Categories: Swahili Service

KUGUZWA UPYA

MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 10:1-21

 

Leo tunajifunza jinsi ya kupokea uguzo mpya kutoka mbinguni. Hakuna chochote kimeandikwa kinyume juu ya maisha na huduma ya nabii mkuu Danieli na manabii wachache tu katika Biblia wasiokuwa na lawama. Danieli aliishi katika mazingira mabaya sana maisha yake yote. Maadui walikuwa wengi sana juu ya maisha yake.

Pamoja na kuishi katikati ya maadui wengi hivi, Danieli aliamua na kuazimu kuwa yeye ataishi karibu na Mungu maisha yake yote.

Danieli alichukuliwa mateka kutoka nchi ya Israeli-Yuda nchi ya kuzaliwa bado kijana mdogo pengine miaka 12-14. Danieli alijikuta Babeli, maili 1,000 (kilomita 1,600) kutoka Israeli. Mfalme Nebukadreza aliwachagua vijana wa Israeli wenye hekima, sura na maarifa hili wafundishwe elimu yote ya Babeli.

Mfalme Nebukadreza aliazimu kuwalea hawa vijana wa Yuda kulingana na njia na maarifa ya wa Babeli.

Danilei pamoja na rafikize watatu walikataa kula chakula na divai ya mfalme. Mungu alikuwa mwaminifu kwao mpaka hawa vijana wakawa hodari zaidi, afya zaidi, hekima zaidi na maarifa zaidi kuliko vijana wote wa Babeli.

Katika mlango wa tano wa Danieli, mfalme Belshazzar, mfalme wa Babeli aliandaa karamu kuu-wakalewa wote, wakanywa pombe zao na viwekwa wakfu vyombo vya Mungu wa Israeli, ndiposa kidole cha Mungu kiliandika juu ya ukuta wa nyumba ya mfalme, “Mene mene, Tekeli, Persi-Ufalme wako umegawanwa na kupewa wengine.”

  • Hakuna mtu awaye yote angeweza kutafsiri isipokuwa Danieli. Danieli alikuwa na uongozo wa Mungu juu ya maisha yake.
  • Mungu alimwokoa Danieli katika tundu la simba (mlango 6).
  • Sasa katika Danieli 10, Danieli nabii mkuu, umri wake pengine miaka 95, Danieli aliona mbinguni, alipata uguzo mpya.
  • Danieli amekuwa mtu wa maono, ndoto, Ufunuo na miujiza katika maisha yake yote, sasa akiwa miaka 95, bado Danieli anahitaji kuguzwa upya na mkono wa Mungu.
  • Je, wewe na mimi tunahitaji kuguzwa upya leo? Je, umeishi katika mto wa kutoamini? Je, umesononeka katika moyo wako? Je, umeishi katika ukiwa? Je, unajua jinsi ya kupokea upya nguvu za Mungu?
  • Danieli leo anatufunza jinsi tuwezavyo kupokea nguvu mpya, kwa kuguzwa tena upya na mkono wa ajabu wa Mungu. Hebu tuone:-

NI LAZIMA TUTAMANI KUPOKEA NGUVU ZA MUNGU KWA KUGUZWA TENA NA MUNGU-Danieli 10:2-3.

  • Katika vifungu hivi tunaona umuhimu wa maombi na pia kufahamu nguvu za kiroho ambazo zinapingana na watu wa Mungu katika ulimwengu usioonekana wa kiroho.

Ni lazima kuomba kwa nguvu zaidi na kwa ushupavu mwingi-Vs. 2-3.

  • Kufunga saumu ni njia ya maana sana katika maisha ya Mkristo wa kweli.
  • Kufunga kwa kweli kunaletwa na mzigo wa kiroho.
  • Kufunga kwa kweli kunaletwa na moyo na roho iliyovunjika mbele za Mungu.
  • Tamaa ya chakula na vinywaji inaondolewa na ule mzigo wa roho juu ya maisha yako.
  • Tamaa ya maombi inakuwa na nguvu zaidi juu ya tamaa ya chakula na raha zote.
  • Danieli alifunga kwa majuma tatu (21 days).
  • Danieli alikuwa amemwona Mungu akimshindania hapo mbele.
  • Lakini sasa mbingu zilikuwa kimya, Danieli hakujisifia ushindi wa miaka iliyopita, sasa Danieli anaomboleza, kuomba na kufunga.
  • Danieli alikuwa akiomba katika kipindi cha pasaka na sherehe za mikate isiyotiwa chachu.
  • Karamu hizi mbili zatukumbusha jinsi Mungu aliwakomboa Israeli kutoka utumwa wa Misri (miaka 400).
  • Huu ulikuwa wakati wa Israeli kufurahi kula na kunywa na kuomboleza mbele za Mungu!!
  • Wengi wetu tumeona ufufuo hapo mbele, wengi tumetembea na Bwana miaka, lakini leo tunahitaji upako mpya na kuguzwa upya na Mungu.

Ni lazima kuomba na maono ya Mungu-Danieli 10:12-13; 20-22.

Kucheleweshwa si kukatazwa (Delay is not denial)-Vs. 12-13.

  • Ni lazima kumngojea Mungu mpaka kupokea majibu.
  • Wakati mwingine majibu kwa maombi yetu inachukua wakati.
  • Danieli alipoanza kuomba, Mungu alianza kumjibu.
  • Jibu lilikuwa njiani, hakuna pingamizi mbinguni.
  • Tunapoingia katika maombi ya kufunga, tunaingia katika daraja ya juu zaidi kiroho.

Kucheleweshwa si kushindwa-Vs. 20-21; 12:1-4.

  • Tutashinda kibinafsi-Vs. 20-21.
  • Tutashinda kiunabii-Danieli 12:1-4.
  • Tutashinda kwa nguvu nyingi zaidi (Yuda 8; 1 Wathesalonike 4:16; Ufunuo 12:11).
  • Tunasoma kwamba Michaeli ndiye amri jeshi wa majeshi ya mbinguni.
  • Michael (Mikaeli) alipofika ndiye alimshinda mfalme wa Uajemi.
  • C.H Spurgeon alisema “Mungu anapotaka kufanya kazi kuu, anaanza na kuwaweka watu wake kwa maombi.”

Mwaka wa 33AD mji wa Yerusalemu, muinjilisti asiyesoma, mvuvi samaki alihubiri mpaka watu 2,000 wakaokoka. Jina lake lilikuwa Petro.

  • Petro alipata ushindi kwa sababu watu 120 walikuwa katika maombi katika chumba cha juu!!

Mwaka wa 1,700, India, Missionari William Carey, fundi wa viatu alienda India kutoka Europa, aliishi India miaka 42, alitafsiri Biblia kwa lugha 25.

  • William Carey ndiye baba wa missions siri ya kufaulu kwani alikuwa ni dada yake kiwete mle England. Kiwete huyo aliomba kila siku, alipokea maombi kutoka India kila siku, akamwombea nduguye William Carey.
  1. Mwaka ulikuwa 1,830, mji wa Richester N.Y.
  • Muinjilisti Charles Finney aliwaokoa watu 10% ya mji. Siri ilikuwa Charles Finney alikuwa na muombaji kwa jina lake Able Clarey.

2. Mwaka ulikuwa 1872, mji ni London England. Mhubiri alikuwa kiongozi wa YMCA kwa jina D.L Moody. Watu waliokolewa kila siku.

  • Siri yake ilikuwa mwanamke mkongwe kwa jina Mary Ann Adler alikuwa mwombaji hodari katika huduma ya D.L Moody.

3. Mwaka ulikuwa 1934, Mji ni Charlotte N. C. Mhubiri Mordecai Ham, alihubiri mpaka kijana wa mkulima akaokoka, kijana huyo ndiye Billy Graham.

  • Siri ilikuwa babaye Billy Graham alikuwa na kikundi cha maombi shambani kwake. Kikundi hiki cha maombi kilikuwa kikundi cha wafanya biashara.

4.Mwaka ulikuwa 1949, mji wa Los Angeles, kijana alianza kuhubiri kwa nguvu sana. Kijana huyo alitoka mji wa Charlotte N. C. jina lake Billy Graham. Siri ilikuwa maombi ya watu wengi. Hapo ndipo Billy Graham Evangelistic Association ilianza.

MAONO YETU YA YESU KRISTO NDIYO MWANZO WA KUGUZWA UPYA NA MUNGU-Danieli 10:4-9.

Utukufu wa Yesu Kristo-Vs. 5; Ufunuo 1:12-15.

  • Yesu alikuwa anavaa katani nyeupe, ishara yake ni utakatifu. Tunachosokota katika wakati ndicho tutavaa mbinguni milele.

Dhamana yake Yesu Kristo.

  • Yesu pia alivaa mshipi wa dhahabu. Yesu ni wa dhamani sana!!

Ukamilifu wa Yesu Kristo-Vs. 6.

  • Yesu, mwili wake ni kama zabarajadi safi (crystallite).

Ukuu wa Yesu Kristo-Vs. 6.

  • Uso wa Yesu Kristo ni kama umeme.
  • Yesu anataka tumuone kwa jinsi alivyo leo.
  • Yesu ni Bwana wa utukufu.
  • Yesu atarudi tena kama umeme.

Utimilifu wa Yesu Kristo-Vs. 6.

  • Macho yake ni kama miale ya moto.
  • Kwa macho yake Yesu Kristo alimwona Danieli popote pale.
  • Yesu anaelewa na mahitaji yetu yote.

Sababu yake Yesu Kristo-Vs. 6.

  • Yesu Kristo ndiye hakimu-mikono yake na miguu yake ni kama shaba.
  • Mara ya kwanza alikuja kama Mwokozi, Mara ya pili Yesu anarudi kama hakimu.

Nguvu za Yesu Kristo-Vs. 6.

  • Sauti ya Yesu Kristo si kama sauti ya mtu, lakini sauti ya makutano.

Haya maono ya Yesu Kristo kwa Danieli yalim’badilisha Danieli kabisa (Ezekieli 1:26-28; Matendo 9:3-9; Ufunuo 1:13-17). 

USHINDI WETU KUTOKA KWA YESU KRISTO UNALETA UGUZO MPYA WA MUNGU-Danieli 10:10-21.

Uguzo mpya utatuweka juu ya magoti-Vs. 10-11.

  • Kupiga magoti ni picha ya kumtafuta Mungu.
  • Ukitaka uguzo mpya kutoka kwa Mungu ni lazima kumtafuta Mungu.
  • Ni juu ya magoti yetu tutakapopata ushindi kiroho, kimwili, ki hisia, kimawazo.
  • Tutaamishwa kutoka hofu zetu mpaka imani timilifu tutakapokuwa juu ya magoti yetu.

Uguzo mpya utatufanya kuinamisha nyuso zetu-Vs. 9-15.

  • Kuinamisha nyuso zetu ni picha ya kunyenyekea na kujisalimisha kwa Mungu.
  • Danieli aliinama, baadaye alimtazama Yesu Kristo.
  • Danieli alipoona uso wa Yesu Kristo ndipo alipata nguvu mpya.
  • Yesu Kristo alimguza Danieli kujifananisha naye. Pia kule kuguzwa na Yesu Kristo ni upendo wa Yesu Kristo kwa Danieli.
  • Yesu alipokuwa duniani aliwaguza wale hawapendwi na mtu yeyote.

Uguzo mpya utatusimamisha juu ya miguu yetu-Vs. 18-19.

  • Mungu anatuleta chini hili atuinue juu.
  • Shetani anatuleta chini tukae chini.
  • Uguzo wa Mungu utatuinua kutoka magoti yetu, mpaka uso, mpaka miguu, hii ndio picha ya kumsimamia Mungu.

MWISHO

  • Je, ni lini utaomba na kufunga?
  • Je, ni lini utaazimia kabisa kumtafuta Mungu wako?
  • Je, ni lini wewe utakuwa na maono ya Mungu, maono ya mbinguni, maono ya Mwokozi wako Yesu Kristo? Je, ni lini?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago