MFULULIZO: VITA VYA KIROHO
SOMO: ZAKARIA 13:6-10; DANIELI 2:22
Katika Zakaria 13:6 tunaona kwamba;
- Kunaye mtu aliyepata jeraha.
- Huyu mtu alijua aliyempa jeraha.
- Jeraha zake zilitoka mahali hakutarajia.
- Alijua kwamba majeraha yake yalitoka kwa mafiki zake.
Katika vita vya kiroho, kuna watu walio rafiki na wasio rafiki.
Rafiki asiye rafiki ni mtu ambaye anajifanya rafiki lakini matendo yake ni Matendo ya adui.
Mtu huyo anaweza kuwa baba, mama, ndugu au watu wa karibu sana kwako.
Mtu anaye kujeruhi sana ni lazima awe mtu wa karibu, kuweza kukujeruhi kiasi kikubwa.
Katika Danieli 2:22- “Yeye hufunua mambo ya mafumbo na siri, huyajua yaliyo gizani na nuru hukaa kwake.”
Kuna mambo ambayo ni siri ya ndani kabisa. Mambo haya ya siri yanajulikana na Mungu pekee.
Katika 1st Wafalme 14:1-3- mwana wa mfalme Yeroboamu alikuwa mgonjwa karibu kufa, dawa hazikufanya kazi kwake.
Mfalme Yeroboamu hakujua afanyeje.
Aliamua kumtuma mkewe kwa nabii wa Mungu Ahija.
Alitaka sana kujua kiini hasa cha ugonjwa wa mwanae.
- Kwa sababu mfalme Yeroboamu alikuwa na uhasama na nabii Ahija, ilimbidi kumtuma mkewe.
- Alimwambia mkewe aende akiwa amejifanya mtu mwingine.
- Lakini Mungu tayari alikuwa amenena na nabii Ahija na kumjulisha yote.
- Katika 1st Wafalme 14:4- mkewe Yeroboamu alipofika nyumbani, tayari mtoto alikuwa amekufa- 1st Wafalme 14:6-13.
- Kiini cha ugonjwa wa mwanaye Yeroboamu ilikuwa ni hukumu kwa nyumba yote ya mfalme Yeroboamu. Hebu tuone:-
UKWELI WA MAMBO
- Kuna mambo mbayo tunayaita shida.
- Shida ni vitu au hali ambayo yapatikana duniani kote na kwa watu wote.
- Shida haichagui kabila, rangi au cheo.
- Duniani kote kunazo shida na mauti, kujinyonga, ulevi, talaka, wizi.
- Kunayo pepo nyuma ya kila shida maishani.
- Hapa Afrika kuna shida ya umaskini, uchawi, ujinga, magonjwa, ufisadi, lakini shida ni ya ulimwengu.
- Shida na maafa haziheshimu mtu yeyote.
- Shida zinakuja bila mwaliko.
- Hivyo dunia yote imejaa wanaume/wanawake wanao jaribu kutatua shida zao.
- Nyuma ya kila shida na matatizo, kunaye roho mchafu.
- Wakati mwingi tunatumia kupigana na watu lakini tunahitaji kupigana na roho mchafu.
- Yesu Kristo alimkemea Petro- “Rudi yangu shetani.”
- Kuna sauti zinazo nena na watu kutoka kwa shetani.
- Kuna watu wanakimbia ovyo kwa sababu wanasikia sauti ya mtu na amri.
- Kila mtu wa Mungu wakati mmoja au mwingine atapata njama za watu waovu.
- Kama jinsi Yusufu na ndugu zake.
- Kama jinsi Danieli katika nchi ya Babeli.
- Kama jinsi Shadraka, Meshaka na Abedinego, moto, simba na gereza zinatungojea.
- Mateso ya mwenye haki ni mengi. Lakini Bwana atawashinda wote wanao kupangia njama.
- Vita vya kiroho ni vya aina tatu:-
- Hila na mishale ya adui (darts).
- Nafasi katika maisha yetu (foothold).
- Ngome (strongholds)- ngome zinaweza kukaa katika jamii, kizazi baada ya kizazi.
- Ibrahimu alidanganya mfalme Abimeleki baada ya miaka 40, Isaka alimdanganya Farao.
- Baada ya miaka 60 Yakobo alimdanganya Isaka, Labani alimdanganya Yakobo baada ya miaka 80.
- Baada ya miaka 120 Rubeni alilala na mke wa babaye.
- Miaka 140, Yuda alilala na mke wa mwanaye- ngome ya udanganyifu.
- Ngome zinaweza kuvunjwa mara moja- 2nd Wakorintho 10:3-5.
- Wazazi wako wanaweza kukupangia vita utakazo kuwa nazo maishani.
- Vita za kwenu nyumbani zinaweza kukwandama miaka yote.
- Wazazi wanaweza kuwaweka watoto wao katika vita vya maisha.
- Ikiwa kuna vita katika maisha yako, ni ishara tosha kwamba ndani yako kuna kitu cha kupiganiwa. Lazima kupigana vita mpaka uwe huru (Esau na Yakobo) Esau atakapopata nguvu atajikomboa.
- Suluhu ya kila shida imo katika shida yenyewe- Mwanzo 3:15. Kila shida iko na mbegu ya suluhu (nyoka ya shaba jangwani).
- Tuombe Mungu apate kutufichulia siri ya suluhisho ya shida zetu.
- Usiwe adui yako mwenyewe, pombe, sigara, umalaya- safari za pekee.
Kutoka 20:4- pete, nguo, nywele, tattoo.
- Wacha Mungu akufichulie siri ya shida zako.
- MAOMBI
- Kila adui wa wakati na nafasi yangu kufa sasa- katika jina la Yesu Kristo.
- Kila shida ndani yangu pokea ghadhabu ya Mungu na kidole cha Mungu katika jina la Yesu Kristo.
- Kila mishale ya rafiki asiye rafiki shindwa sasa katika jina la Yesu Kristo.
- Kila nguvu na mamlaka yanayoleta mauti kwangu shindwa katika jina la Yesu Kristo.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.