Categories: Swahili Service

JE, WEWE HUKUJUA? HUKUSIKIA?

SOMO: ISAYA 40:28-31.

 

Nguvu za mwanadamu haziwezi kutosha tunapo pitia katika changamoto na magumu ya maisha. Haijalishi wewe ni nani na nguvu zako. Kila mmoja wetu atakutana na changamoto zinazotisha maisha yetu. Hatuwezi kwa nguvu zetu kushinda. Tunahitaji Mungu kila saa-Isaya 40:28-31.

Mungu alimuuliza Isaya nabii, “Je, wewe hukujua? Hukusikia? Mungu wa milele Bwana, muumba miisho ya dunia, hazimii wala hachoki. Akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao.” Katika somo letu hivi leo, Isaya anatupa neno la Mungu. Hii ni ahadi ya Bwana kutusaidia wakati wa udhaifu wetu.

Isaya anatueleza kwamba watu wale wamgojea Bwana watapewa nguvu mpya, watapanda juu kwa mabawa kama tai, watapiga mbio wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu wala hawatazimia.

Hebu waza picha ya mtu kumea mabawa kama tai na kupanda juu hewani kama tai. Wanakimbia bila kuchoka, watatembea bila kuzimia, wataruka kama tai, watapaa juu kwa nguvu za Mungu wao.

Wakati wale wasiomngojea Bwana wanaanguka kila mahali kama nzige au n’zi.

Haijalishi yale unapitia, lazima umngojee Bwana-mtumaini yeye kwa kupewa nguvu kushinda katika kila changamoto za maisha.

Je, ujasikia, wala kujua?

  • Bwana atataka sisi tupate kufahamu kwamba yeye Bwana hajapungukiwa na nguvu.
  • Huenda maombi yako ni hafifu lakini Bwana anasema, Je, wewe hukujua?
  • Hapa Bwana anasema unahitaji kujua au mpaka sasa ujajua kwamba Mungu atakusaidia.
  • Biblia inasema kwamba, Mungu ni wa milele. Mungu ndiye muumba dunia na vyote, yeye ni mwenye nguvu.
  • Huyu Mungu ndiye amekulinda katika mikosi na majaribu.
  • Usijaribu kudanganywa na shetani kufikiri kwamba ni bahati yako ilikukomboa mwaka wa 2024.
  • Tukumbuke yale Bwana alitutendea, ikiwa hakuna kitu amakutendea wewe binafsi hebu tazama jinsi amewatendea wenzako.
  • Hebu upate kuelewa kama jinsi aliwatendea wengine, atakutendea na wewe pia.
  • Nguvu za Mungu ziliwatendea wengine, hata hivyo Mungu atakutendea na wewe.
  • Je, haukujua? Je, haukusikia? Mungu wa milele ni mwenye nguvu zote atafanya yale ameahidi kutenda. Hebu tuone:-

LAZIMA TUJIFUNZE KUMTEGEMEA BWANA.

  • Je, wewe hukujua, hukusikia……tumtegemee yeye pekee?
  • Je, wewe hukujua? Hukusikia? Kwamba wakristo wengi, waliokoka, wana wa ufalme wa Mungu wanaishi maisha ya kushindwa bila shabaha na muongozo?
  • Je, wewe hukujua, hukusikia kwamba Mungu anataka tupate kumtegemea?
  • Je, wewe hukujua? Hukusikia? Wakristo wengi wanakataa kupokea ushauri, hawawezi kuambiwa neno lolote.
  • Je, wewe hukujua, hukusikia? Wakristo wengi wanapenda mahubiri ya mchungaji wao lakini hawataki kubadilisha tabia za uovu?
  • Je, wewe hukujua, hukusikia wakristo wengi wanapenda kuyategemea mawazo yao binafsi huku wakijiona wanajua zaidi kuliko Mungu.
  • Je, wewe hukujua, hukusikia, Mungu yuko na mpango wa ajabu kwa maisha yako, lakini kwa sababu ya kutotii neno wamejipata katika taabu nyingi zaidi-Mithali 3:5-6; 14:12.
  • Je, wewe hukujua, hukusikia, kama unapenda kuwa mshindi katika njia zako zote, basi husitegemee mawazo na akili zako, bali ukamtegemee Mungu.

BWANA ATAWAPA NGUVU MPYA.

  • Je, wewe hukujua, hukusikia kwamba Mungu huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo-Vs. 29.
  • Kuzimia ni wakati unaona dhambi imeanza kukuwinda, tamaa za mwili zimewaka upya katika maisha yako-Mungu atampa nguvu anayezimia.
  • Wasio na nguvu Bwana anawaongezea nguvu.
  • Mungu huwapa nguvu wanaozimia, huwaongezea nguvu wasiokuwa na uwezo.
  • Mwili wako unapokosa nguvu, kumbuka Mungu huwapa nguvu wanaozimia.
  • Mungu atakurudishia furaha ya wokovu wake.

NI LAZIMA KUJIFUNZA JINSI YA KUMNGOJEA BWANA.

  • Je, wewe haukujua, hukusikia kwamba ni lazima kumngojea Bwana?
  • Bwana anasema ikiwa tutamngojea, yeye Bwana atatupa nguvu mpya na kila jambo litakuwa shwari.
  • Mungu anasema kwa sasa huenda unateseka, unaumia, unakosa kazi, umekabwa na deni, watu wanakufitini, lakini ningojee.
  • Roho mtakatifu anasema ningojee msaada wako u karibu, Mungu anakujia.
  • Mungu yuko karibu zaidi kukukomboa kutoka utumwa.
  • Je, wewe haukujua, haukusikia kwamba mambo mapya Bwana yatendeka kwako?
  • Kumbuka jinsi Samsoni alipoteza kila kitu.
  • Alipoteza nywele, nguvu, macho, cheo, jamii, mke na heshima yake.
  • Alishuka kutoka mwamuzi wa Israeli mpaka mtumwa wa kusaga unga ya maadui zake, mwishowe alipomwomba Mungu, nguvu zake zilirejeshwa.
  • Maombi yake Samsoni yalikuwa “Bwana wangu, nimeanguka, siwezi kwa nguvu zangu kusimama, lakini ninakungojea wewe peke yako kunikomboa.”
  • Alizidi kuomba “Bwana ninakusihi wewe, Mungu wangu, nipe nguvu tena. Kwa kumngojea Mungu Samsoni alipata nguvu tena-Isaya 40:31.
  • Wakati macho yako yamejaa machozi mngojee Bwana.
  • Wanaomngojea Bwana ndio watapata nguvu mpya, ndio watapaa kama tai.

UNAPOMNGOJEA BWANA ATAKUFANYA UKAPAE NA MABAWA KAMA TAI.

  • Je, hukujua, hukusikia, wao wamngojeao Bwana watapewa mabawa na kupaa kama tai.
  • Je, hukujua, hukusikia? Wamngojeao Bwana watakimbia bila kuchoka, watatembea na kwenda kwa miguu wala hawatazimia-40:31.
  • Bwana anasema kama utamngojea yeye atafanya mabawa yako kama tai.
  • Mungu atakupandisha juu ya dhoruba na mawingu ya maisha yako.
  • Je, hukujua, hukusikia, kwamba tai hawezi kuruka ndani ya dhoruba lakini anapaa juu zaidi ya dhoruba na mawingu?
  • Je, hukujua, hukusikia, ikiwa unapenda kutembea bila kuzimia na kukimbia bila kuchoka ni lazima kwanza umjie Yesu Kristo kwa moyo wote.
  • Mwambie Yesu Kristo kwa nguvu zako umeshindwa, mwambie udhaifu wako, mwambie Yesu kwamba unatishika katika maisha yako, mwambie unaona giza mbele zako.
  • Mlilie Mwokozi wako, nilijifanya kama ni na nguvu lakini mimi ni mdhaifu sana, Bwana nisaidie, nipe nguvu zako.

MWISHO

  • Omba Bwana akurejeshee nia ya kupigana.
  • Mwambie Yesu Kristo jinsi unasikia kujiuzulu maisha, mwambie jinsi umekauka katika moyo wako.
  • Omba nguvu mpya sasa, omba ujazo mpya.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago