Categories: Swahili Service

MAUA MATANO KATIKA UKOO WA BWANA YESU KRISTO

MFULULIZO: KUZALIWA KWA YESU KRISTO

SOMO: MATHAYO 1:1-17

 

Katika ukoo wa Bwana Yesu Kristo papo wanawake watano. Katika maisha ya hawa wanawake, tunaona neema ya Mungu kuokoa wenye dhambi. Hawa wanawake kweli ni maua yanayopendeza. Neema ya Mungu kuokoa inatufanya kuwa maua ya kupendeza mbele ya watu, vizazi juu ya vizazi. Hebu tuone hawa wanawake wa neema:-

MAUA MATANO YA NEEMA YA MUNGU

TAMARI (Thamar) V.3 Mwanzo 38:1-30.

  • Tamari alikuwa Binti mkwe wa Yuda.
  • Tamari alikuwa Mkanaani, hivyo alikuwa Myunani (Gentile).
  • Tabia yake ilikuwa ya dunia hii.
  • Kwa neema ya Mungu Tamari aliingia katika jamii na ukoo wa Mwokozi wetu Yesu Kristo.

RAHABU (Rahab) V.5- Yoshua 2:1-24.

  • Rahabu alikuwa Myunani (Gentile).
  • Rahabu pia alikuwa kahaba mashuhuri mle Yeriko.
  • Rahabu alitoka kwa watu walio chini ya laana ya Mungu kwa sababu ya uasi wao.

RUTHU (Ruth) V.5.

  • Ruthu alikuwa mtu wa Moabu, Myunani (gentile).
  • Alikuwa mjane wa Mahloni, mwana wa Elimeleki na Naomi, wazaliwa wa Bethlehemu ya Yuda wakati wa waamuzi wa Israeli.
  • Ruthu alikuwa mwanamke wa sifa, tabia yake ilikuwa tabia ya kiungu, alikuwa mwenye haki.
  • Ruthu alikuwa mwanamke mwaminifu na roho ya fadhili.
  • Ruthu alikuwa mwaminifu kwa Mungu wa Israeli, alikuwa ameokoka kwa neema kwa njia ya imani- Ruthu 1:16-17.

BATHSHEBA V. 6. 2nd 11.

  • Bathsheba alikuwa mke wa Uria, alikuwa mwanamke msherati- 2nd11:3.
  • Alifanya uasherati na mfalme Daudi mmewe Uria alipokuwa vitani.
  • Hakumwambia mmewe yaliyofanyika wala kumlinda mbele ya mfalme Daudi.
  • Alifahamu njama ya mfalme Daudi kumuua Uria lakini alimsaliti mmewe.
  • Baadae Bathsheba alifanyika mkewe mfalme Daudi na kumzaa mfalme Suleimani.

MARIAMU (Mary) V.16 Luka 1:26-38.

  • Mariamu alikuwa mwanamwali, bikira, mtakatifu.
  • Mariamu alikuwa tayari kuyafanya mapenzi ya Mungu popote pale.
  • Katika orodha hii ya wanawake watano, wanne walikuwa Wayunani (Gentile), mmoja pekee alikuwa Myahudi.
  • Watatu wao walikuwa wenye dhambi.
  • Wawili wao walikuwa wa dini.
  • Wote watano walitoka mataifa mbalimbali.
  • Wote watano walishiriki mambo mawili:-
  1. Wote waliingia kizazi na ukoo wa Mwokozi Yesu Kristo.
  2. Wote watano walikuwa wenye dhambi, walihitaji Mwokozi kwa nafsi zao- Warumi 3:23; 5:12.

BARAKA TANO!!

Kwa kutazama maisha ya hawa wanawake ni vigumu kuona maana lakini kwa neema ya Mungu waliokoka!!

Baraka zao tunaziona tunapoelewa na maana ya majina yao.

  • Majina yao yanaonyesha neema na upendo wa Mungu. Hebu tuone:-
  1. Tamari- mtende- mtende ni mti wa dhabiti na ni mti unaopeana uhai, uzima na nguvu.
  • Mtende unamea zaidi huko jangwani.
  • Yesu Kristo alipeana udhabiti katika maisha.
  • Yesu Kristo anatupa sababu ya kuishi na kurejesha mioyo inayopotea.
  • Yesu Kristo ni kijito cha maji jangwani za maisha.
  • Tunakuwa wafu bila Yeye- Waefeso 2:1.
  • Tunapata uzima tunapomwamini Yesu Kristo- Matendo 16:31; 1st Yohana 5:12.
  1. Rahabu- Maanake ni upana!! (wide, broad).
  • Neema ya Mungu ni pana, upendo wake unawafikia wote duniani- Yohana 3:16; Yeremia 31:3.
  • Neema ya Mungu ni kwa kila mtu atakaye – Warumi 10:13!! Waebrania 11:31.
  • Yesu Kristo anabadilisha maisha ya wote wamjiaye.
  1. Ruthu- maanake ni RAFIKI.
  • Yesu Kristo ni rafiki wa karibu kwa kila mtu mwenye dhambi- Mathayo 11:19.
  • Kwa upendo wake alitufia msalabani- Yohana 15:13.
  1. Bathsheba- Maanake ni “Binti anayetosha kabisa”
  • Utoshelevu wote uko ndani ya Yesu Kristo.
  • Zaburi 107:9; Mathayo 11:28.
  1. Mariamu- Maanake ni “Uasi wao” (their rebellion).
  • Katika Yesu Kristo tunapata upatanisho na Mungu.
  • Yesu Kristo anauchukua uasi wetu na kufanya utii- 1 Yohana 4:19.
  • Je, wewe umeokoka bado?

UREMBO WAO (The beauty).

Haijalishi chochote katika maisha yako leo au jana!! Haijalishi vikwazo- Yesu Kristo ni Mwokozi wako leo.

  • Yesu Kristo hajali:-
  1. Ulikotoka
  2. Ukoo wako.
  3. Daraja ya maisha yako.
  4. Dhambi zako za kale na za leo.
  5. Mipango ya maisha yako.
  6. Hali yako ya sasa.
  • Yesu Kristo anawakubali wakosa wote- Yohana 6:37.

Swali kubwa ni je, unataka kuokoka? Je, unataka kuingia mbinguni? Basi mjie Yesu Kristo sasa.

  • Hawa wanawake wote watano waliokolewa kwa neema kwa njia ya imani- Waefeso 2:8-9.

MWISHO

  • Leo kamjie Mwokozi wako.
  • Leo Kristo amekujia, tafadhali na wewe mjie.
  • Kama umeokoka tayari, mtumikie, muishie yeye aliyekufia.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago