MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI
SOMO: 1 SAMWELI 21:10-15
Hapa tunaona mwimbaji wa Israeli aliyemuua Goliathi, mtu atakaye kuwa mfalme wa Israeli alijifanya mwendawazimu. Hapa twaona mtu aliyetupa mbao. Daudi alishuka chini kiasi. Je, kwa nini Daudi alishuka kiasi hiki?
Kila mtu chini ya jua anategemea mwenzake au kitu fulani kwa kuishi.
Hivyo kila mtu anayo system ya tegemea. Tunawategemea watu zaidi kuliko Mungu.
Mungu alituokoa ili tumtegemee Yeye kuliko kuwategemea watu au vitu. Mungu anapoona tunategemea watu au vitu, atatufundisha jinsi ya kumtegemea Yeye pekee.
Tunatazama kanuni ya kumtegemea Mungu katika maisha ya Daudi. Hebu tuone jinsi Mungu alimfunza Daudi jinsi ya kumtegemea. Jifunze kumtegemea:-
- DAUDI ALIJENGA TEGEMEO LAKE
- Katika ujana wake Daudi, twaona katika maisha yake mtu wa imani, mshujaa, utii, uadilifu na kujitoa kwa Mungu.
- Mungu kwa neema alimpa Daudi watu na vitu vya kutegemea. Hebu tuone:-
Daudi alitegemea cheo chake- 1 Sam. 18:13.
- Mfalme Sauli alimfanya Daudi akida juu ya askari 1000 (elfu) katika jeshi.
- Mfalme pia alimfanya mwimbaji katika ikulu lake.
- Cheo chake kilimfanya Daudi kuwa na tegemeo katika maisha.
- Daudi aliona cheo chake kuwa hatua nzuri kupata cheo cha ufalme wa Israeli.
Daudi alitegemea sifa zake- 1 Sam. 18:16.
- Watu wa Israeli walimpenda sana Daudi na kumheshimu sana.
- Sifa zake mbele ya wtu zikawa tegemeo kubwa kwa Daudi.
Daudi alitegemea kuungwa mkono na watu wote.
- Mungu aliweka watu kadha katika maisha ya Daudi katika siku hizo za shida.
Mikali alikuwa tegemeo kubwa- 1 Sam.18:20, 28.
- Daudi alipewa mke aliyempenda Daudi sana.
- Upendo na mapenzi ya Mikali kwa Daudi ilikuwa tegemeo kubwa.
- Wengi wetu tunategemea mapenzi ya mke au mume sana.
Yonathani mwana wa Sauli alimpenda sana Daudi- 1 Sam.18:1-4.
- Yonathani alikuwa rafiki mwaminifu zaidi kwa Daudi.
- Yonathani alikuwa macho na masikio ya Daudi katika ufalme wa Sauli.
- Yonathani alimpenda Daudi kuliko upendo wake kwa Sauli baba yake.
Nabii Samweli- 1 Sam. 16:13; 19:18.
- Nabii Samweli alikuwa tegemeo kubwa kwa Daudi.
- Nabii Samweli alimfundisha Daudi juu ya jinsi ya kutoa dhabihu, kutumika na kuabudu. Alikuwa tegemeo wakati wa ujana.
Daudi pia alitegemea busara yake mbele ya watu wote.
- Alikuwa mtu wa kuwaheshimu wote.
- Alikuwa na heshima zake mwenyewe, alikuwa mtu wa kiasi, sifa zake.
Tunahitaji kumshukuru Mungu kwa tegemeo aliyetupa kila mmoja.
- Tegemeo ya mme au mke.
- Tegemeo ya marafiki zetu.
- Tegemeo ya kanisa lako.
- Tegemeo la neno la Mungu (Biblia).
- Tegemeo la watu wa Mungu, ukipatikana na kitu tuko pamoja na wewe.
TEGEMEO YA DAUDI ILIVUNJWA MARA MOJA
Hatua za kuvunja tegemeo.
- Hata ingawa Daudi alikuwa na tegemeo kubwa, siku moja tegemeo lake lote lilivunjika!!
- Siku moja Daudi alikuwa juu ya dunia, sasa yuko chini mavumbini.
- Daudi akawa mtu wa kuwindwa na adui zake, akawa anawindwa na mauti na uaribifu- 1 Sam.20:3.
- Mungu mwenyewe alihusika katika kuvunja tegemeo za Daudi zote.
Daudi alipoteza cheo chake- 1 Sam.19:8-10.
- Akida mkuu wa Israeli na jeshi lake katika historia ya Israeli alishushwa cheo.
- Akida amekuwa mkimbizi duniani.
Daudi alipoteza sifa.
- Sasa Daudi ametolewa kutoka kwa mwangaza na jicho la watu wote.
Daudi alipoteza watu wake wote.
- Kila mtu aliyekuwa tegemeo kwa Daudi aliondolewa:-
- Mikali aliondolewa- 1 Sam. 19:11-17.
- Yonathani aliondolewa- 1 Sam. 20:41-42.
- Samweli aliondolewa- 1 Sam.20:1. Baadaye Daudi alikimbilia Samweli, lakini sasa lazima Samweli kuondolewa.
- Sifa na heshima za Daudi ziliondolewa- 1 Sam.21:10-15.
Sababu za kuvunja tegemeo za Daudi.
- Kwa nini Mungu alivunja tegemeo za Daudi?
- Kwa nini Mungu aliruhusu dhiki katika maisha ya Daudi?
- Mungu alifanya hivyo kwa Daudi ili Daudi ajifunze jinsi ya kumtegemea Mungu kuliko kutegemea watu na vitu.
- Watu wa Mungu wanahitaji kumtegemea Mungu pekee.
- Tulipokuwa watoto, tuliwategemea wazazi wetu. Tulipoenda shule, tukawategemea walimu na marafiki zetu.
- Tulipopata kazi, tulitegemea waajiri na pesa, mishahara.
- Tunapokuwa Wazee tunawategemea watoto au pesa za uzeeni na uekezaji wetu.
- Tegemeo zetu zinaweza kuchukua mahali pa Mungu ndani ya maisha yetu- Kumbukumbu 33:27; Isaiah 41:10.
- Tegemeo zetu zinaweza kuzuia kumwona Mungu na usaidizi wake.
- Tegemeo zetu ni za mda mfupi lakini Mungu ni tegemeo la milele- Waebrania 13:5; Mathayo 28:20.
- Mungu anavunja tegemeo zetu ili tupate kumtegemea Yeye pekee.
DAUDI ALIMFANYA MUNGU KUWA TEGEMEO LAKE LA PEKEE- Zaburi 34
- Daudi alipopoteza tegemeo zake zote ndipo alijifunza jinsi ya kumtegemea Mungu pekee- Zaburi 34.
Daudi alijifunza kutegemea sifa za Bwana- V. 1-3.
- Badala ya kuwategemea watu na mali, Daudi alianza kuntegemea Mungu pekee- Zaburi 86:10.
Daudi alijifunza kumtegemea Mungu kwa ulinzi na usalama wa maisha yake- V.4-7.
- Mungu ni ulinzi wa watu wake- Isaya 54:17.
Daudi alijifunza kutegemea utoshelevu wa Mungu- V.8-10.
- Alikula mikate katatifu kutoka kwa madhabahu ya Mungu- Zaburi 37:25.
Daudi alijifunza kutegemea ahadi za Mungu- V.9-17.
- Ahadi zake ni za milele- Zaburi 119:89.
Daudi alijifunza uwepo wake Mungu- V.18.
- Alimfanya Mungu kuwa rafiki wake wa karibu- Mithali 18:24.
Daudi alijifunza kutegemea fadhili na kudumishwa na Mungu pekee- V.19-22.
- Mungu pekee ndiye aliyedumisha watu wake na kuwahifadhi- Zaburi 61:2.
MWISHO
- Je, tegemeo lako ni nani?
- Mungu anavunja tegemeo zetu, watu na vitu ili tumtegemee kwa imani.
- Mungu ndiye udhabiti wetu- Zaburi 46.
- Leo, mpe Kristo moyo na maisha yako, kamtegemee Yeye pekee kwa wokovu na mahitaji yako yote.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.