MFALME ALIYE SIKIZA WAJINGA

I WAFALME 12:1-19

UTANGULIZI

Biblia inatufindisha kutafuta ushauri. Lakini si kila ushauri ni ushwari mwewa na wa busara. Kweli, kila mtu ni mshauri na kuna ushauri mwingi kila mahali. Lakini je, tutafahamu aje ushauri bora na ushauri mbaya? (Mithali 12:15; 15:22; 19:20) Mfalme Sulemani alikuwa mwenye hekima na moyo wa adili kuliko yeyote yule. Sulemani alikuwa mshauri wa mwanaye Rehoboamu (Mithali 1:8)ambaye alikuwa Kifungua mimba wake .Siku moja Rehoboamu alihitaji ushauri.

Mfalme Sulemani alipokufa, Rehoboamu alishika nafasi na enzi yake. Watu wa Israeli wakamjia mfalme wao mpya, yaani Rehoboamu wao wakamwambia “baba yako alilifanya zito kongwa (nira) letu, basi sasa utupunguzia utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako na lile kongwa zito alilotutwika, nasi tutakutumikia” (V.4)

Kwa hekima Rehoboamu aliwaomba watu hawa siku tatu kisha atawajibu (V.5)

Rehoboamu kwanza aliwaendea wazee, washauri wa babaye mfalme Suleimani (V.7) lakini Rehoboamu alikataa ushauri wa wazee, marafiki zake hawakuwa na hekima, bali walikuwa kiburi na ubinafsi.

Hawa vijana walimshauri Rehoboamu vibaya (V.6-11)

Hayo hayakuwa maneno ya mfalme kuwaambia watu. Maneno hayo yalikuwa ya kuvunja ufalme. Hivyo Israeli ikatawanyika na kuwa na ufalme mbili, Israeli kabila 20 na Yuda kabila mbili. Mpaka leo falme hizi mbili bado ziko mbali mbali. Hebu tujifunze:-

I.  SI KILA USHAURI NI USHAURI MWEMA

  • Zaburi 1:1-6 Mungu anatuonya tujiadhari ni nani tunashirikiana naye
  • Mungu anasema watu wa dunia ni wajiga, watu wa dunia hawataketi na wenye haki siku ya hukumu.
  • Watu wa dunia hii wasiokoka watapotea, hivyo
  1. Heri ni mtu yule asiyekwenda katika shauri ya wasio haki.
  2. Heri ni mtu yule asiyesimama katika njia ya wakosaji
  3. Heri ni mtu yule hakuketi barazani pa wenye mizaha.
  4. II Wakorintho 6:14-18 “usifungiwe nira pamoja na wasioamini”
  • Washauri wa Rehoboamu hawakupenda watu wapone, wala kuwasaidia.

II.  BASI TUMSIKIZE NANI?

  • Yesu Kristo alianza kanisa hili waliookoka wapate ushauri wa kibiblia.
  • Watu wa kwanza Rehoboamu kutafuta ushauri walikuwa wazee (I Wafamle 12:6)
  • Musa alikuwa na wazee 70 (Hesabu 11:16, 25)
  • Baadaye wazee waliketi katika kila mji kuwaamua watu (Kumbukumbu 25:7)
  • Paulo aliwashauri wachungaji vijana Timothe na Tito – Kuwatawaza wazee katika kanisa (Tito 1:6-9)
  • Wazee wanahitaji kuwa mume mwema, baba wema na viogozi wema.
  • Unapohitaji ushauri mwema unahitaji kuwatumia wazee wa kanisa.
  • Sulemani alimshauri mwanaye Rehoboamu (Mithali 3:4-7)
  • Lakini Rehoboamu hakwenda kwa kuhani, nabii hau wenye hekima (II Timotheo 1:12)

III. REHOBOAMU ALIKATAA KUWASIKIZA WATU WAKE (12:15-19)

  • Wasomi wa mawasiliano wamebuni njia za ushauri mwema. Si vizuri kuwaambia watu hau mtu habari mbaya moja kwa moja.
  • Unampongeza mtu kwanza, baadaye unaleta ushauri wako (1+1)
  • Unampa mtu pongezi mbili kwa kila ushauri moja (2+1)
  • Unampa mtu pongezi mbili kwa kila ushauri (2+2) hau pongezi mbili, ushauri na pongezi moja (2+1+1)
  • Wana wa Israeli walitawanyika, roho ya uasi iliwapata mpaka hivi leo.
  • Umoja wa ufalme wa miaka 80 ulivunjika kwa siku tatu (I Wafalme 11:42)
  • Tunaposikiza Wajinga, matokeo ni kuvunja ufalme, nyumba, ndoa, kanisa, urafiki etc.

MWISHO

  • Ukamilifu wa kuhimika hakuwezi pitishwa kijamii hau kuzaliwa. Ni vizuri kujizunguka na watu wakamilifu.
  • Je, unawasikiza wajinga? (Mithali 15:1)
  • Je umewashauri wengine vibaya wakavunja nyumba zao, ndoa na jamii?
  • Uchauguzi wa mioyo yetu unahusu watu wengine.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

4 weeks ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago