Categories: Swahili Service

KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI

MFULULIZO: MKARIBU MUNGU.

SOMO: ZABURI 42:7 (42:1-11).

 

Wakristo wengi wanafurahi kukaa katika maji ya ufuoni. Wengi hawapendi kuingia ndani zaidi na kumfahamu Mungu wao. Ukristo wa namna hii hauleti mabadiliko na ukaribu na Mungu. Lakini Mungu anatuita kuingia mpaka kilindini, kilindi cha ibada, kilindi cha maombi, kilindi cha neno, kilindi cha shabaha na lengo, kilindi cha ufahamu wa Mungu.

Kilindi chapigia kelele kilindi ni safari ya kuingia ndani ya Mungu.

Zaburi 42:7, “Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maporomoko ya maji yako, gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.”

Kunao kilio katika moyo, kilio cha kuingia kwa kina, kuingiana na Mungu kilindi kwa kilindi. Kilindi cha Roho wa Mungu kinapigia kelele kilindi cha mioyo yetu.

Huu ni mwaliko wa kumkaribia Mungu kwa karibu zaidi wala si kumjia kwa mbali kama jinsi dini na mapokeo yanavyotaka.

Safari ya kumkaribia Mungu inahitaji kujitoa kama jinsi kujitupa katika kilindi cha bahari.

Mungu ametualika kuingia katika ushirika mkuu.

  • Kilindini ndipo tutapata maajabu ya Mungu kuonekana, kilindini ndipo tutapata uponyaji wake, kilindini ndipo tutapata fadhili na faraja; kilindini ndipo tutapata mizigo kuondolewa, kilindini ndipo tutapata nguvu mpya. Hebu tutazame:-

MWITO WA KILINDI NI MWITO WA KUMKARIBIA MUNGU KWA KARIBU.

  • Kabla Mungu akutumie kwa nguvu ni lazima kwanza akufahamu na kukujua ndani kabisa.
  • Kilindi cha Mungu ni lazima kupigia kelele kilindi cha moyo wako!!

Mungu anafichua siri zake kwa wale wanaomkaribia kwa karibu-Zaburi 25:14.

  • Mungu anashiriki maaajabu yake na wale wanaotumia wakati wao katika uwepo wake.

Ushiriki wa karibu unahitaji kujitenga na vikwazo-Mathayo 6:6.

  • Ni lazima kuingia mahai pa siri tupate kusikia sauti yake.

Uhusiano unakua panapo ushirika wa kuchagua kuwa karibu-Yakobo 4:8.

  • Mungu ameahidi kuwakaribia wale wamtafutao.

Kujitoa kwa reja reja, ki juu juu ni kikwazo kwa ufahamu wa Mungu-Luka 10:41-42.

  • Musa alipata kumjua Mungu uso kwa uso, kwa sababu aliutafuta uso wa Mungu kila wakati-Kutoka 33:11.

KILINDI CHA MUNGU KINALETWA NA NJAA YA KIROHO.

  • Bila kuwa na njaa ya kiroho tutatosheka na makapi wakati Mungu ametutengenezea karamu.

Kilindi cha njaa ya kiroho inatufanya tumkaribie Mungu-Yeremia 29:13.

  • Mungu anakutana na wale wamtafutao kwa mioyo yao yote.

Njaa na kiu ya haki inatufanya kudumu katika kumtafuta Mungu-Luka 18:1-8.

  • Wanao mtafuta Mungu wanapata majibu kwa maombi yao.

Njaa na kiu inavunja uzembe wa kiroho-Ufunuo 3:15-16.

  • Mungu hapendezewi na vugu vugu.
  • Njaa ya kiroho inafungua milango ya Ufunuo wa Mungu-Mathayo 5:6.
  • Mfalme Daudi alipata kiu cha kumwona Mungu mle jangwani na Mungu alimtokea-Zaburi 63:1-2.

SAFARI YA KUINGIA KILINDI CHA MUNGU INAHITAJI KUJITOA NA KUJISALIMISHA.

  • Kilindi cha Mungu kinahitaji kumpa Mungu kila eneo ya maisha, nafsi, mwili, mali, fedha, jamii na elimu.
  • Kujitoa kama dhabihu iliyo hai kuna mruhusu Mungu kufanya kazi yake ndani yetu-Warumi 12:1.
  • Kule kujitoa kabisa kwa Mungu kunaleta mabadiliko ya dhati-2 Wakorintho 3:18.
  • Tunapojitoa kwa Mungu tunafanana naye.
  • Kujitoa ndio njia hasa ya kupokea mamlaka ya kiroho-Wagalatia 2:20.
  • Yesu Kristo anapata kuyaishi maisha yake ndani yetu.
  • Tunapojitoa kwa Mungu mapenzi ya mioyo yetu inaenda sambamba na mapenzi ya Mungu-(Luka 22:42).
  • Isaya alijisalimisha ndipo akapata mwito wa Mungu-(Isaya 6:8).

KILINDI KINAPIMWA NA MAFURIKO YA ROHO MTAKATIFU-(Ezekieli 47).

  • Ezekieli anatuonyesha hatua za kutembea katika Roho Mtakatifu.

Maji ya viweko vya miguu ni kiasi cha Roho Mtakatifu mara tunapookoka.

  • Huu ni mwanzo tu, wala si mwisho wa safari ya kiroho.

Maji ya mpaka magoti, maanake ni maombi na maombezi.

  • Hapa ndipo tunajifunza kuomba na kuwasiliana na Mungu.
  1. Maji ya mpaka viuno maanake ni nguvu za kuzaa matunda bora, mazao yanazidi jinsi tunapoingia katika kilindi cha Mungu wetu.
  2. Maji ya kiasi kisichoweza kuvunjika, maji ya kuogelea maanake ni kule kuingia katika  kilindi cha Mungu.
  • Hapa Roho Mtakatifu anachukua mamlaka juu yetu kabisa.
  • Huko ndio kujazwa kabisa, hapa kilindi cha Mungu kinapiga kelele kwa kilindi cha mioyo yetu.
  • Yesu Kristo alifikia kilindi cha Mungu alipojaribiwa na ibilisi jangwani–(Luka 4:1).

KILINDINI NDIPO NGUVU ZA MUNGU MAUSIA NA UFUNUO WA MUNGU ANAPATIKANA.

  • Ikiwa unapenda kutembea katika nguvu za Mungu na makusudi yake ni lazima kutembea mpaka Kilindini.

Kama unapenda kukaa ufuoni, huwezi kupata nguvu za Mungu-(Luka 5:4-6).

  • Samaki wanapatikana katika vilindi vya bahari.

Mipango ya Mungu kwa maisha yako itajulikana tu Kilindini–( Isaya 6:1-9).

  • Nguvu za Mungu zinapatikana, kilindi cha Mungu kinapo kutana na kilindi cha moyo wako.

Kilindini ndipo hatima yako inapatana na ukuu wa Mungu–(Zaburi 37:4-5).

  • Hapa mapenzi ya Mungu yanakuwa mapenzi ya moyo wako–(Luka 5:10-11).

MWISHO.

  • Mwito wa kufika Kilindini si mwito kwa wachache waliochaguliwa lakini ni mwito kwetu sote.
  • Ukristo wa ufuoni ni Ukristowa starehe lakini inakosa nguvu za Mungu.
  • Mungu anatuita kuingia Kilindini cha maombi, ufunuo, kujitoa na kupokea nguvu.
  • Mambo ya siri ya kilindi cha Mungu haijafichwa kutoka kwetu lakini yamefichwa kwa ajili yetu–Ni wale wako tayari kufanya safari ya kwenda mpaka Kilindi chake Mungu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

3 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

6 days ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

6 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

6 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

2 weeks ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

1 month ago