Categories: DANIELSwahili Service

MAANDIKO JUU YA UKUTA

DANIELI 5:1-31

UTANGULIZI

Mungu amenena nasi kwa njia nyingi. Lakini zaidi Mungu amenena kupitia kwa Yesu Kristo na kwa neno lake. Katika Danieli 1-4, Nebukadneza alikuwa mfalme wa Babeli. Alitawala kwa miaka 40 (605-562 Bc) . Baadaye Amel-marduk (563-561 Bc), Neriglisser (560-556BC), Nabonidus  (556-539 Bc).Nabonidus alikuwa mwenda safari sana, hivyo akatawala pamoja na mwanaye  Belshaza (553-539 Bc) Kutoka Nebukadneza mpaka Belshaza ilikuwa miaka 25. Kila moja wetu ako na usiku wa mwisho, kupumua kwa mwisho, neno la mwisho. Kila moja wetu anapimwa katika mizani ya Mungu kila siku. Belshaza alifanya dhambi dhidi ya  Nuru aliyekuwa nayo (He sinned against the light) V.22                “EE Belshaza hukujinyenyekeza  moyo wako       ijapokuwa ulijua hayo yote” Belshaza alipewa nafasi nyingi kuokoka, Danieli 4:27-34. Leo wengi wetu tunafanya dhambi kinyume na ufahamu wa kweli. Belshaza alifanya makosa mengi sana. Baba yake Nabonidus alikuwa safarini Arabia.

Hebu tuone:-

I.  KARAMU ILIKUWA KUBWA ZAIDI (5:1-4)

  1. Karamu kubwa sana (v.1)
  2. A)Belshaza aliona baba yangu yuko mbali, hivyo tupange karamu na kuwaita wote kusherekea.
  3. B)Pombe ilikuwa nyingi pamoja na mambo yanayo enda pamoja na pombe.
  4. Pombe haina mwalimu (2-4)
  • Pombe ni chanzo cha shida nyingi duniani.
  • Belshaza aliviagiza vyombo vya dhahabu, navyo ni vya Mungu.
  • Vyombo hivi vilikuwa wakfu, takatifu na sifa kwa Mungu wa Mbinguni.
  • Baba yake Nebukadneza hakuvitumia vyombo hivi.
  • Belshaza alifahamu yote– lakini pombe.
  • Belshaza alikuwa anaonyesha kila mtu kwamba hana heshima kwa vitu vya Mungu– Kuasi.
  • Belshaza alikuwa kipovu kiroho, hakupambanua (I Wakorintho 11:29-31)
  • Vitu vinavyo wekwa wakfu kwa Mungu ni vyake Mungu (II Wakorintho 4:3-6)
  • Miungu ya dhahabu, fedha na shaba ilikuwa maana kwa Belshaza kuliko Mungu wa mbinguni.
  • Belshaza alijiinua juu ya Mungu wa Mbinguni.

II.  MAANDIKO JUU YA UKUTA (5:5-9)

  1. Mungu alivunja karamu yao (5-6)
  • Mungu alitokea ghafla, naye akayaandika.
  • Uso wa mfalme ukambadilika, fikira zake zikamfadhaisha, viuno vyake vikalegea, magoti yake yakagongana, akalia sana.
  • Babeli ilikuwa imestawi sana, chakula, mali, ulinzi. Mioyo yao ilikuwa imenona sana.
  1. Wachawi, wanganga, wakaldayo na wenye hekima hawakuweza kutafsiri maandiko juu ya ukuta!!
  2. Je, maandiko ya Mungu juu yako yanasema nini? Maandiko juu ya Kenya!
  3. Belshaza alikataa kutubu dhambi zake, mbali aliwaendea wachawi! (2 Mambo ya Nyakati 7:14)

III. MALKIA MWAMINIFU (5:10-16)

  1. Danieli hakuwako kwa ile karamu.
  • Watu wa Mungu si watu wa karamu za dunia hii.
  • Watu wa Mungu si watu wa kwenda “Bashi” za mapepo.
  • Watu wa Mungu hawapatikani katika sherehe za pombe, ngoma na danzi
  • Hata wakialikwa wanakaa mbali (I Petro 3:12)
  • Baadaye Danieli aliitwa kwa mfalme, Danieli alikuwa tayari (2 Tim.2:15, Tito 3:1, I Petro 3:15) (Share, Care, Love)

IV.  TAFSIRI YA KWELI (5:17-30)

  1. Danieli akajibu (17-24)
  2. A)Danieli kwanza alihubiri.
  3. B)Danieli alisema ukweli mtupu.
  4. C)Danieli– sitaki zawadi zako, dhawabu zako mpe mtu mwingine!! (Danieli hakuwa mkenya)
  5. D)Danieli alimweleza mfalme kwamba alikuwa pale kumwakilisha Mungu wa mbinguni.
  6. E)Danieli– wewe mfalme ulikuwa na kiburi, ubinafsi na mjinga.
  7. F)Daniel– wewe mfalme umefanya dhambi dhidi ya nuru uliyepewa na Mungu.
  8. G)Danieli– wewe mfalme ulijua vyema kabisa (v.22) Luka 12:48, Mathayo 11:20)
  9. H)Danieli– wewe Belshaza ulijiinua juu zaidi ya Mungu wa Mbinguni (Pumzi yako, Njia zako ziko mikononi mwa Mungu)
  10. MENE, MENE (Numbered, Numbered) Umehesabiwa, umehesabiwa. Belshaza– wakati wako umekwisha- “Kila mtu atatoa hesabu yake mwenyewe”
  11. TEKELI– Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka (v.27). Unaweza fikiri wewe ni mtu wa maana sana kumbe !
  12. PERESI- “Ufalme wako umengawanyika nao umepewa wamedi na waajemi” (v.28)
  • Usiku huo (13 Octoba 539 BC!) V.30
  • Usiku huo Belshaza alikufa na ufalme ukaanguka

 

MWISHO

  • Kuna usiku wa mwisho kwa kila moja wetu.
  • Kuna pumzi ya mwisho kwetu zote.
  • Kuna neno la mwisho kwa kila mwenye mwili.
  • Kila mtu anapimwa kila siku mbele ya Mungu
  • Mizani yako inasema nini?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

2 days ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

2 days ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

2 days ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

6 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago