Categories: Swahili Service

JINSI YA KUVUNJA VIKWAZO ZA BARAKA ZAKO

MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA.

SOMO: 2 WAFALME 2:19-22

 

Ujumbe wa leo ni juu ya jinsi tunaweza kupata ukombozi juu ya maovu. Pengine wewe utasema pasta, mimi nimeokoka, hivyo tayari nimekombolewa kutokana na uovu wote, hivyo mimi sihitaji kusikia maujumbe juu ya ukombozi.

Lakini wewe unaishi dunia gani? Maana Biblia inazungumzia juu ya tenzi tatu za kuokoka. Tuliokolewa (past), tunaokoka (present), tutaokolewa (future).

Yesu Kristo alitia maanani sana juu ya ukombozi mpaka akatufundisha kwamba tunapoomba kusema, “Bali utuokoe na ubaya.” Hebu tutazame:-

TUNAHITAJI UKOMBOZI KUTOKANA NA MAMBO

  • Tunahitaji ukombozi kutoka nguvu za uovu.
  • Tunahitaji ukombozi kutoka wanaopanga maovu.
  • Tunahitaji ukombozi kutoka kwa mapenzi yetu kutenda maovu.
  • Tunahitaji ukombozi kutoka kwa watu wa uovu, watu wanaouza maovu, uwepo wa maovu, tabia na mipango ya uovu.
  • Tunahitaji ukombozi kutoka kwa aibu, mateso, utawala, uhalifu na mafundisho ya uovu.
  • Tunahitaji ukombozi kutokana na wanaofundisha maovu, wanaotumia maovu.
  • Maombi na sala ya Bwana- “Bali utuokoe na yule mwovu.”
  • Leo hii somo letu ni juu ya ukombozi kutokana na hukumu juu ya dhambi za baba na babu zetu (sins of the fathers).
  • Wewe na mimi tunahitaji ukombozi juu ya vizuizi vinavyozuia baraka zetu.
  • Kwa kweli Yesu Kristo alilipa deni ya dhambi zetu zote, lakini pia ni kweli hukumu zingine zinadumu mpaka sasa, kama vile mpaka leo miiba na kwekwe zingalipo mashambani, wanawake wangali wanazaa kwa utungu mwingi, mpaka wengine wanakufa wanapozaa, tungali tunapata chakula kwa jasho jingi, pia tungali tunakufa mauti.
  • Katika 2 Sam. 12:13-14, Nabii Nathani alimwambia mfalme Daudi, kwa sababu ya ile dhambi ya uasherati na mauaji, kwamba amesamehewa lakini yule mtoto lazima atakufa!!
  • Pia kwa sababu ya ile dhambi maovu na upanga hautatoka nyumbani mwa mfalme Daudi.
  • Mimi ninaamini kwa neno la Mungu kwamba familia inaweza kulaaniwa! Kudumu kwa laana, lakini pia laana inaweza kuondolewa kwa nguvu za Mungu.
  • Laana zinaweza kubadilishwa zikawa baraka kupitia damu ya Yesu Kristo.
  • Walawi walitawanyika katika Israeli kupitia laana- Mwanzo 49:5-7.
  • Laana juu ya Lawi na Simioni ilitokana na baba yao.
  • Lakini naye Musa alivunja hiyo laana juu ya Walawi- Kumb. 33:8-11.
  • Mle Yeriko Elisha alibadilisha laana yake, zikawa baraka- 2 Wafalme 2:21.
  • Hivyo laana ya Yoshua ikaisha juu ya watu na mji wa Yeriko- Yoshua 2:26.
  • Yeriko ulikuwa mji mzuri sana, lakini walikuwa na shida ya ndani.
  • Ni kama wewe pia. Tunakuona ukipendeza sana, umbo zuri, kazi nzuri, masomo mazuri, lakini unazaa mapooza!!- 2 Wafalme 2:19.

SHIDA, CHANZO CHAKE NA DAWA YAKE

  1. Shida za Yeriko- 2 Wafalme 2:19.
  • Mungu alikuwa amekataza Yeriko kujengwa tena.
  • Mungu kupitia Yoshua alilaani Yeriko maji chungu- sumu. Ardhi na udongo wake zililaaniwa, kiasi nchi huzaa mapooza.
  • Maji ya Yeriko yalifanya wanyama wakinywa yale maji mimba zao zinatoka, mimea inatupa maua na matunda yake yangali mabichi.
  • Hata wake zao zilimwagika!! Hivyo laana ya Yeriko ilikuwa mbaya zaidi, lakini pia hio laana ilikuwa fiche. Baada ya miaka 600, watu wa Yeriko hawakufahamu kinachowafanyikia wao.
  • Dhambi za mababa na mababu na laana juu yao inakuwa siri kubwa, watoto wasijue kinachowakula!!
  • “Maji yake hayafai”- katika Kiebrania ni (“ra”) Maanake ni “ovu” (evil)- Mwanzo 6:5; Mithali 3:13; Mwanzo 2:9, “Ovu” maji hayo yaliumiza watu, wanyama na mimea kama jinsi upanga- Zaburi 144:10- “Upanga wa uovu.”
  • Yeriko pamoja na kuwa nchi nzuri na kupendeza macho, ilikosa jambo moja la maana zaidi (maji).
  • Yeriko ilikuwa kama jinsi Naamani, hodari, sifa na ujuzi, lakini alikosa cha maana zaidi katika maisha- Afya!!- 2 Wafalme 5:1.
  • Naamani alikuwa mwenye ukoma!! Pamoja na sifa zote, utajiri, ukoma wa Naamani ulimnyima yote- mke, watoto, marafiki.
  • Kisima cha maisha kinapokuwa chungu-sumu, hakuna faida- dhambi ni mbaya!!
  • Somo ndio hii- hata ingawa mambo yako yanaendelea, lakini kuna kizuizi kwa baraka zako.
  1. Chanzo cha laana.
  • Chanzo cha shida ya Yeriko ilikuwa fumbo kwa watu wake.
  • Lakini shida yao sisi twafahamu ilikuwa laana- Yoshua 6:17-26.
  • Shida ya Yeriko haikuwa maji, ardhi yao, lakini laana!!
  • Je, unaweza fikiri jinsi watu wa Yeriko walifanya kazi kwa bidii?
  • Mji wa Yeriko ulikuwa na wana wa nabii zaidi ya 50!!
  • Hawa manabii hawakuweza kufanya chochote Yeriko maana hawakujua dawa ya shida zao.
  • Hukumu juu ya dhambi za baba zao ikawa kizuizi kwa baraka zao.
  • Baraka zao zilikuwa zinawakwepa wao (abortion).

VIZUIZI VYA BARAKA ZAO

  1. Kupuuza amri za Mungu- Kutoka 4:24.
  • Musa alikataa kuwatahiri wanawe akapuuza amri za Mungu juu ya Agano.
  • Wewe unaweza kuwa umeokoka lakini je, umebatizwa Kibiblia katika maji mengi mbele ya watu?
  • Tunabatizwa kwa sababu tumeokoka, lakini si tunabatizwa ili tuokoke!!
  • Ubatizo wa kibiblia ni kwa watu wazima si kwa watoto wachanga!!
  1. Kuvunja Agano- 2 Sam. 21:1.
  • Mfalme Daudi na Israeli wote walipata janga la njaa kwa miaka mitatu (3) kwa sababu mfalme Sauli alivunja ile Agano la Israeli na watu wa Gibeoni (Wagibeoni).
  • Kumbuka Daudi sio yeye alifanya Agano na Wagibeoni, wala si Daudi aliwaua wale Wagibeoni, lakini Daudi aliteseka na Israeli.
  • Mungu, ni Mungu wa Agano- Zaburi 25:14.
  • Watu wengine hawajatubu dhambi ya kuachana na wake zao.
  • Wengine wanachumbia wanawake wake zao wangali hai. Wanavunja maagano ya ndoa zao.
  1. Kuweka vikwazo mbele za watu- Luka 17:1-2.
  • Kuna watu tunaoweka vikwazo mbele yao.
  • Je, uliweka kikwazo kwa watu, mpaka sasa hujakitoa kile kikwazo.
  • Ulichumbia binti akashika mimba, akazaa mtoto yuko hapa duniani na wewe haukujali.
  • Wengine uliwafundisha dhambi, pombe, madawa ya kulevya.
  • Umeokoka leo lakini wao wanaenda jehanamu. Je, unajali vikwazo  uliofanya mbele za wengine?
  • Leo waombee waondolewe vikwazo na majeraha yao.
  1. Kumkosea mke wa ujana wako- 1 Petro 3:7; Malaki 2:14-16.

DAWA YA LAANA NA VIKWAZO VINAVYOZUIA BARAKA ZAKO- 2 Wafalme 2:20-21

  1. Pambana na kiini chenyewe si ishara zake.
  • Elisha alienda kwa kisima chenyewe.
  1. Lazima kuweka kitu katika kiini chenyewe kuvunja nguvu za laana- Kutoka 15:23:25.
  2. Elisha alitumia chumvi.
  3. Elisha alifanya tendo la unabii.
  • Watu walileta chumvi na bakuli mpya.
  • Nabii Elisha alitumia neno la Mungu na kuweka ile chumvi.
  • Mungu aliponya yale maji kabisa mpaka leo zaidi ya miaka elfu tatu (3,000 years).

MWISHO

  • Hebu tukamwamini Mungu kwa uponyaji na msamaha juu yetu na baba zetu.
  • Hebu tukakubali msamaha na urejesho wa Mungu kwetu.
  • Hebu tukapokee uponyaji, kuondolewa vikwazo na kupokea baraka za Mungu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

4 weeks ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago