Categories: Swahili Service

JINSI YA KUWASHINDA ADUI ZAKO

SOMO: ZABURI 81:13-14

 

Zaburi 81 inaanza na mwaliko wa sifa na ibada. Iliandikwa kuwa Zaburi ya sifa kwa bara mwezi, inatueleza jinsi Mungu alivyo wakomboa wana Israeli kutoka utumwa Misri.

Zaburi hii iliandikwa na Asaphu, alikuwa nabii. Katika mistari ya 8-11, anaanza kutoa unabii kwa nguvu za Mungu, jinsi Israeli wamekataa kusikiza sauti ya Mungu na kukata, kumtii, hivyo Mungu amewaacha kwa mbinu na njia zao potevu.

Katika mistari ya 13-14, twaelezwa jinsi yalivyo mapenzi ya Mungu kuwashinda maadui zetu. Hivyo ujumbe wetu hivi leo ni “JINSI YA KUWASHINDA ADUI ZETU”-

KILA MMOJA WETU ANAO MAADUI.

Je, wewe unao maadui?

  • Adui ni kila mtu hau watu wanaokuchukia, wanaopinga, wanaopenda kukuudhi, wanao kuzuia kufanya isifanye malengo yako.
  • Sisi zote tunao maadui, watu wasiopenda mawazo yetu, misimamo yetu, watu wanao wivu juu ya maendeleo yetu.
  • Hata ikiwa huna adui hapa duniani, bado unao adui-shetani.
  • Shetani alikuja kuiba, kuua na kuharibu-Yohana 10:10.
  • Lazima kila wakati tuwe tayari kwa vita na ibilisi shetani kwa kukaa upande wa Mungu na chini ya ulinzi wake.

Mungu ameahidi ulinzi kwa watu wake-2 Mambo ya Nyakati 15:9, Zaburi 34:7, Zakaria 2:5, Luka 21:18.

Je, sisi tuko na adui ndani yetu?

  • Adui mkubwa ni sisi wenyewe-kiburi chetu, ubinafsi wetu, uzembe wetu, tamaa zetu na ulafi wetu.
  • Tunahitaji kufuata ushauri wa Yaboko na kumpinga shetani.
  • Je, utatembea na shetani au utatembea na Mungu?

NJIA MBILI KUPATA USHINDI

  • Zaburi 81:13-14, ushindi wetu uko na Bwana.
  • Ushindi wetu utatufikia tunapojipanga upande wa Mungu na shabaha zake.

“Laiti watu wangu wangenisikiliza.”

  • Watu wengi wanasema wanamsikiliza Mungu lakini si kweli-Mathayo 13:13.
  • Katika Zaburi 81:11, Mungu anawaonya watu wake kukataa kusikiza-Warumi 1:24-28.
  • Tunahitaji kumsikiliza Mungu kwa mioyo yetu si kwa maskio yetu-Wakolosai 3:1-4.

“Enendeni katika njia zangu”-Zaburi 25:4.

  • Kuenenda katika njia za Mungu ni kusoma na kutii neno la Mungu,

NJIA YA YESU KRISTO KUWASHINDA ADUI.

Penda adui zako-Mathayo 5:43-45.

  • Mtume Paulo-Warumi 12:20.

Shinda uovu kwa mema-Warumi 12:21.

  • Unapompendeza Mungu, Mungu atawafanya adui zako kuwa na amani nawe-Mithali 16:7.

MWISHO

  • Mungu alisema “ikiwa watu wangu wanisikiliza na kunifuata nitawashinda adui zako na mkono wangu utawamaliza.
  • Je, unao adui wanaokusumbua moyo? Chagua njia ya Mungu kupambana nao.
  • Je, unamfanya Mungu kuwa Bwana na Mwokozi wako, na kumsikiliza na kumtii yeye pekee?
  • Njia pekee ya kuwashinda adui zako ni kumsikiliza Mungu na kufuata njia zake!
  • Leo, tujisalimishe kwake na kuwaweka adui zetu mikononi mwake. Amen.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

14 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

16 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

18 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago