MFULULIZO: MATENDO YA ROHO MTAKATIFU
UJUMBE: KITI CHA DIRISHANI
SOMO: MATENDO YA MITUME 20:7-12
Ujumbe huu ni kwa wale walio na tabia za ulimwengu, lakini ni watu wa kanisa. Ujumbe huu wa leo ni Baraka na onyo kwa wanao lala kanisani wakati wa ibada na zaidi wakati wa ujumbe.
Ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma, Jumapili. Mitume wa Yesu walianza kwenda ibada siku ya Jumapili kwa maana Jumapili ndio siku Yesu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu.
Ndio siku Roho Mtakatifu alishuka kanisa la kwanza lilipozaliwa.
Ndio siku Kristo alinyakuliwa kwenda Mbinguni.
Ndio siku ya ibada kwa wale wameokoka.
Eutiko (Eutychus) aliketi kwa kiti cha dirisha au aliketi juu ya dirisha na akalala usingizi. Dirisha ilikuwa katika orofa ya tatu.
Kanisa hili pengine halikuwa na bawabu makini au pia bawabu walilala.
Ibada pia ilikuwa ndefu zaidi mpaka usiku wa manane, kisha mpaka asubuhi yake.
Lakini kuna mahali pa kiroho paitwapo “Dirishani.”
Hebu tuone:-
- KITI CHA DIRISHANI
- Dirisha si mahali pa kuketi na kulala.
- Dirisha si mahali pa usalama bali ni mahali pa upepo na mwangaza.
- Kiroho kuna wakristo wa dirishani leo kama jinsi Eutiko aliyeketi mahali hatari- kiti cha dirishani.
- Kuna weza kuwabna sababu kadha za kuketi dirishani:-
- Kwamba chumba kilijaa watu, hivyo mahali palikosa.
- Pengine kulikuwa joto hivyo Eutiko alihitaji hewa safi.
- Pengine Eutiko alikuwa amechoka na mambo ya kiroho, alikuwa mbali na Mungu na Roho Mtakatifu.
- Kiti cha dirishani ni hali mtu anaweza kuwa ndani ya kanisa na pia ndani ya ulimwengu.
- Kiti cha dirishani ni hali ya kurudi nyuma na kupotea kabisa- Waebrania 10:39.
- Kunao watu wa kuteketea na kupotea. Leo katika makanisa mengi kunao roho ya kupotea. Watu wanao taka uponyaji, miujiza, ustawi, lakini bila kujitoa.
- Hawa watu ikiwa ni wakati wa kupokea Baraka, wako mbele ya wengine lakini kujitoa, utakaso wako mbali sana.
- Hawa watu wanakojoa sana Jumapili, wanapokea simu, wanaitwa nje mara kwa mara, ni watu wa internet na mitandao ya jamii katika ibada.
- Kiti cha dirishani wanaoketi pale ndio wanaona sana shida za kanisa, ndio wanaona kwaya haikuimba vizuri, mhubiri alizidi saa.
- Kiti cha dirishani mtu anaona yale aliyoacha duniani na wapenzi wa kitambo.
- Mioyo na akili zao zimejaa mafikra ya sinema na vipindi vya T.v- Waefeso 4:27.
- EUTIKO HAKUWA NA MPANGO WA KUANGUKA- Waebrania 2:3
- Lazima kila mtu kulinda wokovu wake.
- Eutiko maanake ni bahati au mtu mwema.
- Kama jinsi Eutiko wewe pamoja nami tumeonewa huruma, kibali cha Mungu- lakini tusipolinda wokovu tutapoteza.
- Kwa nini Eutiko alianguka mpaka kifo?
- Alipoteza hamu ya mambo ya Mungu.
- Alikuwa nje kuliko ndani ya kanisa.
- Usiku wa manane ni wakati wa maana sana.
- Usiku wa manane Malaika wa kifo na mauti alipita juu ya Misri, akawaua wazaliwa wa kwanza wa watu na wanyama.
- Usiku wa manane Bwana Arusi alitokea kuwapata wanawali wamelala!
- Usiku wa manane Paulo na Sila walifunguliwa gereza.
- Usiku wa manane ni wakati wa kuchagua.
- Kiti cha dirishani si mahali pa raha.
- Leo ni ombi langu wanaoketi dirishani watajipatia viti ndani ya nyumba ya Mungu na kuhusika katika kazi ya Bwana.
- Kila Eutiko amepata Baraka za Mungu lakini ukianguka na kufa, pengine Paulo hatakuweko kukufufua!!
- Je, leo utaondoka kutoka kwa dirisha yako?
- AMKENI KANISA- Warumi 13:11-12
- Kanisa lahitaji kuamka kutoka kwa usingizi na kuona kinachoendelea duniani.
- Maneno ya mwisho ya Yesu Kristo- Mathayo 25:5- “Hata Bwana Arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi”- Warumi 13:11-12; Waefeso 5:14.
- Sura moja imetengwa na Biblia juu ya kanisa kulala- 1st Wathesalonike 5:1.
- Lazima kujua wakati tunaoishi.
- Kanisa limelala ni kama wakati wa Sodoma na Gomorra wakati wa Lutu.
- Wahubiri wengi wamelala- Isaya 56:10.
- Tumeshindwa kutambua sisi ni watoto wa Nuru.
- Tunahitaji kuwa macho kwa nyakati na majira- 1st Wathesalonike 5:2-8.
- Tunahitaji kuwa na imani timilifu- Marko 11:22.
- Tunahitaji kuwa na upendo ndani ya mioyo yetu.
- Tunahitaji kuwa na tumaini, kufahamu Kristo yuaja upesi.
- Tunahitaji kuamka na kutumikiana mmoja kwa mwenzake- 1st Wathesalonike 5:9-11.
- Tunahitaji kila mmoja katika mwili wa Yesu Kristo- Matendo 2:42.
- Tunahitaji kuamka na kuwatumikia watumishi wa Mungu- 1st Wathesalonike 5:12-13.
- Tunahitaji kuwatumikia watumishi wa Mungu walio wa kweli.
- Tunahitaji kufurahi na kuomba na kutoa shukrani kwa kanisa- 1st Wathesalonike 5:17-18.
- Shetani hapendi furaha.
- Furaha inatupa nguvu- Nehemiah 8:10.
- Hivyo tupate kuamka- Waefeso 5:14.
MWISHO
- Je, umekuwa kama Eutiko kulala kanisani?
- Je, furaha ya Mungu ndio nguvu zako?
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.