Categories: Swahili Service

MAJIRA YAKO YATAPAMBAZUKA.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI

SOMO: ISAYA 58:8-9.

 

Majira kupambazuka ni wakati Mungu anachukua nafasi juu ya vita vyako, wakati Mungu anapata kukuinua na kuonyesha utukufu wake katika maisha yako.

Kunafika wakati katika safari ya maisha, wakati Mungu anaviondoa vikwazo na vizuizi njiani mwako. Huu ni wakati Mungu anavunja kila ngome mbele zako hili matokeo uliyotazamia kwa muda mrefu yanaanza kudhihirika wazi kwa kila mtu.

Huu ni wakati Mungu anakupitia mwendo wa kasi (speed) kufanya na kufaulu katika mambo yaliozuiliwa kwa miaka mingi.

Mungu wetu (YEHOVA) ni Mungu hodari katika kugeuza kifungo chako, kukufanya upambazuke katika kila eneo ya maisha yako.

Mungu anapotangaza majira ya kupambazuka kwako mbingu inaruhusu mabadiliko makuu, kupandishwa, maonyesho ya utukufu wake juu ya maisha yako.

Kwa watu wengi hapa leo, kuchelewa na vita ambayo umepitia ndio ishara kwamba mapambazuko na majira yako imefika.

Ujumbe huu wa leo ni tangazo kwako kwamba majira na msimu wa mapambazuko yako yamewadia. Hebu tutazame:-

MUNGU NDIYE BWANA WA MAPAMBAZUKO.

  1. Mungu anatembea mbele ya watu wake kuwatengenezea njia-Mika 2:13.
  • Mungu wako ndiye Yehova, anapenda sana ukapenye, anakuongoza ukatoke katika vikwazo vyote.
  1. Mungu ndiye hodari wa mapambazuko-Isaya 58:8.
  • Nuru yake inapoaangaza hatima yako inaonekana wazi.
  1. Bwana anapuuza mipango na itikadi zote na kukupandisha-Isaya 43:19.
  • Mapambazuko yako yanapita fahamu zote za mwanadamu.
  • Mungu anafungua milango na hakuna anayeweza kufunga-Ufunuo 3:8.
  • Mungu anapotangaza majira yako ya kupambazuka, hakuna nguvu zozote zinaweza kusimamisha.
  • Wana wa Israeli walipitia bahari ya Shamu-Mungu aliwatengenezea njia mahali hapana njia-Kutoka 19:21-22.

ISHARA MAJIRA YA MAPAMBAZUKO IMEWADIA.

  1. Mungu anatetemesha mambo ya kawaida-Matendo 16:26.
  • Mungu anatetemesha mambo ya dunia na mipango ya watu hili alete mambo mapya ndani ya maisha yako.
  1. Hali ya kuchelewa inaanza kupinduliwa-Danieli 10:12-13.
  • Mambo yaliyofungwa yanafunguliwa.
  • Milango ya mbingu inaanza kufunguliwa.
  • Maombi ya tangu kitambo yanaanza kujibiwa-Ezekieli 1:1.
  • Ufunuo, kibali na kutembelewa kunaanza kuwa dhahiri zaidi.
  1. Mambo yaliyosimama yanafunguliwa.
  • Mambo yaliyokataa kuamka yanainuka-Yohana 5:8-9.
  • Mfano mzuri ni Yusufu mle Misri, baada ya miaka gerezani mambo yalipambazuka mara moja-Mwanzo 41:14-40.
  • Yusufu aliamishwa kutoka gereza mpaka ikulu ya Farao. Kwa masaa 24, mambo yalibadilika.

MAMBO YANAOHARAKISHA MAJIRA YA MAPAMBAZUKO YAKO.

  1. Maombi ya nguvu yanaharakisha majira ya mapambazuko yako-Yakobo 5:16-18.
  • Maombi yanaharakisha majibu yanayoleta mapambazuko.
  1. Utii kwa Mungu unaachilia baraka za Mungu kwako-Isaya 1:19.
  • Kila majira ya mapambazuko yanaanza na amri. Ni lazima kutii hiyo amri.
  1. Imani timilifu ndani ya ahadi za Mungu na kuamini kwamba yote yanawezekana kwa Mungu-Waebrania 11:6.
  • Imani ndio mkono unapokea miujiza yako kutoka mbinguni.
  1. Ibada na sifa inavutia uwepo wa Mungu kwako-2 Nyakati 20:22.
  • Kuta za Yeriko zilianguka kwa sababu ya shwangwe za ibada na sifa-Yoshua 6:20.
  • Kwa sababu ya utii, ibada na sifa, yasiowezekana yalitimia.

BARAKA ZINAZOFUATA MAJIRA YA MAPAMBAZUKO.

  1. Urejesho wa chochote kilichopotea, kuibiwa na kuaribiwa na adui zako-Joeli 2:25-26.
  • Kilichopotea kinarudishwa kwako pamoja na faida wakati wa majira ya mapambazuko.
  1. Urejesho unapokuja mara hio unaanza kuonekana, kutambulika na kukubalika-Esta 2:1
  • Mara moja tu dhamana yako inaongezeka na kuonekana na watu. Sauti yako inasikika na kukubalika na watu wote.
  1. Mungu anakupatia mwendo wa kasi zaidi (speed) na kuchelewa kwako kunaondolewa kiasi unafikia hatima yako kwa kasi-1 Wafalme 18:46.
  • Mambo yanayochukua miaka mingi kufanya, wewe unafanya kwa miezi au wiki.
  1. Ahadi zilizochukua miaka zinatekelezwa na kuafikia mara moja-Mwanzo 21:1-3.
  • Neno na ahadi za Mungu zinatimia mara moja.

MWISHO

  • Majira ya kupambazuka ni wakati ule Mungu anaingilia katikati ya vita vyako, wakati Mungu anakuinua na kuonyesha utukufu wake.
  • Huu ndio wakati wa majira ya kupambazuka kwako.
  • Jiweke tayari kupitia maombi, utii na imani na utaanza kuona ishara ya mapambazuko yako.

OMBA

  • Bwana wangu, achilia nuru ya mapambazuko yako kama jinsi nuru ya asubuhi.
  • Kila kuta za vizuiizi mbele zangu, vunjika sasa, katika jina la Yesu Kristo.
  • Bwana achilia majira ya mapambazuko yangu leo, nipe neema ya kutambua majira ya kupambazuka kwangu, katika jina la Yesu Kristo.
  • Kila hali ya kuchelewa ndani ya maisha na jamii yangu, shindwa sasa katika jina la Yesu Kristo.
  • Ninatangaza majira ya kupambazuka kwangu, katika jina la Yesu Kristo.
  • Bwana washa utukufu wako uonekane kwangu na nuru ya wema wako inifuate katika jina la Yesu Kristo.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

2 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

6 days ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

6 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

6 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

2 weeks ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

1 month ago