HEZEKIA AKALIA SANA

II WAFALME 20: 1-11

UTANGULIZI

Katika Biblia watu wengi walilia, nayo mbingu   ikapanguza machozi yao.

  • Yohana 20:11-15, Mariamu alilia na kukosa tumaini, Yesu Kristo alipokuja akasema, unanitafuta mimi, kwa nini unalia? Ninaomba wewe ukapate kuona kinacho kufanya ulie, ni mtoto? Ni kazi? Ni mume? Mi mke? Ni njia, Mungu akutane nawe sasa.
  • Hajiri alilia (Mwanzo 21;160 mtoto Ishimaeli alikuwa anakufa kiu—Mungu alifungua macho yake Hajiri akaona chemchemi ya maji. Ninaomba Mungu akafungue macho yako uone chemchemi yako.
  • Esau alilia kwa kupoteza urithi wake (Mwanzo 27:38)
  • I Samweli 1:9-10 – Hanna alilia maana alikuwa tasa – Mungu alifungua tumbo. Bwana akufungulie mimba ukapate watoto.
  • II Samweli 15:30, mfalme Daudi alilia maana alinyanganywa ufalme wake – je, kuna mtu anataka kukunyanganya mke hau mume?     Mungu atakupingania. (II Samweli 18:9-10) kile kinabeba adui yako kitamwacha akininginia  hewani!
  • Zaburi 137:1 – wana wa Israeli walilia kwasabau ya utumwa wao, walipokumbuka zayuni na mema ya siku za kale. Je, unalilia mema ya   jana? Mungu atakurejesha.
  • Nehemia 5:1-5 – watu walilia sababu ya deni zao. Lakini deni zao zilifutwa (5:12)
  • Ufunuo 5:3-4, Yohana alilia sana maanake hakukupatikana mtu mwenye uwezo wa kukifungua kitabu cha unabii– je, unalia maana hakuna anaye kufungulia kitabu cha kufaulu?
  • Usilie kwa maana Yesu Kristo, simba wa Yuda ameshinda vita
  • Hezekia alitawala vyema sana, lakini amepokea habari mbaya katika ugonjwa wake, atakufa wala hataishi. Je unao ugonjwa wa mauti, Mungu alimpa Hezekia miaka 15 zaidi , lakini kwako Mungu anakuongezea 51 miaka. Hebu tuone:-

I.  TANGAZO LA GHAFLA (II WAFLAME 20:1).

“Tengeneza mambo ya nyumba yako, maana utakufa, wala hutapona”.

  • Hezekia alikuwa mfalme kijana tu, alikuwa mfalme mwema kuliko wote Israeli na Yuda.
  • Lakini ufanisi na kufaulu si kinga ya kifo.
  • Wengi waliofanya mengi na mema kwa watu waliishi maisha mafupi sana. Alexander, Kristo, Tom Mboya, J.M e.t.c.
  • Cha muhimu sana ni kutengeneza mambo ya mioyo yetu na nyumba zetu kabla mauti .Mauti yanaweza kuja upesi sana kama jinsi Hezekia.
  • Nyumba yake ilikuwa nyumba ya ufalme wake (Yuda).
  • Hezekia hakuwa na mwana bado, maisha si kuishi na kufa, lakini ni pamoja na kuwajibika na waajibu wetu juu ya wale watakaorithi baadaye.
  • Watu wanakufa lakini, maisha na dunia inaendela.

II.  MAOMBI YA DHATI (20:2-3)

  • Hezekia alikuwa anatawala miaka 15. wakati wa habari hizi mbaya, Hezekia alikuwa na miaka 40.
  • Hezekia alipopata habari za kifo, hakuwa tayari kufa.
  • Hezekia alijigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana – Hezekia hakutumainia usaidizi kutoka kwa mwanadamu.
  • Hezekia aliomba kwa jna la Bwana Mungu wake. “Bwana unikumbuke sasa. Jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na moyo mkamilifu na kutenda yaliyo mema mbele ya macho yako.”
  • Maombi ya Hezekia yaonyesha uhusiano wa binafsi na wa karibu sana na Mungu.
  • Na wewe, uhusiano na ushirika wako na Mungu huko vipi?
  • Hezekia alikuwa na uhusiano (Relationship) na ushirika (Fellowship) na Bwana Mungu.

 

III.  JIBU KWA MAOMBI (20:5-6)

  • Kabla Isaya hajatoka mjini Yerusalemu, jibu lilitoka mbinguni. (Isaya 65:24)
  • Hezekia aliponywa na kuongezewa miaka 15 kwa maisha yake.
  • Yuda na miji yake italindwa na Bwana, kwa ajili ya Bwana mwenyewe wa kwa ajili ya Daudi mtumishi wa Bwana.

IV.  MIAKA 15 YA TAABU NA UJINGA.

  • Shida nyingi zilipatikana wakati wa miaka 15 ya kuongezea Hezekia.
  • Ingekuwa bora kama Hezekia angekufa akiwa miaka 40, kuliko miaka 55, kwa maana katika mwaka wa kwanza wa hio nyongeza, Hezekia aliwapokea wapelelezi kutoka babeli.
  • Hezekia aliwaonyesha hawa wapelelezi mali yake yote na akiba ya dhahabu ya nyumba ya Mungu.
  • Baada ya miaka mitatu ya kupona, Hezekia aliamzaa mwana kwa jina Manase kupitia kwa mwanamke kwa jina HEFZIBA maana yake “furaha yangu hiko ndani yake”. Furaha ya    Hezekia ilikuwa ndani ya mke wake kuliko ndani ya Bwana.
  • Huyo mwana, Manase aliyaaribu yote, Hezekia aliyafanya pale Yuda.
  • Manase aliwarudishwa watu wa Yuda kwa ibada za shetani na sanamu.
  • Manase alijenga madhabahu ya shetani katika hekalu Bwana.
  • Manase aliwaendea wachawi na warogi, akamwaga damu isio na hatia (II Wafalme 21:1-16)
  • Kama Hezekia angalikufa kwa ugonjwa wake Manase angezaliwa!
  • Huenda maisha mafupi hupunguza maovu.

 

MWISHO

  • Je, utamlilia Bwana kwa hali yako?ninaomba sisi tuwe watu wa kulilia Bwana kwa maombi.
  • Mungu anajibu maombi kulingana na uhusiano na ushirika tulionayo na yeye.
  • Mungu anajibu Maombi.

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

View Comments

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago