MANASE – BWANA NDIYE MUNGU

II MAMBO YA NYAKATI 33:1-17

UTANGULIZI

Mungu anaweza kumwokoa yeyote yule. Neema ya Mungu inawafikia wote walio karibu na walio mbali sana kama mfalme Manase wa Yuda. Musa alikuwa muuaji, Daudi alikuwa muuaji – msherati, Rahabu alikuwa kahaba, Mariamu Magdalene alikuwa mwenye pepo saba. Ibrahimu alikuwa mwabudu sanamu, Yakobo alikuwa mdanganyifu, Paulo alikuwa mpinga Kristo na wewe na mimi tulikuwa mbali na Mungu wetu (Waefeso 2:13-22)

Hebu tuone jinsi neema ya Mungu ilivyo:-

I.   UTAWALA WA MANASE (II MAMBO YA NYAKATI 33:1-6)

  1. Manase alimkataa Mungu kabisa
  • Alijenga tena madhabahu ya shetani aliyoyabomoa baba yake Hezekia (V.3)
  • Alijenga tena madhabahu ya mfalme Ahazi (V.3)
  • Aliabudu jeshi lote la mbinguni na kulitumikia (jua, mwezi na nyota) (Waefeso 2:2-3) V.3
  • Alijenga sanamu katika nyumba ya Mungu V.3
  • Aliwapitisha watoto wake katika moto kama kafara ,katika mikono ya moto ya sanamu ya Molochi .
  • Leo wazazi wanawapitisha watoto wao kwa pombe ,wanao wafundisha watoto wao uasherati,ulevi na udanganyifu.
  • Manase pia alijiusisha na ibaada kutazama bao,akabashiri ,akafanya uganga,akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi akamkasirisha Bwana.
  • Hivi ndivyo ilivyo hapa kwetu Kenya leo.

II.   KUARIBIKA KWAKE MANASE (II MAMBO YA NYAKATI 33:9-11)\

  1. Aliwaelekeza Yuda na Yerusalemu kumkataa Bwana. (V.9)
  2. Manase na watu wote wakamkataa Bwana Mungu (V.10)
  3. Mungu aliachilia Jeshi la mfalme wa Ashuru, wakamkamata Manase na wakuu ya Yuda (V.11)

III.  UKOMBOZI KWA MANASE (II MAMBO YA NYAKATI 33:12-13)

  1. Manase alipokamatwa na kuwekwa pingu na ndoana katika pua zake, Manase alimlilia BWANA.
  • Manase akamwomba Bwana Mungu.
  • Manase akanyenyekea sana mbele ya Bwana
  1. Matendo ya Mungu
  • Mungu aliyasikia maombi ya Manase
  • Mungu akamurudisha tena Yesuralemu katika ufamle wake.

IV.  WOKOVU NA MABANDILIKO YA MANASE (II MAMBO YA NYAKATI 33:15-16)

  1. Manase akaiondoa miungu migeni (V.15)
  2. Manase akaondoa sanamu katika nyumba ya Bwana na madhabahu yote aliyojenga katika milima ya nyumba ya Bwana.
  3. Manase akajenga upya madhabahu ya Bwana (V.16)
  4. Manase akatoa juu ya madhabahu ya Bwana sadaka za Amani na za shukrani akawaamuru Yuda kumtumikia Bwana, lakini watu walikataa. (V.16)
  5. Ushahidi wa kuokoka ni maisha yaliobandilika na ushuhuda wa Roho Mtakatifu ndani yetu.
  6. Manase alitawala miaka 55 katika Yuda zaidi kuliko wafalme wote wa Yuda na Israeli.
  7. Hata ingawa mfalme Manase aliokoka lakini alikuwa amechelewa sana, Manase akalala na baba zake.
  8. Amoni akatawala mahali pake Manase
  • Wakati mzuri wa kununa bima (insurance) si siku ya kufa kwako. Wakati mzuri wa kuweka vifaa vya kuzima moto si wakati nyumba inawaka moto. Wakati wa kujenga hisia nzuri juu ya utakatifu si wakati dhambi imekuja – lakini in mapema katika maisha.
  • Yusufu alichangua moyoni kutofanya dhambi ya uasharati akiwa kijana (Mwanzo 39:7-13)
  • Timotheo alifundishwa na mtume Paulo (2 Timotheo 2:22, I Wakorintho 10:13)

MWISHO

  • Manase aliokoka masaa ya mwisho kabisa, mbinguni aliingia, lakini maskini
  • Tunaokoka tukatumike mbele za Bwana Mungu na kupokea dhawabu.
  • Usingoje mpaka mwisho kama jinsi Manase
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago