Categories: Swahili Service

MKARIBISHE MUNGU KWA KARIBU

MFULULIZO: KARIBU NA MUNGU.

SOMO: YAKOBO 4:8.

 

Kumkaribia Mungu si jambo la kufanya mara moja tu, lakini ni safari ya kuendelea kuutafuta uso wake, kwa moyo wako wote.

Kumkaribia Mungu ni moja wapo ya nidhamu za imani ya Kikristo.

Kumkaribia Mungu ni njia ya kujenga uhusiano wa karibu na Mungu kwa unyenyekevu wote, kujitoa na kujisalimisha kwa Mungu wako.

Tunapomkaribia Mungu tutapata kuhisi uwepo wake, amani yake na nguvu zake katika maisha yetu.

Ujumbe wa leo ni pamoja na kutufundisha jinsi ya kumkaribia Mungu na madhumuni ya kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu. 

Hebu tutazame:-

MTAFUTENI MUNGU KWA MOYO WA KWELI.

Jitoe kwa moyo wote-Yeremia 29:13.

  • Kumkaribia Mungu ni kumtafuta na moyo wote.
  • Shabaha ya kumtafuta Mungu ni kumjua na kumfahamu kabisa.

Kutafuta Mungu kwa moyo safi-Yakobo 4:8.

  • Kumwona Mungu ni lazima kuwa na moyo safi na mikono safi.

Maombi ya kudumu-1 Wathesalonike 5:17.

  • Maombi ni njia dhabiti ya kuwasiliana na Mungu.
  • Tunapowasiliana na Mungu, tunapata kuingia katika uwepo wake.
  • Mawasailiano yana hatua tano:-
  • Kukosa mawasiliano kabisa.
  • Kuwasiliana ukweli ulivyo-yale unayojua tu (facts).
  • Kuwasiliana jinsi unavyojisikia-hisia zako (feelings).
  • Kuwasiliana mawazo-kile unafikiria (thinking).
  • Kuwasiliana wewe ni nani-jinsi ulivyo (transparency).
  • Mungu anapenda uhusiano wetu ufike kiwango cha kuwa wazi mbele zake.

Soma neno la Mungu.

  • Tunasonga karibu na Mungu kwa kusoma neno lake, kutafakari neno lake-Zaburi 119:105.
  • Biblia inafichua hasa tabia na mapenzi ya Mungu kwa maisha yetu.
  • Mfalme Daudi alimtafuta Mungu kwa moyo wote, hata wakati wa kuanguka kwake katika dhambi-Zaburi 27:4.

UTII WA AMRI ZA MUNGU.

Utii huleta ukaribu na ufahamu.

  • Kumtii Mungu ni ishara ya upendo wetu kwake na heshima kwake.
  • Yesu Kristo alisema ikiwa tunampenda tutamtii amri zake-Yohana 14:15.

Ishi maisha ya haki.

  • Haki ni kutembea katika njia za Mungu.
  • Haki ni kuishi katika utakatifu. Utakatifu unatuvuta karibu na Mungu. Dhambi inatutenga na Mungu, lakini utakatifu unatuleta karibu na Mungu-Isaya 59:1-2.

Salimisha mapenzi ya nafsi yako kwa Mungu (self-will).

  • Kumkaribia Mungu ni pamoja na kusalimisha mapenzi ya mioyo yetu kwa Mungu.
  • Yesu Kristo alijisalimisha kwa Mungu Baba pale Gethsemane-Luka 22:42.

Tegemea mpango wa Mungu kwako.

  • Kutegemea ni mojawapo wa uhusiano na Mungu.
  • Tunapotegemea mpango wa Mungu kwetu na kutii mwongozo wake, tunapata kusongea karibu na Mungu-Mithali 3:5-6.
  • Ibrahimu alimwamini Mungu, alionyesha tegemeo lake kwa Mungu-Mwanzo 22:1-12.

ONYESHA UNYENYEKEVU NA TOBA MBELE ZA MUNGU.

Unyenyekevu mbele za Mungu.

  • Mungu anawapinga wenye kiburi.
  • Kumkaribia Mungu ni lazima kumjia Mungu kwa unyenyekevu, huku tukionyesha tegemeo letu kwake-Yakobo 4:6.

Tubu dhambi zako.

  • Dhambi ni kikwazo katikati yetu na Mungu.
  • Kuungama dhambi kunatoa vikwazo kati yako na Mungu wako na kukufungulia njia ya kumkaribia Mungu moyo safi-1 Yohana 1:9.

Kuungama na kusamehe.

  • Kuungama dhambi zetu kwa Mungu na kupokea msamaha wake kunarejesha ule uhusuano wetu na Mungu-Zaburi 51:10-12.

Kutegemea neema ya Mungu.

  • Hatuwezi kumkaribia Mungu kwa nguvu zetu, lazima kutegemea neema na msaada kuishi maisha ya haki na kumkaribia Mungu wetu-Waebrania 4:16.
  • Mwana mpotevu alinyenyekea na kutubu dhambi zake, ndiposa alipokelewa kwa upendo mwingi sana-Luka 15:18-24.

MPENDE MUNGU JUU YA VITU VYOTE.

Mpe Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako.

  • Kumkaribia Mungu kunahitaji kumweka Mungu kwanza na juu zaidi ya yote yale.
  • Lazima kumpenda Mungu na moyo wote, nafsi yote na akili zako zote-Mathayo 22:37.

Penda sana kuwa katika uwepo wa Mungu.

  • Mwandishi wa Zaburi alipenda sana kukaa katika uwepo wake Mungu-Zaburi 42:1-2.

Tenga wakati wako na Mungu.

  • Tenga wakati mzuri kukutana na Mungu wako kwa mombi, sala, kutafakari, neno na ibada-Zaburi 63:1; Waebrania 11:6.
  • Mariamu alichagua kuketi mbele zake Yesu Kristo-Luka 10:39-42.

MADHUMUNI YA KUMKARIBIA KARIBU MUNGU WAKO:

Utapokea uwepo wa Mungu.

  • Tunapo msongea MUNGU, yeye ameahidi kutusongea kwa karibu.
  • Tunapokea amani na furaha-Yakobo 4:8.

Tunapokea muongozo na mwelekeo.

  • Wale wanaotembea karibu na Mungu ndio wao wanaopata mwongozo wake, ndio wanapata njia na mapito yake-Zaburi 32:8.

Wanapata nguvu wakati wa taabu zao.

  • Kukaribia karibu na Mungu ndio kupewa nguvu, faraja na upendo wakati wa dhiki-Zaburi 46:1.

Kukaribia karibu na Mungu ni kupokea baraka na kibali.

  • Mungu anawabarikia wale wanasonga karibu naye, kibali chake kwao, na baraka zake zinawafikia wao-Zaburi 5:12.
  • Henoko alitembea karibu na Mungu, kiasi Mungu akamtwaa. Uhusiano wake na Mungu ulikuwa wa karibu zaidi-Mwanzo 5:24.

MWISHO:

  • Kumkaribia Mungu si jambo la kufanya safari moja, bali ni kumsongea Mungu kila siku, kila saa.
  • Kumkaribia Mungu ni safari ya kumtafuta Mungu wako kwa moyo wako wote.
  • Tunaponyenyekea Mungu na kupenda sana kuwa katika uwepo wake.
  • Tunamtafuta Mungu katika kila sehemu ya maisha yetu.

MAOMBI

  • Bwana, nisaidie kutafuta kwa moyo wangu wote na kukukaribia zaidi.
  • Bwana, nipe moyo safi na neema ya kutembea nawe, nipe kiu na njaa ya uwepo wako.
  • Bwana, nipe amani yako na furaha ya kutembea nawe.
  • Bwana, ninaomba kibali chako juu ya maisha yangu, ninapozidi kutembea karibu nawe.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

2 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

5 days ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

5 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

5 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

2 weeks ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

4 weeks ago