Categories: Swahili Service

KANISA MLANGO WAZI.

MAKANISA SABA YA UFUNUO

UFUNUO 3:7-13.

Tunaendelea somo letu katika Nyaraka Saba za Mwokozi wetu Yesu Kristo kwa makanisa saba ya Asia Ndogo (Asia Minor). Tayari tumeona makanisa tano kwa makanisa yote saba. Tunaendelea kutazama kitabu hiki cha Ufunuo. Napenda kuwakumbusha kwamba makanisa haya yanaweza kueleweka kwa njia tatu.

  1. Nyaraka hizi ziliandikiwa makanisa yaliyokuwa Asia wakati ule na siku zile.
  2. Nyaraka hizi zinaweza kueleweka kiunabii.
  • Kila moja ya haya makanisa ya Ufunuo inasimamia wakati fulani katika historia ya kanisa tangu Pentekoste mpaka kunyakuliwa kwa kanisa mbinguni.
  • Kanisa la Filadelfia linasimamia wakati wa 1,700AD-1980AD.
  • Katika wakati huu, kanisa la kweli la Yesu Kristo, ingawa ndogo ki idadi, kanisa lilianzisha ‘mission’ duniani kote. Huu pia umekuwa wakati wa ufufuo na uamsho mkuu sana duniani na zaidi Marekani na Uingereza mpaka uamsho wa Africa Mashariki yaani East African Revival.
  1. Nyaraka hizi pia zinaweza kueleweka kibinafsi. Kila Mkristo anaongeleshwa na Mungu katika barua hizi na pia kila kanisa.

Leo hii twatazama waraka huu kwa kanisa la Filadelfia.

  • Hebu nihubiri juu ya kanisa mlango wazi.
  • Filadelfia ulikuwa mji mdogo kuliko miji yote katika Asia Minor na miji yote saba Kristo alipotuma nyaraka hizi saba.
  • Filadelfia ulikuwa mji wa mlangoni wa Asia minor na Asia kubwa. Filadelfia ulijengwa katikati ya milima miwili na njia nyembamba yaani pass.
  • Filadelfia ulikuwa mji wa majeshi ya Roma.
  • Filadelfia ulipata jina hili kutoka kwa Mfalme Attalus 2, mfalme wa pili wa Pergamo. Mfalme Attalus 2 alijulikana sana kwa sababu ya mapenzi yake makuu kwa ndugu yake Eumenes. Baadaye huyu ndugu Eumenes alikuja kuitwa Philadephos. Maanake “Philadephos” ni “yule anayempenda ndugu yake.” Hivyo Filadelfia ulikuja kujulikana kama “Mji wa Upendo”-“The City of brotherly Love.”
  • Kanisa la Filadelfia lilistahimili kwa miaka nyingi mpaka mwaka wa 1000AD wakati Filadelfia ulivamiwa na Waislamu kutoka Mashariki ya Kati na kanisa la Filadelfia likafa mpaka leo.
  • Yesu Kristo hakuona lawana yoyote juu ya kanisa la Filadelfia. Hivyo Kristo anawajia na maneno ya faraja, pongezi na ahadi.
  • Maneno ya Yesu Kristo kwa Filadelfia kanisa aminifu ni faraja kwetu leo. Hebu tupate mahubiri juu ya “Kanisa mlango wazi” :-
  1. KANISA LA FILADELFIA NA BWANA WAO (Ufunuo 3:7-8)
  2. Bwana wa kanisa la Filadelfia anajitambulisha
  • Yesu Kristo anajitambulisha kwa njia mbili.
  1. Anawajia kama yeye aliyemtakatifu.
  • Maana ya “Mtakatifu” ni kwamba Yesu Kristo ni bila dhambi-ni safi kabisa.
  • Biblia inamshuhudia Kristo kuwa mtakatifu. 1 Peter 2:22 “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.” 2 Wakorintho 5:21 “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki.”
  • Jehanamu inatoa ushuhuda juu ya Kristo. Marko 1:25 “Nakutambua u nani, wewe ni mtakatifu wa Mungu…….”
  • Mbingu inatoa ushuhuda juu ya Kristo. Luka 1:35 “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.”
  • Ushuhuda wa Yesu Kristo juu yake mwenyewe. Yohana 8:46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”
  • Yesu Kristo anazungumza na kanisa lililo jaribu sana kuishi katika utakatifu katikati ya dunia ya dhambi na ufisadi.
  1. Kristo anawajia wa Filadelfia kama yeye aliye wa kweli.
  • Yesu Kristo ni yeye aliye kweli. Filadelfia walizungukwa na ibada za sanamu na miungu ya uongo.
  • Yesu Kristo ndiye kweli, Mwokozi wa ulimwengu-Matendo 4:12; Yohana 14:6.
  • Tunaishi katika dunia ‘fake’. Watu fake, sukari fake, nyama na mayai fake, wamama na wababa fake, mambo mengi ni fake hapa duniani hata makanisa.
  1. Mamlaka ya Bwana wa kanisa la Filadelfia.
  • Yesu Kristo anasema ni yeye aliye na mamlaka, yeye aliye na ufunguo wa kufunga na kufungua.
  • Yesu Kristo anabeba “Ufunguo wa Daudi”-Isaya 22:20-25.
  • Eliakimu katika unabii wa Agano la kale alikuwa picha ya Yesu Kristo.
  • Ufunguo maanake ni mamlaka, njia na uwepo.
  • Kristo anazo funguo za mauti. Ufu. 1:18 “Aliye hai, nami nilikuwa nimekufa, na tazama ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.”
  • Yesu Kristo ndiye Bwana wa mauti. Huwezi kufa mpaka yeye afungue mlango, huwezi kukaa mauti ikiwa unamfahamu-Yohana 11:25-26.
  • Yesu Kristo ndiye anazo funguo za kuzimu, yeye pekee anafungua na kufunga jehanamu. Yeye ndiye funguo za mbinguni.
  • Yesu Kristo ndiye anazo funguo za wokovu. Ni yeye uzima wa milele kwa wote wamjiao-Yohana 14:6; Yohana 10:9.
  • Yesu Kristo ndiye anazo funguo za huduma-1 Wakorintho 16:9.

Kristo anaamua tutahudumu wapi, lini na muda wa huduma.

  • Yesu Kristo anazo funguo za usalama wetu-Wakolosai 3:3. Hakuna anayeweza kuwaguza walio wake.
  • Yesu Kristo yuko katika kazi ya kufungua na kufunga milango-Matendo 16:6-10.
  1. Pongezi ya Bwana wa kanisa la Filadelfia.
  • Kristo anawaeleza wa Filadelfia kwamba anayajua matendo yao. Anafahamu yote, nia zao na matendo yao-Waebrania 14:13; Mithali 15:3.
  1. KANISA LA FILADELFIA NA HUDUMA YAO (U funuo 3:8-11)
  2. Huduma yao ilihusu nafsi.
  • Yesu Kristo alikuwa amewapa wa Filadelfia mlango wazi wa huduma.
  • Yesu anawaambia kwamba wanazo nguvu kidogo, yaani hawakuwa wengi. Fedha zao zilikuwa ndogo lakini Bwana aliwapa nguvu za kumtumikia.
  • Yesu Kristo anawaambia kwamba wamelitunza neno lake-walikaa katika doctrine ya neno la Bwana.
  • Yesu Kristo anawaambia kwamba wao hawakulikana jina lake-waliendelea kuhubiri habari njema ya Injili na nguvu za Shetani hazikuweza kuzima ushuhuda wao kwa ulimwengu.
  1. Huduma yao ilihusu upinzani.
  • Sinagogi la Shetani lilikuwa pale Filadelfia.
  • Sinagogi la Shetani lilikuwa ni Wayahudi waliopingana na Injili ya Kristo.
  • Sinagogi la Shetani ni watu wanaosema wameokoka lakini bado wanashika dhambi.
  • Sinagogi la Shetani ni watu wanaosema wanampenda Mungu lakini maisha yao ni kinyume-Ufu. 21:8.
  • Yesu Kristo anawaambia kitambo kidogo Mungu atawahukumu mara-Wafilipi 2:10-11.
  • Kanisa linalohubiri kweli linachukiwa na zaidi siku hizi za mwisho.
  1. Huduma yao ilihusu imani na subira.
  • Bwana amewaahidi ulinzi wakati wa kujaribiwa dunia hii.
  • Ukombozi wao utaonekana wakati janga za dunia zinakuja juu ya ulimwengu.
  • Katika wakati wa kujaribiwa dunia, Mungu atakuwa pamoja na wa kanisa la Filadelfia.
  1. Huduma yao ilihusu kushika imani (Vs. 11)
  • Yesu Kristo anawaambia kushika mambo mawili.
  • Wanaitaji kusubiri kuja kwa Bwana mara ya pili.
  • Wanahitaji kushika sana mwenendo wao wa imani.
  • Waangalie wasinyang’anywe taji yao.
  • Kristo anawaeleza kumwishia Kristo na kumtazama Kristo.
  • KANISA LA FILADELFIA NA UJUMBE WAO (Ufunuo 3:12)
  1. Ujumbe wa udhabiti.
  • Yesu Kristo anawaahidi wa Filadelfia kuwafanya nguzo ya hekalu la Bwana Mungu.
  • Filadelfia watakuwa na udhabiti hata ingawa pale Filadelfia palikuwa mahali pa tetemeko la ardhi mara kwa mara.
  • Kristo anawaeleza hata tetemeko, dhoruba, majaribu na shida ziwe kwao, Kristo angali mwamba ulio salama.
  • Katika hekalu za Shetani, heshima kuu ilipewa wale wamejenga nguzo za hekalu. Majina yao yaliandikwa juu ya hizo nguzo.
  • Kristo anawaambia atawafanya nguzo katika hekalu ya mbinguni.
  1. Ujumbe wa usalama.
  • Usalama wetu u katika Yesu Kristo. Kwamba yeye ni wetu na sisi tu watu wake.
  • Wakristo wa Filadelfia hawakuwa salama katika mji wa Filadelfia lakini usalama wao uko katika Kristo Bwana.

MWISHO

  • Mlango wa hatima yako umefunguliwa na Yesu Kristo.
  • Bwana ametupa funguo za kufungua milango ya kibali, ushindi, ukombozi na kupenya, kufaulu, afya na amani.
  • Sifa zilifingua milango ya gereza-Matendo 16:22-27
  • Maombi-Luka 11:5-10.
  • Hodari-Zaburi 24:7-8.
  • Kutoa-Malaki 3:6-10
  • Mungu akufungulie mlango leo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago