Categories: Swahili Service

JINSI YA KUISHI NA WATU WAGUMU

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA DAUDI

SOMO: 1 SAMWELI 21:1-9; 1 SAMWELI 22:6, 23, ZABURI 52

 

Watu wagumu wako kila mahali. Watu wagumu wanaweza kuwa wewe au mimi. Je tutaishije na watu wagumu, je tufanye nini na watu hawa? Maisha ya Daudi ni kielelezo na funzo kubwa kwa kila mmoja wetu na jinsi ya kuishi na watu wagumu.

Katika 1 Sam. 21-22 kuna jumbe tatu za maana sana.

Daudi alikimbia mfalme Sauli, akajificha katika, mji wa Gathi.

  • Gathi ulikuwa mji wa yule Goliathi aliyeuawa na Daudi.
  • Daudi alipojulikana na watu wa Gathi, alijifanya mwenda wazimu-1 Sam. 21:10-15.
  • Daudi aliandika (Zaburi 34) wakati huu.
  • Petro anakiri (Zaburi 34) katika 1 Petro 3:8.

Kuna ujumbe wa jinsi Daudi alikimbia mfalme Sauli akajificha katika pango la Adulamu- 1 Sam. 22:1-2.

  • Watu wa kila aina walijiunga na Daudi, watu waliokuwa na dhiki, watu wa madeni, watu wote wenye uchungu mioyoni mwao.
  • Wazazi wake Daudi pia walimkimbilia Daudi.
  • Tunahitaji kuwatii wazazi na kuwatumikia- Kutoka 20:12; Kumbukumbu 5:16.

Kuna ujumbe juu ya jinsi mfalme Sauli aliwaua makuhani wa Mungu mle Nobu- 1 Sam. 21:1-9.

  • Mfalme Sauli aliwaua Ahimeleki Kuhani wa Makuhani 85, pia na wake zao watoto na wanyama wao.
  • Daudi aliandika kisa hiki katika (Zaburi 52).
  • Ni ujumbe huu tunaangazia hivi leo.
  • 1 Samweli 21:1-9. Hebu tuone:-

DAUDI NA KUHANI AHIMELEKI HUKO NOBU- 21:1-9

    • Basi Daudi katika kukimbia alifika mji wa NOBU.
    • Daudi alifika kwa Ahimeleki akiwa na udanganyifu mwingi sana.
    • Daudi alidanganya kuhani kwamba amefika huko akiwa ametumwa na Mfalme Sauli.
    • Daudi alidaganya kuhani kwamba amefika huko Nobu pamoja na vijana wengine.
    • Daudi aliomba chakula na silaha za vita.
    • Kuhani bila shaka alimpa Daudi mikate takatifu na pia ule upanga wa Goliathi.
    • Kisa hiki ni kweli kwa sababu Yesu Kristo alikizungumzia katika- Mathayo 12:3-4.
  • Yesu Kristo anasema haikuwa halali Daudi na waliokuwa naye kula ilie mikate kwa sababu.

SHIDA KUBWA-DAUDI ALIONEKANA NA DOEGI MTUMISHI WA MFALME SAULI- 21:7

  • Doegi alikuwa mchungaji mkuu wa mfalme Sauli.
  • Doegi alikuwa huko kwa kuhani mkuu (Ahimeleki) kwa shughuli za utakaso au kwa sababu ya nadhili fulani.
  • Doegi alimuona Daudi na yale alifanyiwa na kuhani Ahimeleki.
  • Shida kubwa ni kwamba Doegi alimsema Daudi kwa mfalme Sauli 1 Sam. 22:6-10.
  • Doegi alikuwa mtu wa Edomi (Edom) ni mzaliwa wa Esau, Ndugu yake Yakobo.
  • Mfalme Sauli hali amejaa ghadhabu na hasira, akiwa na mkuki mkononi anawatisha watumishi wake wote.
  • Doegi ndipo alisema yale aliyoyaona- 1 Sam. 22:9-10.
  • Mtu mwenye wivu ni mtu asiye salama, mtu mharibu, mtu muuaji- mfalme Sauli amekosa usalama wa binafsi.
  • Daudi aliandika- Zaburi 52:1-9 juu ya kisa hiki.
  • Mawazo ya Daudi kwa Doegi ni mengi.
  1. Doegi anajisifia uovu- Vs. 1.
  2. Ulimi wake unatunga madhara kama wembe mkali- V.2, V.4.
  3. Anapenda mabaya na uongo- V. 3.
  4. Hamtumaini Mungu, lakini mali – V.7.

WATU WAGUMU 

  • Watu wagumu wako kila mahali na kila jamii hata kanisani kuna aina (10) za watu wangumu. Wewe na mimi twaweza kuwa mmoja ya hawa watu.

Wajuaji – (The know-it-all)

  • Hawa ni watu wanao amini kwamba wanajua sana, wanajua yote.
  • Hawa wanajua zaidi kuliko watu wengine.
  • Hawa watu ni vigumu sana kupokea ushauri.
  • Watu hawa hawawezi kubali makosa yao lakini yao ni kuwalaumu wengine.

Mwenye kuingilia -(The Interrupter)

  • Huyu ni mtu hawezi kumpatia mtu mwengine ruhusa ya kuongea, huyu ni mtu asiyesikiza wengine wanapoongea.
  • Huyu ni mtu anayeingilia wengine wakiongea anapenda kukatisha mtu na kumpotezea wazo.

Mwenye kuwapuuza watu (The Ignorer)

  • Mtu huyu anachagua ni nani atakaye sikiza na kuonyesha wale wengine wote kuwa hawako, hawaonekani.

Mwenye kubore (The Bore)

  • Huyu naye anakufanya usikie kwamba unabore sana na kuwa unavyoongea ni upuzi.
  • Hawa ni watu unapoongea wanaingia shughuli zao na mawazo yao. Pengine wanaenda nje, wananema na simu au wanasoma kitu.
  • Hawa wanaona ni wao tu na mawazo yao yaliyo na maana, lakini kila mwingine anabore sana.

Wabinafsi (The prima Donna) 

  • Hawa wanaamini maisha ni juu yao pekee (everything is about them).
  • Kila kitu ni mawazo yao, mahitaji yao, maendeleo yao.
  • Hawa watu wanafanya kazi yao kwa bidii ili waweze kuwa maonyesho kwa kila mtu.

Wafanya kazi kufa na kupona (The work Martyr).

  • Huyu ni mtu anayefanya kazi bila kukoma na kongea juu ya kazi yake.
  • Chochote utendacho hakiwezi kuwafikia wakati wanaotumia kazini, nguvu na hekima wanaotumia katika miradi yao.
  • Hawa ni watu wanaofanya kazi wakitarajia pongezi kutoka kwa watu.

Mwenye kulalamika (The Whiners).

  • Hawa wanaona dunia hii hakuna haki (woe-is-me syndrome).
  • Hawa ni watu wanaolalamikia kila kitu katika maisha.
  • Hawana asante na shukrani kwa kitu chochote katika maisha.

Mwenye kinyume (The Negativity spreader).

  • Huyu ni mtu ambaye mawazo yake ni kinyume na kila wakati lazima kuongea na kuenda kinyume.
  • Hawa wanaona tu giza wala hawaoni nuru katika maisha yote.
  • Kwao kuwatendea mazuri ndio kutenda mbaya.
  • Hawa watakuonyesha jinsi mpango wako huwezi kufaulu.

Mwenye kutengeneza mvua (The Rainmaker).

  • Huyu naye hapendi sheria na utaratibu wa mambo- (No norms).
  • Kwa sababu yeye ndiye nyota (Superstar) kila mtu lazima kufanya kama yeye apendavyo kwa maana ya viwango vyake (Standards) ndizo bora Zaidi.

Mwenye kuvuka mipaka (The boundary crosser) 

  • Huyu naye anavuka mpaka na kuingilia wengine (Physically and emotionally).
  • Huyu atachukua vitu vyako bila ruhusa au kukwambia juu ya maisha yao zaidi kuliko unavyo dhani.
  • Hawa wote ni watu wagumu kuishi na kushiriki na wao.
  • Hali iliendelea kuwa mbaya zaidi-1 Sam. 22: 11-23.
  • Mfalme Sauli aliendelea kumshtaki Ahimeleki kuhani wa Mungu- 14-15.
  • Lakini pia unabii wa Mungu juu ya Ahimeleki na jamii yake ulitimia.
  • Ahimeleki alikuwa wa nyumba ya kuhani Eli-kuhani mkuu wa kale- 1 Sam.2:31-32.
  • Abiathari peke yake aliokoka mauti na kumkimbilia Daudi  lakini baadaye Abiathari aliuliwa mfalme Suleimani- 1 Wafalme 2:26-27.
  • Baadaye mfalme Sauli aliona haitoshi kuwaua makuhani (85) aliwaendea pia jamii zao na mali yao yote- 1 Sam. 22:19-23.
  • Hivyo Sauli ni mtu mgumu na Doegi pia mtu mgumu.

JINSI YA KUISHI NA WATU WAGUMU- 1 Sam. 22:20-23.

  • Tazama jinsi Daudi alifanya, Daudi alimfariji na kumpokea Abiathari.
  • Daudi hakuwachukua wanaume wote 400 na kuanza vita.
  • Daudi hakumshauri Abiathari kulipisha kisasi.
  • Daudi hakwenda koritni au kuandika kwa Facebook, Twitter.
  • Daudi alimpokea Abiathari na kumpokea mtoto yatima na kuonyesha neema ya Mungu.

MWISHO

  • Watu wagumu wataendelea kuwa sehemu ya maisha yako, wape neema- 1 Petro 3:8-9.

“Neno la mwisho ni hili, muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitivu, wanyenyekevu, watu wasiolipa mabaya kwa mabaya au laumu kwa laumu bali wenye kubariki. Kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi Baraka.”

  • Je unao watu wagumu katika maisha yako? Basi waonyeshe neema, upendo, unyenyekevu na huruma.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago