MAISHA YA IMANI- Waebrania 11:8-19

UTANGULIZI

Je, umewahi kufikiri jinsi mtu anapata kibali mbele ya Mungu ? Je, ni kupitia dini ? Kwenda kanisa ? Kushika Torati na Amri kumi ? Utumishi wake ? La, kuna njia moja pekee ya kumpendeza Mungu, Imani katika waebrania 11:6, “Lakini, pasipo Imani haiwezekani kumpendeza”. Kuna njia mbili za kuishi, kwa kuona, na kwa Imani. Wengi duniani wanaishi kwa kuona. “Kuona ni kusadiki” “Believing is seeing” lakini, wampendao Mungu wanaishi kibibilia, wanaishi kwa Imani.

Jumapili iliyopita tuliona Imani ya kweli ina Abudu Mungu-Habili, Imani ni Kutembea na Mungu-Henoko, Imani inamtumikia Mungu-Nuhu. Leo, hii tutaona mambo matatu yanayo changia maisha ya Imani katika maisha ya       Ibrahimu (11:8-19)

Hebu tujifunze:-

I.  KWANZA, IMANI YA KWELI NI UTII.(V.8)

  • Maisha ya Imani yanaanza na kutii sauti ya Mungu akuitapo na kuacha maisha ya dhambi.
  • Kwa Imani Ibrahimu alipoitwa, aliitika, atoke, aende mahali atakapopata urithi.
  • Ibrahimu aliondoka, akenda asijue aendako.
  • Mungu alimwita Ibrahim atoke na kuacha upangani na ibada za sanamu-Aingie katika uhusiano na Mungu.
  • Mungu hakumwita kuhubiri, hau kutenda kazi fulani, lakini kwanza-uhusiano.
  • Maisha ya Imani yanaaza tunapo acha mahali pa dhambi na kutoamini.
  • Imani ya kweli inatuelekeza kuchukua hatua.
  • Ibrahim alikuwa na umri wa miaka 75 alipoaza maisha ya Imani– safari ya kwenda inchi ya ahadi.
  • Ibrahimu aliacha ushuhuda wa mtu wa Imani.
  • Kwa wengine hapa, Mungu anawaita kuacha maisha ya dhambi na kumfuata Mungu katika utii wa Imani

 II.  IMANI YA KWELI NI KUGOJA (11:9-16)

  • Imani ni Subra na Subira na kutazamia kwa kugoja
  • Maisha ya Imani kwa Ibrahimu haikwisha kwa kuacha inchi yake Uru . (V.9-10)
  • Ibrahimu alipofika Kanaani, aliishi kama mgeni, katika hema, hivyo Isaka na Yakobo, walishiriki katika Imani.
  • Dunia si mahali kwetu, Kwetu ni Mbinguni tuendako, hivyo usikae starehe (I Petro 2:11)
  • Lengo na shabaha ya Ibrahim haikuwa Kanaani, bali alitazamia mji wa kudumu, mji wa milele ambaye mwenye kujenga ni Mungu.
  • Ibrahimu aligoja kwa subira ahadi, alikufa kabla hajaipata– lakini alikufa akitazamia.

 

 

  • Lakini wakati wa kugoja si wakati wa kupoteza (V.12-16)

 

III. TATU, IMANI YA KWELI NI KUTOA DHABIHU (11:17-19)

  • Imani ya kweli lazima kutoa dhabihu na sadaka.
  • Ibrahimu alimtoa mwana wake Isaka kama dhabihu ya kuteketezwa kwa moto.
  • Isaka alikuwa mpendwa namba moja katika maisha ya Ibrahimu.
  • Ni kitu gani muhimu sana dani ya maisha yako ? Je , Familia, fedha, nyumba, shamba, gari, sura ?

 

MWISHO

¨ Imani ya kweli ni utii, kugojea, kutoa

¨ Je, umeanza safari ya Imani ?

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

1 day ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

1 day ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

1 day ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

5 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago