SOMO: MATHAYO 1:8-25
Siku kuu ya Krismasi imefika kwetu tena. Krismasi ni siku ya kusherehekea tumaini letu katika Kristo.
Yesu Kristo alikuja duniani kutuletea mpango na wokovu kwa wote watakao weka imani yao ndani yake.
Jina YESU ni jina lililo juu ya majina yote maanake, “Yehovah ni Mwokozi.” Kristo maanake ni “Masihi” aliyepakwa mafuta.
Wafalme wa Israeli walipakwa mafuta kuwa wafalme wetu. Kristo ni Mwokozi, Mkombozi, Mfariji na rafiki wa karibu.
Jina la Yesu lina maana nyingi kwa watu wengi. Yesu Kristo ni mwalimu, hivyo Yeye ni kweli Kristo kama rafiki ni mfariji, yuko karibu nasi kuliko ndugu.
Leo naomba tujifunze juu ya moja ya majina ya Yesu Kristo. Jina hilo ni Emmanueli. Jina Imanueli ni jina alilopewa na malaika alipomjia YUSUFU na pia ni jina lililo tabiriwa na nabii Isaya- Isaya 7:14.
Isaya 7:14-“Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume naye atamwita jina lake Imanueli.”
Jina Imanueli maanake ni “Mungu pamoja nasi.”
Hii ni ahadi ya ajabu sana, ahadi hii inatuhusu sisi leo. Hivyo napenda kushiriki pamoja nanyi njia kadha. Yesu ni Mungu pamoja nasi leo.
MUNGU PAMOJA NASI- NJIA MUNGU ANAPOWAOKOA WENYE DHAMBI.
- Biblia inatueleza jinsi tulivyo wenye dhambi na jinsi tumepungukiwa na utukufu wa Mungu- Warumi 3:23.
- Mtume Paulo pia anatueleza jinsi mshahara aa dhambi ni mauti- Warumi 6:23.
- Ni dhambi iliyoleta mauti duniani.
- Bila msamaha wa dhambi kwa damu ya Yesu Kristo, wanadamu wataishia jehanamu milele.
- Kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti, ilipasa mtu atufie msalabani apate kulipa deni yetu ya dhambi.
- Dunia bila Kristo ni dunia bila mwongozo, ni dunia ambayo watu daima wanatafuta amani, furaha na amani.
- Bil Yesu Kristo tunakaa katika dunia bila furaha, tunapotea na kukaa katika hukumu katika dhamiri zetu.
- Bila Yesu Kristo tunaishi katika dunia kuvunjika roho, dunia ya kilio na ufukara.
- Yesu Kristo alipokuja hapa duniani alikuja na mishoni ya kuokoa dunia hii kutoka dhambini.
- Kristo alipokuja Bethlehemu, alikuwa anatazamia Kalvari, mahali pa kuondoa dhambi. Alizaliwa ili afe!!
- Kristo alikuja ili tupate tumaini mpya na hakikisho ya uzima wa milele.
- Yesu Kristo duniani alikuwa ni kipimo cha kutuonyesha dhambi zetu. Uzuri na ubora wa Yesu Kristo ulionyesha dhambi zetu.
- Wokovu ni kipawa cha Mungu kwetu lakini kipawa si kipawa mpaka tukipokee- Waefeso 2:8-9.
JINA IMANUELI- MUNGU PAMOJA NASI- INAFANYA MUNGU KUWA FARAJA YETU WAKATI WA DHIKI- Luka 4:18.
- Kuna wakati katika maisha tunayosema hayana maana kamwe.
- Katika huduma tunaita wakati huo wa kunyamaza- “Huduma ya uwepo.”
- Dhiki na simanzi huleta kiwango moja, kila mmoja wetu anafikia wakati wa kilio.
- Wanadamu bila Yesu Kristo hawana njia mwafaka kukabili kilio na dhiki ya maisha.
- Kuna kufunguliwa wale wako ndani ya Yesu Kristo wanapokea faraja, amani na tumaini.
- Uwepo wa Yesu unatupa raha, tumaini, furaha ambayo dunia hii haiwezi kutoa- Mathayo 11:28-30.
JINA IMANUELI- MUNGU PAMOJA NASI- INABAKI KUWA TEGEMEO KWA WATOTO WA MUNGU.
- Uwepo wa Mungu ndani ya maisha yetu inakuwa tegemeo, inatupa moyo na motisha.
- Wakati mwingine maisha yanajaa watu wasio na shukrani.
- Ni ngumu kuishi na watu wanao kuhukumu kila wakati.
- Lakini tunapotazama ahadi za Mungu inatupa kuvumilia.
IMANUELI- MUNGU PAMOJA NASI- MUNGU YUPO PAMOJA NASI WAKATI WA MAUTI.
- Mauti inaogopesha watu wote, lakini sisi tulio ndani ya Imanueli tunapata mwongozo mpya, amani na utulivu wa kutuongoza katika bonde la uvuli wa mauti- Ufunuo 21:2-4.
- Yesu Kristo alishinda mauti- Zaburi 23:4.
- Imanueli – Mungu pamoja nasi.
- Mungu ameyafanya mauti kuwa kivuli juu yetu- kivuli hakiumi.
- Lengo la Mwokozi Yesu Kristo ilikuwa ni kuokoa wenye dhambi- Luka 19:10.
MWISHO
- Imanueli ni Mungu pamoja nasi siku zote mpaka mwisho- Mathayo 28:20, (Immanence).
- Hitaji kuu ya mwanadamu ni kuokoka, ndiyo Mungu alimtuma Mwokozi- Wagalatia 4:4.
- Kama mahitaji yetu yangekuwa habari Mungu angemtuma mwalimu.
- Kama mahitaji yetu yangekuwa tekinolojia, Mungu angemtuma mwanasayansi.
- Kama mahitaji yetu yangekuwa dawa, Mungu angelituma daktari.
- Kama ni pesa- mwanauchumi (economist).
- Kama ni kutumbuiza- msanii.
- Kama jeshi na usalama- askari.
- Kama haki- hakimu.
- Kama sheria- mwanasiasa.
- Lakini hitaji letu kuu ni wokovu, hivyo Mungu alimtuma Mwokozi duniani- Wagalatia 4:4-5.
Je, umeokoka? Mjie Mwokozi wako leo.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.