MFULULIZO: YUSUFU
SOMO: MWANZO 39:1-23 (20-23).
Maisha ya Yusufu ni moja wapo wa hadithi kuu katika Biblia. Maisha ya Yusufu ni kisa cha huzuni na utukufu, uchungu na kufaulu. Maisha ya Yusufu yanatupatia masomo kadhaa. Somo moja imeandikwa katika vifungu vya Mwanzo 39:20-23.
Katika kifungu hiki tunampata Yusufu katika hali mbaya. Kijana wa miaka 17, ameuzwa kama mtumwa katika nchi ya Misri. Mle Misri Yusufu amenunuliwa na mkuu wa jeshi la Misri, yaani Potifa.
Katika nyumba ya Potifa, Mungu amemfanikisha Yusufu na kumpandisha cheo kusimamia yoye ya nyumba ya Potifa.
Lakini, mke wa Potifa amempenda Yusufu kiasi kutafuta kufanya mapenzi naye.
Yusufu amekataa kufanya uasherati na mke wa Potofa, Yusufu ameikimbia dhambi; lakini nguo zake zimeachwa mikononi mwa mke wa Potifa-Mwanzao 39:7-13.
Kwa mara ya pili sasa vazi lake Yusufu limemweka katika taabu-Mwanzo 39:14-18; 37:3-4.
Bwana Potifa alipofika nyumbani, mke Potifa amemshitaki Yusufu kwamba alipanga kum’baka. Potifa mkuu wa jeshi la Misri mara moja alimtupa Yusufu gerezani ya mfalme.
Ni katika gereza hili Yusufu alijifundisha masomo mengi sana. Yusufu alijifunza mengi juu ya Mungu gerezani.
Leo tunajifunza masomo alijifunza Yusufu hapa gerezani ya mfalme.
Lakini si Yusufu pekee alipitia katika maisha gerezani.
Wengi wa watumishi wakuu wa Mungu walipitia gerezani, Samsoni, Danieli, Yeremia, Hosea, Yohana Mbatizaji, Yohana, Petro, Paulo na Sila.
Katika gereza Mungu aliwafunza hawa watumishi wake mambo makuu.
Kwa kweli, Mungu ametujulisha kwamba kama watoto wake tutapitia milimani, mabondeni na mitoni ya majaribu.
Katika yale yote, Mungu ameahidi kuwa pamoja na watu wake!!
Hebu tuone jinsi ya kustahimili katika gereza za maisha:-
GEREZA NI MAHALI PA MATESO-Vs. 20.
- Biblia inatufundisha kwamba Yusufu alifungwa gerezani.
- Yusufu alipoteza uhuru wake, kinyume na ndoto zake-Mwanzo 37.
- Gerezani palikuwa mahali pa dhiki kuu na shida.
- Sisi pia kuna wakati tunapo fikiri na kuhisi hali ya gereza-Ayubu 14:1; Mhubiri 2:23.
- Kila mtu anaogopa hali ya gereza, lakini sisi sote tunapitia hali hii.
- Hakuna mtu hatapitia hali ya shida na majaribu.
- Lakini Yusufu alijifunza kwamba mtu akiwa ndani ya Kristo yuko huru hata gerezani.
- Mtu aliye ndani ya Kristo yuko huru hata katikati ya kuta za gereza-Ayubu 23:10.
- Mfalme Daudi alijifunza Zaburi 23, alipopitia katika gereza yake.
GEREZA NI MAHALI PA KUSAULIKA-Vs. 20.
- Yusufu alipouzwa mtumwa na ndugu zake na alipofungwa gerezani, Yusufu aliona ndoto zake hazitatimia kamwe-Mwanzo 37:7-10.
- Aliona kama Mungu alimsahau, alijisikia pweke, ameshindwa na kuachwa na kila mtu.
- Gereza za maisha zinatufanya kusikia tumeachwa na Mungu na watu.
- Shetani anapata nafasi ya kutujaribu. “Je Mungu wako yuko wapi? Unaona ulimtumikia kwa uaminifu, sasa kwa nini huko hapa?”
- Lakini sivyo, Mungu yupo. Wengine wanaweza kukuacha lanini Bwana yu pamoja nawe-Luka 12:6-7; Waebrania 4:15.
- Tunapokuwa pweke, tunapoona kama Mungu ametuacha kumbuka Eliya-1st Wafalme 19:1-18.
- Mungu anajua mahali ulipo, anajua gereza yako, nyenyekea mbele zake.
GEREZA NI MAHALI PA FURSA-Vs. 21.
- Yusufu alijifunza kwamba uwepo wa Mungu, sababu za Mungu na nguvu za Mungu ni dhairi katika shida zetu.
- Mungu amekutana na watu wake katika mahali pa kujitoa, mahali pa madhabahu, mahali pa sadaka.
- Yusufu alijifunza kwamba tunakutana na Mungu katika majaribu yetu.
- Danieli alimwona Mungu katika tundu la simba.
- Waebrania watatu waliona mkono wa Mungu katika tanuri ya moto.
- Martha, Mariamu na Lazaro walielewa ufufuo katika mauti ya Lazaro.
- Mwanamke aliyetokwa na damu alijifunza Yesu anaponya kwa kupitia shida na kumaliza fedha zake zote kwa matibabu.
- Tunapopita katika majaribu na gereza za maisha, tunajifunza kwamba Mungu anao uwezo wa kudumisha watu wake-Warumi 8:28.
GEREZA NI MAHALI PA UTII-Vs. 22.
- Katika gereza, Yusufu alizidi kuwa mwaminifu, aliamua gereza ni mahali pa huduma.
- Mungu anafanya watu wake kumea mahali wamepandwa.
- Mungu yupo katika ushukani wakati wote-Zaburi 50:10-12; 115:1-3.
- Mtumikie Mungu popote ulipo.
- Mungu anatafuta uaminifu katika gereza za maisha-Mathayo 5:13-16.
GEREZA NI MAHALI PA USHINDI-Vs. 23.
- Yusufu alikaa gerezani kwa miaka mitatu.
- Lakini hata gerezani Mungu alimtumia.
- Yusufu alitoka gerezani mpaka ikulu la mfalme wa Misri, kwa siku moja!!
- Katika yote Yusufu alikuwa mwaminifu.
- Juu ya nyumba ya babaye.
- Juu ya nyumba ya Potifa.
- Juu ya gereza.
- Juu ya nchi na ufalme wa Misri.
- Tunapopitia katika gereza za maisha, Mungu anaendelea kutufundisha njia zake-Luka 16:10-13.
- Kwa hivyo, tusiasi juu ya gereza za maisha.
- Tunanyenyekea mbele za Mungu, anajua yote na ni juu ya yote katika maisha yako.
- Usinungunike juu ya njia za Bwana wako juu ya maisha yako.
MWISHO
- Je, we uko gerezani fulani katika maisha yako?
- Je, unaendelea kumea mahali Mungu alikupanda?
- Mungu na akusaidie kuelewa na misimu ya maisha yako.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.