MFULULIZO: UPENDO WA MUNGU NI WA MILELE
SOMO: MALAKI 1:6-14
Mungu apendezwi na vitu ovyo ovyo. Kama ni ibada na sifa afadhali hasipokee ibada kuliko ovyo. Mpe Mungu yaliyo mema kabisa (give God Your best). Siku moja jumapili kijana wa miaka 6 alisikiza mchungaji akiubiri ujumbe mrefu, kijana akachoka sana. Kijana akamuliza baba yake ‘Je, huyu mhubiri anafanya kazi gani katikati ya juma?’ baba akamwambia kijana, “huyu mhubiri huwa na kazi nyingi, anafanya kazi ya office, anawatembelea wangojwa, anatengeza ujumbe wa kuhubiri jumapili, anafanya ushauri wakristo, halafu anapumzika, kwa maana kuhubiri ni kazi zito sana.” kijana akafikiri sana baadaye akasema “kusikiliza mhubiri si rahisi pia!!” kusikiliza si rahisi, zaidi ukiwa haupendi kusikia. Malaki 1:6-14, iliandikiwa wachungaji wa kulipwa kama mimi.
Wana wa Israeli walikuwa wamerudi kutoka babeli kwa uamisho wa miaka 70. Hekalu tayari ilikuwa imejengwa upya na ibada kuazishwa upya. Lakini hata ingawa kutoka nje mambo yalionekana shwari, pale ndani uzembe wa kiroho ulikuwa umeanza kutawala watu kama jinsi saratani (cancer). Katika hali hiyo Malaki alitokea na changamoto kwao na sisi pia, kumpa Mungu yaliyo mema zaidi (giving God the best).
Mungu anataka sisi kujua kitu moja “Mungu anatupenda”. Mungu anatupenda na upendo mkuu, upendo usio na kifani. Lakini kama jinsi watu wa wakati wa Malaki miaka 2400 iliyopita, walichukia sana upendo wa Mungu kwao. Pengine wewe pia ni moja wao.
Kwasababu ya kuchukia Mungu, ibada yao ililegea, viongozi wao walikuwa wazembe, ndoa zao ziliaribika na kuvunjika. Sadaka na zaka zao, zilikuwa hoi hoi, walikataa kutumika. Kama tutaendelea mbele katika ratiba ya kiroho ya Mungu, Mungu anasubiri tumpe yaliyo bora zaidi. Kuna njia tatu za kumpa Mungu yaliyo bora zaidi:-
I. UWE NA IMANI TIMILIFU (1:6-7) (Embrace an authentic faith)
II. MPE NAFASI YA KWANZA KWA MALI NA VITU VYAKO(1:8-9) (Give God priority over possessions)
III. FAHAMU NA TAFAKARI UKUU WA MUNGU (1:10-14) (OF GOD) (Grasp the greatness of God)
MWISHO
MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13. Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…
SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19. The journey of fulfilling your destiny does not…
SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15 Thankfulness is a great attitude…
SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5 There are levels of the anointing and each…
MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18. Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…
SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9. God has the power to…