MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI.
SOMO: WAAMUZI 6: 11-16
Moja ya vizuizi kubwa zaidi kwa maendeleo ya maisha si upinzani kutoka nje lakini vizuizi vya binafsi. Vizuizi ndani yetu ni pamoja na hofu, kukosa usalama wa Nafsi, kuhukumiwa ndani, hali ya udhaifu wa nafsi, kujionea huruma haya. Yote yanavunja mtu kuliko adui walio nje yako.
Watu wengi wanaishi katika kifungo cha kujiwekea (cages), hawa wanaruhusu mafikira yao binafsi kudhibiti umbali watakao enda katika maisha yao.
Gideoni mwana wa Yoashi hata ingawa alikuwa amechaguliwa na Mungu kubwa mkombozi wa Isreali, alijificha katika pango kwa hofu kuu.
Gideoni alijiona kuwa bure kupigania nchi na taifa lake.
Lakini Mungu naye aliona ndani ya Gideoni shujaa hodari. Ndipo Mungu akamwita toka mafichoni katika lile pango.
Kama Gideoni hakuvunja kile kidhibiti cha hofu ndani ya maisha yake, Gideoni hangaliweza kubwa mkombozi na muamuzi katika Isreali.
Kama wewe na mimi hatutavunja mafikira duni tulionayo katika akili zetu hatuwezi kufanya mapenzi na makusudi ya Mungu juu ya maisha yetu na kutimiza hatima zetu.
Kuvunja hizi vizuizi vya ndani ndio mwanzo wa kutimiza hatima zetu katika Bwana. Hebu tuone:-
JINSI YA KUTAMBUA VIUIZI NA VIDHIBITI VYA NDANI.
- Kabla kupata ushindi juu ya adui walio inje yako ni lazima kushinda walio ndani yako.
- Kujifahamu na ufahamu wa binafsi ni wa maana sana katika mageuzi ya Binafsi.
- Hofu ya kutofaulu-(2nd Timotheo 1:7).
- Hofu ni roho inayo dhoofisha na kuharibu kabisa hatima ya mtu.
- Ndoto na maono ya watu wengi yamekufa kwa sababu ya hofu.
- Hofu inafanya mtu aone Giza badala ya kuona Nuru mbele.
- Kujiona duni na kujiona bure ni kizuizi kubwa ( Negative self-image and negative identity)-(Wamuzi 6:15).
- Gideoni alijiona kuwa mdogo zaidi katika nyumba ya baba yake, Na kabila yao ndio ndogo zaidi katika Manase!! Na maskini zaidi.
- Unapojipima kulingana na ulikozaliwa, umaskini wako na watu wenu, udhaifu wenu, tayari umejiwekea kikwazo kuinuka.
- Maisha ya Kale magumu yaliokupata yanaweza kudhibiti akili yako-(Isaya 43:18).
- Watu wanapo ruhusu, yaliopita kutawala maisha yao, yawe ni Mabaya waliopitia, yawe ni Magumu waliyopata, hawa watu wanakwama mahali moja tu.
- Mungu anapenda tuyasahahu yaliyopita tupate kutazama yaliomapya.
- Kujilinganisha na watu wengine hili ujipime nao ni dhambi kubwa-(Wagalatia 6:4).
- Usijilinganishe na watu wengine kupima dhamani yako.
- Unapojipima na kujilinganisha na watu wengine utajisikia bure na kukupatia wivu.
- Mungu alikuumba tofauti na kiumbe mwanya kabisa na viumbe vyote.
- Kujipima na watu wengine na kulinganisha na wao kunakifanya kuwa kipofu kwa vipawa vyako kutoka kwa Mungu.
- Wale wapelelezi waliotumwa na Musa walijiona kuwa mapanzi, si kwa sababu wanafili waliwaona kubwa mapenzi–(Hesabu 13:33).
MUNGgU ANAVYOKUONA NA JINSI UNAVYOJIONA (GOD’S VIEW VERSUS YOUR VIEW).
- Uhuru wa kweli unapatikana wakati utakaye acha kujiangalia na macho yako mwenyewe na kuanza kujitazama na macho ya Mungu.
- Mungu anatazama nguvu na uwezo wako wala si udhaifu wako–(Waamuzi 6:12)
- Mungu alimwita Gideoni shujaa hodari hata kabla ya Gideoni kupigana vita hata moja!!
- Mungu anaongea na hatima yako si kwa hali yako ya sasa.
- Mungu anawatumia walio dhaifu apate kuonyesha nguvu zake–(2nd Wakorintho 12:9)
- Mungu anapenda sana kuwatumia walio dhaifu hili nguvu na uwezo wake zipate kumpa utukufu.
- Udhaifu wako sio kizuizi kwa Mungu– udhaifu wako ni nafasi kubwa ya Mungu apate kukutumia.
- Mungu tayari amekuhami na kila kitu unachohitaji katika maisha–(2nd Petro 1:3)
- Mungu amekupa yote anayohitaji kwa kuishi na utaua (godliness)
- Wewe pamoja nami hatujapungukiwa na kitu chochote, bali tumejazwa na kila tunachohitaji.
- Vikwazo na udhaifu wako havijafichwa mbele ya macho ya Mungu–(Kutoka 4:10-12)
- Mungu alimweleza Musa kwamba, Mungu ndiye muumba ya wote anatufahamu zaidi ya jinsi tunavyo kufahamu.
- Yeremia alijiona mtoto, bila nguvu na ufahamu–(Yeremia 1:6-10)
JINSI YA KUJIWEKA HURU KUTOKANA NA IMANI (ITIKADI) ZINAZO KUDHIBITI.
- Njia ya kujiweka huru ni dhairi. Ni lazima kutumia mipango ya kiroho kuvunja imani potovu zinazo kudhibiti akili.
- Tumia neno la Mungu kukuweka huru–(Warumi 12:2)
- Kufanywa upya akili na nia kunaanza katika mafikira yetu.
- Waza yalio kweli na kutupa mbali uongo.
- Zungumza na bashiri uzima juu ya maisha yako kila siku–(Mithali 18:21)
- Jitangazie mema juu ya maisha yako, jipe moyo katika Bwana na nguvu zake–(Mithali 27:17).
- Shirikiana na watu wanao kudhamini, watu wanao kusaidia kuvunja ngome zilizoko ndani ya maisha yako–(Yoshua 1:9).
- Daudi alikataa kutumia silaha na mavazi ya mfalme Sauli, alikataa kupingana huku amevaa mavazi ya mwingine–(1 Sam. 17:38-40).
MWISHO
- Vidhibiti vya ndani ni adui kubwa kuliko adui walio kando yako.
- Unapogundua vizuizi vilio ndani yako na kuvitoa utapata uhuru wa kumtumikia Bwana.
- Leo Mungu anakuita ukajiweke huru kutoka kwa roho duni, roho ya kujidharau, roho ya hofu, roho ya kujiona wewe bure, roho ya majina duni uliyoitwa na watu kitambo.
- Nguvu zako ziko katika Yesu Kristo, na hakuna vizuizi vinavyoweza kuvunja hatima yako katika Bwana.
Maombi:-
- Bwana, nifichulie vizuizi vilivyo ndani yangu, nipe nguvu ya kuvikabidhi.
- Bwana, ninavunja kila roho ya kujiona bure.
- Leo nimeshinda roho ya hofu ndani yangu.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.