Categories: Swahili Service

JINSI YA KUANGUSHA NGOME

MFULULIZO: JINSI YA KUFANYA VITA VYA KIROHO

SOMO: 2 WAKORINTHO 10:4-5; MATHAYO 11:12; MATENDO 7:54-60

 

Kila mmoja wetu ameitwa kuwa askari wa Yesu Kristo. Tunahitaji kupigana vita vizuri vya imani. Tunapigana na ngome za dhambi. Ngome ni mawazo, fikra, imani, Matendo na maneno. Tunaye mshindi hodari Yesu Kristo, hatuwezi kushindwa. Milango ya kuzimu haiwezi kutushinda. Leo tunajifunza jinsi ya kuangusha ngome. Hebu tuone:-

MTUME PAULO ALISEMA, “VITA VYETU”

Kila mkristo ni askari.

  • Je, ni kitu gani kinaonyesha kuwa mtu ni askari? (Uniform, nywele, maneno, sura, ujasiri).
  • Mungu anasema lazima sisi sote kuwa askari. Rais Thomas Jefferson alisema, “kila mwananchi lazima kuwa askari.”
  • Warumi na wagiriki wa zamani waliamini kila mwananchi kuwa askari.
  • Kuwa askari ni kuwa huru, kila nchi na taifa huru inaomba kila mwananchi kuwa askari!!
  • Paulo alisema, “ushiriki taabu pamoja nami kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna apigaye vita, ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari”- 2 Tim.2:3-4.
  • Tuko vitani katika falme mbili. Ufalme wa giza na ufalme wa nuru. Lazima kupigana vita nzuri na kupigana katika maombi.
  • Askari ndio wanapigana vitani, ndio wanaobeba silaha, ndio wanao hatarisha maisha yao kwa sababu ya mwito.
  • Kanisa sio demokrasia, lazima kutii amri, kutii ndio uhuru wa kila askari.

Adui hawezi kukuachilia kwa amani, lazima kupigana vita.

  • Paulo anatueleza shetani hawezi kutuachilia kuchukua watu wake kwa amani lazima kupigana.
  • Vita ndio njia pekee ya kushindana na ibilisi shetani.
  • Vita vyetu lazima kuwa vita vya mpango- Danieli 11:32.

MASHARTI YA ASKARI

Kujitoa

  • Askari wa Amerika kwa jina Bert Clende alikuwa askari hodari sana, alishinda vita vya Amerika na Philipino. Baadae akawa mhubiri hodari wa Yesu Kristo. Alipowaombea wavuta sigara kuokoka aliwaambia waombe hivi, “Mungu wangu ninaahidi sitavuta sigara tena, na ikiwa nitarudia kufuta sigara tafadhali niue mara moja!!”
  • Mtu akikataa kuomba maombi hayo, Bert alimpiga kofi mpaka kuokoka.
  • Mkristo asiyejitoa kwa Yesu Kristo ni kafiri.
  • Mtume Paulo alisema hivi juu ya kujitoa, Matendo 21:13- “Ndipo Paulo alipojibu, mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina Lake Bwana Yesu.”

Ujasiri

  • Je, askari wanakuwa na hofu kwenda vitani? Ndio, lakini wanakataa hofu ili kumtii jemedari wao na amri zake.
  • Ujasiri ni jambo linaloambukiza.
  • Tunapoona ujasiri wa watu wengine, tunavutiwa kusonga mbele.
  • Ujasiri ni neema inapofanya kazi, Roho wa Mungu anatuvuta kutoka kwa hofu zetu.

Nidhamu

  • Hatuwezi kuwa na jeshi bila nidhamu katika mwenendo, maombi, kusoma Biblia na kuhudhiria kanisa na kushuhudia Kristo.
  • Nidhamu ndio asili ya askari mwema.

KUANGUSHA NGOME

Je, ngome ni nini?

Paulo alitumia “Ngome” kumaanisha “Mahali pa nguvu.”

  • “Ngome” ni mahali ambapo uovu unakaa na kutawala, mahali ambapo ni ngumu kung’oa uovu.
  • Ngome ni imani na mafikira maovu yanayotupeleka njia mbaya.
  • Ngome ni hofu zetu, wasiwasi, hasira, mali, dhambi, uchungu, hisia, Matendo na maovu yetu.
  • Ngome ni chochote kile ambacho hakimpendezi Mungu katika maisha yetu.
  • Ngome ni mila zetu na mapokeo ya babu zetu, mambo yanaopigana na neno na ukweli wa Mungu.

Je, ngome zetu zinaweza kuwa nini?

Aina za ngome:-

  • Wengine wetu tunao watoto bado kuokoka, watoto ambao uhusiano wetu na wao ni mbaya, hiyo ni ngome.
  • Wengine wako na shida kubwa na pesa (financial stress), deni, ukosefu wa ajira, umaskini na kukosa ardhi ya kumiliki.
  • Wengine wanayo ngome ya kukosa afya, maumivu yamewasonga sana na magonjwa sugu.
  • Wengine wanao shida kubwa ya ndoa zao.
  • Wengine wanayo ngome ya upweke na msongamano wa mawazo.
  • Wengine ngome yao ni majaribu, ulevi, madawa ya kulevya, sigara, kulaani watu, kutosamehe watu, mafikra mabaya, uasherati na ukimwi.

Usipoteze vita vyako.

Tunaye Mwokozi anayetuokoa na ngome zote.

Yesu Kristo hajapoteza vita yoyote- Luka 10:19.

Usikufe moyo hata wakati hujapata ukombozi wa haraka- (Kutoka 23:30) utakapo pata nguvu, nyororo zote zitaanguka chini.

Jinsi ya kutupa nyororo za ngome zako.

  1. Kwanza, shinda dhambi iliyo kubwa zaidi ndani ya maisha yako (ulevi, uasherati, tabia mbaya, marafiki waovu, sinema ovu, wizi, uzembe).
  2. Pili, shinda hasira yako, tamaa mbaya, ulafi, uasi, shingo ngumu.
  3. Tatu, pigana na mafikira yako maovu- 2 Wakorintho 10:5.
  4. Ushindi ni wako katika Yesu Kristo- Mathayo 16:18.
  • Tembea katika nuru ya Yesu Kristo- 1 Yohana 4:4.

 

MWISHO

  • Silaha zetu ni kali kutuletea ushindi.
  • Kila askari mwema anayo alama ya vita mwilini (pengine jeraha, mguu moja, jicho moja).
  • Yesu Kristo anazo alama za askari mwema na hodari, alama ya kofia ya miiba kichwani, alama ya mkuki mbavuni zake, alama za misumari katika mikono na miguu.
  • Tutakaposimama mbele zake Kristo, atatutazama, atauliza, “Je, wapi alama zako?”Kama tutasema hakuna alama, Kristo atasema hivi, “je, hakukuwa na chochote cha kupigania?” Je, ni nani wa kuokoka leo?
  • Je, ni wangapi hivi leo wanao ngome, unataka ushindi dhidi yake?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

9 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

11 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

13 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago