Categories: Swahili Service

KANUNI ZA UFALME WA MUNGU

MFULULIZO: JINSI YA KUISHI KATIKA UFALME WA MUNGU. 

SOMO: MATHAYO 6:33.

 

Ufalme wa Mungu si tu mahali, lakini ni hali ya kuishi. Katika ufalme wa Mungu tunaishi kulingana na kanuni za mbinguni. Tunapoishi sawa sawa na kanuni za ufalme, hapo ndipo tunaishi katika nguvu, baraka na amani.

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa”-Mathayo 6:33.

Ufalme wa Mungu unafanya kazi yake tofauti na falme na serikali za ulimwengu. Falme za dunia hii zimejengwa juu ya nguvu, utajiri na heshima, amani na furaha katika Roho Mtakatifu-Warumi 14:17.

Yesu Kristo katika uduma yake hapa duniani alifundisha na kuonyesha jinsi ufalme wa Mungu ulivyo, kanuni zake na jinsi ya kuishi na kuhisi utimilifu wa baraka za Mungu.

Tunapoelewa kanuni za ufalme wa Mungu na kujipanga sawa sawa na mapenzi ya Mungu, tutaona jinsi ufalme wake ulivyo.

Kanuni hizi si sheria au amri, bali ni kanuni za kiroho zinazo simamia jinsi nguvu, utoshelevu na mapenzi ya Mungu yanavyotekelezwa.

Tunapoishi sawa sawa na kanuni zake, basi tutakuwa tumeingia katika nafasi ya kupokea kupenya na dhawabu za milele.

Leo tunatizama kanuni zile za juu zaidi katika ufalme wa Mungu na jinsi ya kudumisha uhusiano na ushirika wetu na Mungu, tukapate kutimiza malengo ya Mungu duniani. Hebu tutazame:-

KANUNI YA KUUTAFUTA KWANZA UFALME WA MUNGU.

  • Ni mapenzi ya Mungu kwamba ufalme wa Mungu na haki yake ziwe maanani zaidi katika maisha yetu.

Ufalme wa Mungu kwanza.

  • Kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza, zaidi ya yote tutafutao ni kutafuta kufanya mapenzi ya Mungu juu zaidi ya mapenzi ya binafsi-Mathayo 6:33.

Tafuta haki yake zaidi ya vitu vya dunia hii.

  • Ufalme wa Mungu si kupata mali ya dunia hii lakini ni hali ya kuwa na uhusiano na Mungu-Warumi 14:17.

Mtegemee Mungu kwa ukamilifu.

  • Tunapomtegemea Mungu kwa ukamilifu, yeye atatutosheleza mahitaji yote, bila kukimbilia vitu-Wafilipi 4:19.

Dhawabu ya kumpa Mungu kibao kwanza.

  • Wale wanao mpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha na shughuli zao, wanapata utoshelevu, usalama na amani-Zaburi 37:25.
  • Mfalme Suleimani aliutafuta kwa ufalme na hekima ya Mungu-akapata kuongezewa yote-1 Wafalme 3:5-13.

KANUNI YA IMANI.

  • Imani ndio sarufi (fedha) inayonunua vyote kutoka kwa Mungu, bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu.

Imani ni muhimu zaidi, tupate kushirikiana na Mungu na kupokea ahadi zake-Waebrania 11:6.

Tunaishi kwa imani, bali si kwa kuona.

  • Wenyeji wa ufalme wa Mungu wanategemea neno la Mungu, wala si hali ilivyo duniani-2 Wakorintho 5:7.

Imani inaachilia nguvu za Mungu ndani yetu.

  • Yesu Kristo alitenda miujiza palipokuwa na imani-Marko 11:23-24.

Imani lazima ijaribiwe.

  • Majaribu yanatia nguvu imani yetu na tegemeo letu kwa Mungu-Yakobo 1:3-4.
  • Imani ya Ibrahimu ilijaribiwa sana-Baadaye Ibrahimu amekuwa baba wa Imani, baba wa mataifa-Warumi 4:18-21.

KANUNI YA KUWAUDUMIA WENGINE.

  • Yesu Kristo alitueleza kwamba atakayependa kuwa mkuu ya wengine lazima awe mtumishi wa wote.

Uongozi kupitia utumishi.

  • Atakaye kuwa mkuu zaidi katika ufalme wa Mungu ni lazima awe mtumishi wa wote-Marko 10:43-45.

Watumikie wote kwa upole.

  • Majivuno na kiburi hakina nafasi katika ufalme wa Mungu, unyenyekevu unavuta kibali cha Mungu-Yakobo 4:6.

Tumikia wengine kwa upendo.

  • Upendo ndio msingi wa utumishi wa kweli-Wagalatia 5:13.

Dhawabu ya utumishi.

  • Wale watakaotumika kwa uaminifu, wao wataheshimiwa na Mungu-Mathayo 25:21.
  • Yesu Kristo hata ingawa alikuwa Mungu, alinyenyekea kiasi akatawadha wanafunzi wake-Yohana 13:12-17.

KANUNI YA UWAKILI.

  • Kila tulichanacho kimetoka kwa Mungu, sisi ni mawakili wa mali yake Mungu.

Mungu ndiye mwenye vyote.

  • Sisi kazi yetu ni kutunza baraka zote tuliopewa, sisi si wamiliki bali mawakili-Zaburi 24:1.

Tuwe mawakili waaminifu.

  • Mungu anahesabia tukatumie talanta, wakati na hazina zetu vyema-Mathayo 25:14-30.

Kutoa katika ufalme.

  • Kutoa mali, wakati, talanta, fedha zetu, zinazidishwa-Luka 6:38.

Tunahesabika mbele za Mungu.

    • Siku moja sisi sote tutatoa hesabu, jinsi tulivyotumia vipawa vyetu-Warumi 14:12.
  • Wanaoweka raslimali zao vyema, watapata dhawabu ya Mungu-Mathayo 25:20-30.

KANUNI YA UPENDO NA MSAMAHA.

  • Upendo na msamaha ni kanuni ya msingi katika ufalme wa Mungu.

Upendo ndio amri iliyo kuu zaidi mbele ya Mungu.

  • Amri zote si sawa mbele ya Mungu, wala dhambi zote si sawa mbele ya Mungu!!
  • Kumpenda Mungu na kuwapenda wengine ni kutimiza amri za Mungu-Mathayo 22:37-40.

Msamaha ni mapenzi ya ufalme wa Mungu.

  • Ni lazima kuwasamehe watu wote dhambi na makosa yao, ili sisi nasi tupate msamaha-Mathayo 6:14-15.

Kuwapenda adui zetu.

  • Wenyeji wa ufalme wa Mungu wanaonyesha upendo hata kwa wale wasiowapenda-Luka 6:27.

Upendo ni ishara ya kweli ya kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo.

  • Yesu Kristo alisema ulimwengu utajua kwamba sisi ni wafuasi wake tunapopenda na kuwapenda walio nje ya ufalme wake-Yohana 13:35.
  • Yusufu aliwasamehe ndugu zake, hata ingaa walimsaliti na kumuuza kuwa mtumwa Misri-Mwanzo 50:19-21.

MWISHO

  • Ufalme wa Mungu si tu mahali fulani, lakini ufalme wa Mungu umetawaliwa na kanuni za Mungu.
  • Tunapotimiza kanuni za ufalme wa Mungu ndipo tutahisi nguvu, baraka na amani.
  • Yesu Kristo alitufundisha jinsi ya kuishi ufalme wa Mungu na ni mataumaini yake tukamfuate kama mfano wetu.
  • Sisi sote tu, kama Kristo tunapotimiza kanuni hizi, ndipo tutakuwa kama Mwokozi wetu Yesu Kristo, kwa utukufu wa jina lake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE

TEXT: LUKE 2:1-14.   The birth of Jesus Christ shattered spiritual, social and eternal barriers,…

15 hours ago

CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME?

TEXT: JOHN 3:16-17.   Christmas unveils the divine mission behind the birth of Jesus Christ;…

1 day ago

KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA

MFULULIZO: KRISMASI NI KUFUNULIWA KWA YESU KRISTO.  SOMO: LUKA 2:8-14.   Krismasi inafunua jibu la…

5 days ago

CHRISTMAS IS WHEN HEAVEN CAME DOWN TO EARTH.

SERIES: CHRISTMAS IS CHRIST. TEXT: JOHN 1:1-14.   Christmas is the divine moment when God…

5 days ago

FOR GOD SO LOVED THE WORLD

TEXT: ISAIAH 53:1-12.   The son of man came to seek and save that which…

5 days ago

JESUS OUR SAVIOR

SERIES: CHRISTMAS IS JESUS CHRIST. TEXT: MATTHEW 1:21   Jesus Christ is the savior of…

2 weeks ago