazi hiki chetu
  • Tumesikia neno, kwa kuhubiriwa, nyimbo, TV, radio, magazeti, wahubiri wakuu.
  • Kama Yerusamelu ya zamani tumekuwa na siku ya kujiliwa, lakini si wengi wameokoka.
  • Wengi kama jinsi mafarisayo wameshika dini zao, mavazi yao, injili zao – walikataa kuokoka. (Mathayo 5:20)
  • Wanadamu hawajabandilika tangu wakati wa Yesu Kristo – bado! Wokovu ungali mbali na wengi makanisani

II.  Wengi pale yerusalemu walikubali kuongozwa na watu waliopotea njia (Yohana 7:40-53)

  1. Babala ya kusikia injili ya Kristo, wengi walichangua kusikiliza viongozi wao.
  2. Leo hii ikiwa wanasayanzi walikataa neno la Biblia – watu wanawafuata.
  • Wengine wanawasikiza wanasiasa na waalimu kuliko kusikiza wachungaji wao.
  1. Wengi wanapotea kwa kutotambua siku ya majira ya kujiliwa kwao – Yesu anawalilia kama jinsi alivyofanya Yerusalemu siku hio.

III. KWA WATU WA YERUSALEMU, KUKOSA MAJIRA YAKUJILIWA KWAO WALIPATA HUKUMU YA MUNGU

  • Jeshi la Roma lilikuja Yerusalemu mwaka wa 70A.D wakaiharibu Yerusalemu na kuvunja hekalu la Mungu tangu leo.
  • Lakini Mungu aliwapa Yerusalemu miaka 35 ya neema, lakini walikataa sauti yake!
  1. Pale msalabani Yesu aliwaombea “Baba wasamehe hawajui walitendalo”
  • Siku ya Pentecoste, Petro na Mtume waliwaonya lakini hawakusikiliza.
  1. Hakuna mwanadamu anayejua majira yake ya kujiliwa na Mungu itakwisha lini!!
  • Kwa jinsi hii, tunahitaji kuchukua nafasi ya kujiliwa kwetu. (II Petro 3:9)
  • Yesu Kristo mwenyewe ametuonya (Yohana 12:13) “basi Yesu akawaambia, nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo…”
  • Nafasi ya kuokoka ni leo, maana jana imepita na kesho huenda haitakuwako.
  • Leo ndio wakati unaokubalika (II Wakorintho 6:2) “sasa ndio siku ya wokovu”
  • Waebrania 3:7-8, tukisikia, tusifanye mioyo yetu migumu.

MWISHO

  • Ujumbe wa jumapili ya mitende (Palm Sunday) ni ujumbe wa Amani
  • Kristo alisema “laiti leo ungalijua, yapasayo Amani”
  • Amani ya Mungu, Amani na Mungu, Amani ndani yetu, Amani duniani, Amani kwa watu wote.
  • Kristo alikuja lakini walimkataa, Bwana wa Amani
  • Wewe leo usimkatae na kupoteza siku ya majira ya kujiliwa kwako. Mpokee Kristo leo hii – Amani.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

View Comments

  • Please; allow me to thank for this voice of HOLLY SPIRIT, that I have learned from this message. Be blessed.
    Charles Mwaseba.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago