HEZEKIA – MFALME WA UFUFUO

II MAMBO YA NYAKATI 29:1-36

UTANGULIZI

Ufufuo huwezi kuja kanisani mpaka viongozi wa kanisa kufufuliwa kwanza. Kanisa ni kama vile samaki, samaki anaanza kuoza kwa kichwa chake. Maitaji kuu ya kanisa hii la FBC ni ufufuo kutoka moyo. Pesa ni ya maana sana, lakini kwanza tunahitaji ufufuo wa watu walio kwa mioyo yao wamejitoa kwa ushuhuda wao kwa Kristo Bwana.

Mfalme Ahazi aliharibu Yuda na Israeli kwa vita. Alifunga nyumba ya Mungu (Hekalu). Uchumi wa Yuda ulikufa, jeshi lake liliangamia vitani na hivyo hapakuwa na uongozi Yuda    miaka yote ya mfalme Ahazi. Lakini Ahazi   alipoendelea kuangamiza maisha yake na     maisha ya Yuda, Mungu alikuwa anaandaa kiongozi, mwana wake Ahazi – yaani Hezikia. Hezekia alikuwa wa baba mbaya zaidi (Ahazi), lakini pamoja na baba mbaya Hezekia alikuwa na   mama yake Abiya, binti yake Zekaria.  Unakumbuka Zekaria kuhani alimsaidia sana     mfalme Uzzia na Zekaria alifanya kazi pamoja na Isaya nabii. Haijalishi, umbaya wa jamii   ulikozaliwa, uamuzi wako na nguvu za Yesu Kristo zinaweza kuvunja ngome za uovu wa jamii. Leo twaona jinsi ufufuo wa Hezekia ulivyo bandilisha Yuda. Lakini ufufuo unaanza kwa viongozi wa kiroho. Hebu tuone jinsi ufufuo unaanza na jinsi ufufuo unadumu:-

 

I.  MWITO WA KUJITENGE (29;3-7) UTAKASO.

  • Huu ni mwito wa utakaso wa binafsi na usafi wa nia.

 

  • Hezekia kwanza aliona umuhimu wa kujitakasa nafsi yake mwenyewe.
  • Hezekia pia aliona sababu ya viongozi wote kujitakasa.
  • Hakuna chama hau kasina inayoweza kuwa bora na kuinuka juu zaidi kuliko viongozi wake.
  • Viongozi wanaongoza, Hezekia alichukua jukumu ya kuongozi wa ufufuo katika Yuda.
  • Hezekia angeanza na maswala ya kujenga uchumi na siasa, lakini kwanza maswala ya kiroho.
  • Hezekia kwanza aliwaita watu kumrudia Mungu wao, baadaye Hezekia atajenga uchumi, jeshi na siasa za inchi yake – lakini kwanza – kutengeza njia ya Mungu wa Israeli.
  • Hezekia kwanza, alifungua milango ya hekalu la Bwana, pili aliwaomba makuhani na walawi kujitakasa
  • Hezekia aliwaimiza kujitenga na dhambi kwa:-
  1. Tubuni dhambi zenu – mkajitakase nafsi zenu.
  • Dhambi inatutenga na ufufuo (V.5)
  1. Tubuni dhambi zenu na dhambi za baba zenu.
  • Hezekia aliweka lawama juu ya uongozi wa kale. Viongozi waendavyo ndivyo inchi yote (V.6)
  1. Tubuni dhambi ya kukosa kuomba. (V.7)
  • Walifunga milango ya nyumba ya Mungu.
  • Walizima taa, hawakuifukiza uvumba, hawakumtolea Mungu sadaka.
  • Viongozi kama ufufuo utaanza hapa kanisani, ni lazima kwanza sisi, katika moyo wa kila moja.

 

II.  MWITO WA KUJISALIMISHA KWA MUNGU (29:20-28)

  • Hezekia alitoa ratiba ya kutoa sadaka kwa madhabahu ya Bwana.
  • Sifa na ibada ilifanyika kwa wote (V.28)
  • Ufufuo unaenda pamoja na sifa na ibada (23-28)
  • Waimbaji na wacheza vyombo husaidia mahali pakubwa katika ufufuo.
  • Cha kwanza kuanguka katika kanisa inayokufa ni sifa na ibada.
  • Huwezi kuwaongoza wengine kusifu na kuabudu ikiwa wewe mwenyewe hauabudu!
  • Sifa ni kitendo cha vinywa vyetu, lakini ibada ni kitendo cha moyo wote. (Warumi 12:1)

 

III.  MWITO WA KUTOA SADAKA       (29:31-36)

  • Watu walileta sadaka zao na sadaka za shukrani
  • Watu wote wenye moyo wa ukarimu wakaleta sadaka za kuteketezwa.
  • Mioyo iliyofufuliwa ni mioyo ya kutoa.

 

 

MWISHO

  • Changamoto kwetu leo ni kujitenga kwa kujitakasa nafsi zetu kwa Mungu.
  • Kujisalimisha nafsi zetu kwa Mungu na kujitoa sadaka, pamoja na kumtolea Mungu sadaka za shukrani kutoka kwa mioyo safi.
  • Ufufuo unaanza na wewe, lakini viongozi ni lazima kuongoza ufufuo.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago